Jamani nisaidieni-huyu dada ananipa presha.

Uzuri wa mtandao wa JF bwana ni ushauri mtu unaoweza kuupata.
Ushauri tu unaweza okoa maisha ya mtu.
Mimi ni mgeni sana JF lakini si mgeni wa maisha.
Nimepitia ukurasa huu ma mimi ninatizo linalo nisibu, tena tatizo linalonipa presha.

Mimi ni mjasiriamali mzuri tu kanda hii ya pwani.
Kuna dada ambaye kumbe ananifuatilia kwa karibu sana na kwa muda mrefu.Mwishowe akabisha hodi ofisini kwangu kama dada wa kutoka sehemu zetu huko milimani na akasema anasalimia tu.
Muda si mrefu simu zikaanza kuwa nyingi na hatimaye akaomba out.
Nisionekane mshamba masikini miye nikamtoa out. Kweli pombe mjumbe wa Ibilisi, muda si muda tukawa tunavunja amri ya sita na huyu dada akwa antaka sana kunimiliki.
Mimi nimeoa na yeye hajaolewa.
Mambo yakaendelea kwa muda kuidogo lakini nikakataa kabisa kujicommit na mabo yote ikawa kwa soksi ili isijetokea ajali ya mimba.
Nafikiri malengo ya dada yakawa hayajakamilika, na akazidi kuwa mkali kwangu kadri siku zilivyoendelea, ikiwa ni pamoja na vitisho kuwa ataniexpose kwa jamii kama nitamwacha.
Nikanwekea mtego siku moja , alipiga simu sikuipokea , lakini nikajidai mimi mke wa jamaa unyempigia.Nikamuuliza unashida gani na mume wangu maana nimesikia sauti ya kike.
Hapo yalianza matusi ya kuua mtu, matusi balaa-ati wewe ulicho nacho ndo mumeo anachofuata kwangu!
Hakika nilipigwa butwaa!
Siku ya pili nikamuuliza mbona ulibishana na mke wangu? naye akajibu, ati anajidai mjanja atanikoma mie!
Hapo ndo nikajua hapa kuna walakin na nika mwacha kwa muda mrefu.
Wanaume tuna matatizo sana, baada ya muda akanibembeleza na kulia sana, baadaye nikampeleka kinywaji tukanywa.
Punde si pundeikawa mechi tena isiyo na soksi safari hii.Bibie alifurahi sana siku hiyo, na akapotea zaidi ya mwezi.
Aliporudi akaja na stori kuwa yeye tayari.Nikamuuliz tayari nini, akaniambia mimba.
Nikachanganyikiwa kabisa lakini baada ya muda mrefu wa kufikiri nikamwambia nitamtafutia kiwanja ajenge ili mtoto asije pata taabu.
Lakini Mungu si Asumani, baada ya miezi minne kumbe mimba haikukaa na nikamuuliza vipi akaanza ukali tena ili mimba ikuzwe.Hapo nikakataa kabisa maana nikaona nimeponea tundu la sindano.
Kuona hivyo huyu bibi akawa kichaa na akaja ofsini nakutukana matusi ya mguoni , na nikaaibika sana.
Bibie akaahidi kunishitaki kanisani na kweli akaenda kumwona Mchungaji ,hata hivyo akapuuzwa kwa vile walimwona punguani.
Mambo yalipozidi kuwa mabaya akaanza kunisimamisha barabarani kwa nguvu, watu wantazama sinema na kushangaa!
Hapo ndo nikaenda fungua RB na kuwajulisha ndugu zake juu ya huyo mtoto wao.
Nilivyokuwa serious , aliwekwa ndani siku moja kwa kunibugidhi lakini ndugu zake wengine wakamwokoa na janga zaidi.

Wana JF hadithi ni ndefu lakini mwisho ndugu zake wakamkana kwa tabia yake na kusihi kutonisumbua na hii ni baada ya kuwalipa wazazi wake kifuta aibu cha kulala na binti wao(ana miaka 32).
Sijawasiliana naye(kwa maana ya kumpigia au kuongea naye) kwa zaidi ya mwaka sasa.

Lakini ka muda huo woote hadi leo ananipigia simu karibu mara kumi wiki na meseji kama kumi hadi ishirini kwa wiki ambazo sizijibu kamwe.
Kwenye simu yangu kama ushahidi nina meseji zilizofikia 831
Meseji ya mwisho imeingia kwangu kama nusu saa iliyopita.
Kwa hakika zinanichefua rohoni kupita kiasi.
Nsaidieni ndugu zangu huyu bibie anamapepo? na mnaweza nishauri nini?

lamba halafu kula kona njoo uombe ushauri tena...
 
