Jamani nisaidieni-huyu dada ananipa presha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani nisaidieni-huyu dada ananipa presha.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Majoja, Jun 10, 2011.

 1. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Uzuri wa mtandao wa JF bwana ni ushauri mtu unaoweza kuupata.
  Ushauri tu unaweza okoa maisha ya mtu.
  Mimi ni mgeni sana JF lakini si mgeni wa maisha.
  Nimepitia ukurasa huu ma mimi ninatizo linalo nisibu, tena tatizo linalonipa presha.

  Mimi ni mjasiriamali mzuri tu kanda hii ya pwani.
  Kuna dada ambaye kumbe ananifuatilia kwa karibu sana na kwa muda mrefu.Mwishowe akabisha hodi ofisini kwangu kama dada wa kutoka sehemu zetu huko milimani na akasema anasalimia tu.
  Muda si mrefu simu zikaanza kuwa nyingi na hatimaye akaomba out.
  Nisionekane mshamba masikini miye nikamtoa out. Kweli pombe mjumbe wa Ibilisi, muda si muda tukawa tunavunja amri ya sita na huyu dada akwa antaka sana kunimiliki.
  Mimi nimeoa na yeye hajaolewa.
  Mambo yakaendelea kwa muda kuidogo lakini nikakataa kabisa kujicommit na mabo yote ikawa kwa soksi ili isijetokea ajali ya mimba.
  Nafikiri malengo ya dada yakawa hayajakamilika, na akazidi kuwa mkali kwangu kadri siku zilivyoendelea, ikiwa ni pamoja na vitisho kuwa ataniexpose kwa jamii kama nitamwacha.
  Nikanwekea mtego siku moja , alipiga simu sikuipokea , lakini nikajidai mimi mke wa jamaa unyempigia.Nikamuuliza unashida gani na mume wangu maana nimesikia sauti ya kike.
  Hapo yalianza matusi ya kuua mtu, matusi balaa-ati wewe ulicho nacho ndo mumeo anachofuata kwangu!
  Hakika nilipigwa butwaa!
  Siku ya pili nikamuuliza mbona ulibishana na mke wangu? naye akajibu, ati anajidai mjanja atanikoma mie!
  Hapo ndo nikajua hapa kuna walakin na nika mwacha kwa muda mrefu.
  Wanaume tuna matatizo sana, baada ya muda akanibembeleza na kulia sana, baadaye nikampeleka kinywaji tukanywa.
  Punde si pundeikawa mechi tena isiyo na soksi safari hii.Bibie alifurahi sana siku hiyo, na akapotea zaidi ya mwezi.
  Aliporudi akaja na stori kuwa yeye tayari.Nikamuuliz tayari nini, akaniambia mimba.
  Nikachanganyikiwa kabisa lakini baada ya muda mrefu wa kufikiri nikamwambia nitamtafutia kiwanja ajenge ili mtoto asije pata taabu.
  Lakini Mungu si Asumani, baada ya miezi minne kumbe mimba haikukaa na nikamuuliza vipi akaanza ukali tena ili mimba ikuzwe.Hapo nikakataa kabisa maana nikaona nimeponea tundu la sindano.
  Kuona hivyo huyu bibi akawa kichaa na akaja ofsini nakutukana matusi ya mguoni , na nikaaibika sana.
  Bibie akaahidi kunishitaki kanisani na kweli akaenda kumwona Mchungaji ,hata hivyo akapuuzwa kwa vile walimwona punguani.
  Mambo yalipozidi kuwa mabaya akaanza kunisimamisha barabarani kwa nguvu, watu wantazama sinema na kushangaa!
  Hapo ndo nikaenda fungua RB na kuwajulisha ndugu zake juu ya huyo mtoto wao.
  Nilivyokuwa serious , aliwekwa ndani siku moja kwa kunibugidhi lakini ndugu zake wengine wakamwokoa na janga zaidi.

  Wana JF hadithi ni ndefu lakini mwisho ndugu zake wakamkana kwa tabia yake na kusihi kutonisumbua na hii ni baada ya kuwalipa wazazi wake kifuta aibu cha kulala na binti wao(ana miaka 32).
  Sijawasiliana naye(kwa maana ya kumpigia au kuongea naye) kwa zaidi ya mwaka sasa.

  Lakini ka muda huo woote hadi leo ananipigia simu karibu mara kumi wiki na meseji kama kumi hadi ishirini kwa wiki ambazo sizijibu kamwe.
  Kwenye simu yangu kama ushahidi nina meseji zilizofikia 831
  Meseji ya mwisho imeingia kwangu kama nusu saa iliyopita.
  Kwa hakika zinanichefua rohoni kupita kiasi.
  Nsaidieni ndugu zangu huyu bibie anamapepo? na mnaweza nishauri nini?
   
 2. Kichwa cha panz

  Kichwa cha panz Senior Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Block number yake kwenye simu unaweza kublock number fulani fulani, ukishindwa waulize service provider watakusaidia. Hana mana alikuwa anatafuta pa kupumulia sasa kakutana na mti mkavu. Ukishindwa kabisa badili number au ukiona itakucost usijibu msg zake hata moja na uendelee kuzifuta zisikutie maruweruwe, akipiga endelea na msimamo wako wa kutopokea mana mwisho wa siku atachoka tu mwenyewe.

  Kingine ni kuwa uliruhusu shetani akutawale kwa kuruhusu mahusiano yawepo kati yako na yeye ilihali una mkeo, tubu fasta kwa hilo na usirudie tena, unajua kuna akina dada wanapenda mtelemko yaani akukute una kila kitu then ale bata tuuuu...

  Huyo dada kingine sio mkaaji (mke wa kuoa) kwa jinsi alivojiexpose tabia zake ni za kiswahili na kichangu na anaonekana alikuwa na stress hivo anatafuta wa kumpunguzia. Shukuru Mungu kakuepushia balaa hilo vinginevo ungekuwa unajutia ndoa yako kuvurugwa na yeye.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Eti zinakuchefua rohoni....na wewe unanichefua kwa tabia yako chafu!!!Mijanaume mingine bwana...wakati mnavunja amri ulikua unanoa raha wala hukushea na mtu leo chefuko la kinafki ndo unajifanya unataka ushauri?!mwone kwanza!‘Alafu eti ukajifanya we ndo mke wako....HOVYOOO!
   
 4. m

  mkuki moyoni Senior Member

  #4
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usipokee wala kujaribu kupokea simu yake kamwe ataweza kukufanyia ukarumanzila wewe
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Lzy nawe unatabia hizo za kungangania mwanaume?dawa wewe muombe ule mtandao wa wanafunzi tigo,najua atakataa na ndipo atakapokuacha.mwambie siku hizi umezoea huko hivyo mbele huna mpango napo.lazima akukimbie
   
 6. Nemo

  Nemo JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 80
  Wana Jf:
  Jamani, is it only to me or does this story sound like the other side ya ile thread ya "Natamani kujiua....................." to anyone else?????

  Majoja
  Two things:
  1. You better Come clean to your wife and apologise, before hajahabarishwa na bibie. Most of the time People tend to find more sincerity in an apologies offered before one's hand gets caught in the cookie jar
  2. Next time try to keep it in your pants. If you know you are weak (which you obviously are), kaa mbali na wanawake! Do not befriend any nor try to take 'em out

  Side note:
  If you dont mind Can you advise if wewe ndiye mume discussed in the named thread above?
   
 7. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kaka lazima ukubali kwamba ulikosea sana toka mwanzo!
  kweli mwanzoni ulilamimika kuingia mkenge na ukajikuta