Pole ndugu,atachoka mwenyewe,huyo sio mzima akilini ana matatizo ya saikolojia!
 
Lizzy,mwenzio kaomba ushauri bana. Mpe ushauri mbona ghafla umekuwa mkali like this na una mahasira povu linakutoka mdomoni like the woman in question? Or are U the one?
Ingekua ni mimi ningeshamlamba makwenzi ya ukweli...nwy kina dada ndo mjifunze wakati mwingine kumtokea mwanaume ni balaa tupu...siku yakichacha unaanza kuambiwa ulijipendekeza na kung‘ang‘ania kisicho chako!!
 
Wana Jf:
Jamani, is it only to me or does this story sound like the other side ya ile thread ya "Natamani kujiua....................." to anyone else?????

Majoja
Two things:
1. You better Come clean to your wife and apologise, before hajahabarishwa na bibie. Most of the time People tend to find more sincerity in an apologies offered before one's hand gets caught in the cookie jar
2. Next time try to keep it in your pants. If you know you are weak (which you obviously are), kaa mbali na wanawake! Do not befriend any nor try to take 'em out

Side note:
If you dont mind Can you advise if wewe ndiye mume discussed in the named thread above?
Nemo nakubaliana na ushauri wako.
Lakini ningependa kuweka wazi kuwa thred nyingine hapo juu nimeisoma na kuna tofauti kubwa tu.
-Mimi ni mkristo wakati kwenye thread ile mwanaume ni mwislamu
-mke wangu hajaonana wala kuongea na bibi huyu fedhuli na wala hajamsikia, hilo nashukuru Mungu

Sijaeleza hadithi yote , huyu bibie wa kwangu ni kichaa, kichaa kabisa maana anatamba kunikomoa kwa vile anatembea na waziri fulani hapa mjini.Kwa kifupi huyu dada ni mchokozi na mn'gang'aniaji wa hali ya juu, wakati tabia yake si nzuri.
 
Ingekua ni mimi ningeshamlamba makwenzi ya ukweli...nwy kina dada ndo mjifunze wakati mwingine kumtokea mwanaume ni balaa tupu...siku yakichacha unaanza kuambiwa ulijipendekeza na kung‘ang‘ania kisicho chako!!

Kunilamba makwenzi bibie ni utashi wako lakini kwa mazingira yaliyopo ni hatari sana.
Mwenzio alpokuja kunikashifu ofisini mbele ya watu wote sikufichi alikuwa anakikaribisha kifo, hili hata mimi niliogopa.
 
Mh. pole sana kwa yote yaliyokukuta, fews things may help:
1. Ulitenda dhambi by going out of your marriage.
2. Ulimkaribisha shetani,ulikula na shetani na uliishi na shetani mara nyingi.
3. Umepoteza heshima kwa kanisa lako ambako huyo dada alienda kutoa habari ya kulazimisha ndoa, na hata jamii yako inayokuzunguka.
Ushauri: Okoka,Mwambie mkeo huo uchafu uliofanya,pia huna sababu ya kublock line coz msimamo wako wa kutokuwa naye utakusaidia.

Asante mkuu kwa ushauri wa kiroho,dhambi tunalipa hapahapa,ni ushauri ninaoutilia maanani, ingawaje tunaokoka kwa Neema.
 
Umeingia choo cha kike mzee,usirudie tena.we rudisha full penzi kwa mkeo si umeona hatari ya nyumba ndogo?
 
Anampango wa kutembela nyota yako huyo.
ni vyema usimjibu chochote, atachoka mwenyewe.
 
Umeingia choo cha kike mzee,usirudie tena.we rudisha full penzi kwa mkeo si umeona hatari ya nyumba ndogo?
Ni kweli ndugu, tamaa mbaya.
Lakini kinachonitia hudhuni ni kuwa nimeingizwa mkenge na huyu dada na nimeingia kichwa kichwa.
Kujinusuru imekuwa nongwa
 
Anampango wa kutembela nyota yako huyo.
ni vyema usimjibu chochote, atachoka mwenyewe.
Asante ndugu, nimefanikiwa kutomjibu kwa mwaka sasa, lakini hachoki kupiga simu na msg.I hope atachoka.
 
Asante ndugu, nimefanikiwa kutomjibu kwa mwaka sasa, lakini hachoki kupiga simu na msg.I hope atachoka.
We cheza na mademu wa siku hizi kama hawajakurudisha kwenu sijui rombo au kimanzichana sijui.
badilisha laini ya simu.
 
Eti zinakuchefua rohoni....na wewe unanichefua kwa tabia yako chafu!!!Mijanaume mingine bwana...wakati mnavunja amri ulikua unanoa raha wala hukushea na mtu leo chefuko la kinafki ndo unajifanya unataka ushauri?!mwone kwanza!‘Alafu eti ukajifanya we ndo mke wako....HOVYOOO!

lizzy mtu mpaka amejianika hivi.. anashida na anahitaji ushauri.... na sio kejeli ....

Mkuu ushauri wangu acha pombe.. maana mambo yote hayo pombe ndio chanzo
 
lizzy mtu mpaka amejianika hivi.. anashida na anahitaji ushauri.... na sio kejeli ....Mkuu ushauri wangu acha pombe.. maana mambo yote hayo pombe ndio chanzo
Ushauri angeomba bila kumdharau huyo dada maana nae ni wale wale....angekua muungwana angeomba kistaarabu au angejidharau na yeye maana sioni kama yeye ni bora kuliko huyo anayedai amemrubuni...wanaume mzima anarubuniwa?!Mara mbili?!Aseme tu alikubali na kama dada anamtia kichefu chefu yeye nae anajitia kichefu chefu kwa tabia yake.Sio anajifanya VICTIM wakati alikua na akili zake zoe wakati wanashiriki mambo yao huko!!!
 
Ushauri angeomba bila kumdharau huyo dada maana nae ni wale wale....angekua muungwana angeomba kistaarabu au angejidharau na yeye maana sioni kama yeye ni bora kuliko huyo anayedai amemrubuni...wanaume mzima anarubuniwa?!Mara mbili?!Aseme tu alikubali na kama dada anamtia kichefu chefu yeye nae anajitia kichefu chefu kwa tabia yake.Sio anajifanya VICTIM wakati alikua na akili zake zoe wakati wanashiriki mambo yao huko!!!
Asante dada yangu , una akili sana na vijembe vyako vimenikolea.
Lakini kurubuniwa na mwanamke(for material gains) ni mchezo uliopao sasa hivi mijini.
Mchezo huu upo tangu zamani za kale enzi za Queen Cleopatra.
Hili halilalaishi makosa niliyofanya, nimeamka na naendelea mbele.
Licha ya vijembe vyako hujajibu swali langu la kutaka ushauri, wa huyo mwenzio anayenisumbua kwa simu na msg-hapo unasemaje mrembo.
 
Asante dada yangu , una akili sana na vijembe vyako vimenikolea.Lakini kurubuniwa na mwanamke(for material gains) ni mchezo uliopao sasa hivi mijini.Mchezo huu upo tangu zamani za kale enzi za Queen Cleopatra.Hili halilalaishi makosa niliyofanya, nimeamka na naendelea mbele.Licha ya vijembe vyako hujajibu swali langu la kutaka ushauri, wa huyo mwenzio anayenisumbua kwa simu na msg-hapo unasemaje mrembo.
Badili hiyo kauli ya kwamba nakupiga sijui nakutupia vijembe (mi sio mpenzi wa taarabu) then ntafikiria kukushauri!!Na huyo dada sio mwenzangu.....
 
Badili hiyo kauli ya kwamba nakupiga sijui nakutupia vijembe (mi sio mpenzi wa taarabu) then ntafikiria kukushauri!!Na huyo dada sio mwenzangu.....
Kajukuu kangu kanoko haka....khaaa!
 
lizzy mtu mpaka amejianika hivi.. anashida na anahitaji ushauri.... na sio kejeli ....

Mkuu ushauri wangu acha pombe.. maana mambo yote hayo pombe ndio chanzo
Hii pombe mnaisingizia vingi sana...... pombe ndo ilimvulisha chupi? Ndo ilimpa namba za simu? Ndo inatukana?...Wakati ameanza kuzoeana naye na kumkaribisha pombe akijua ana mke home, ni pombe ilimtuma?
 
Hii pombe mnaisingizia vingi sana...... pombe ndo ilimvulisha chupi? Ndo ilimpa namba za simu? Ndo inatukana?...Wakati ameanza kuzoeana naye na kumkaribisha pombe akijua ana mke home, ni pombe ilimtuma?

Walitoka out huku na huku Majoja akajikuta anakagua baada ya kupiga chicha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom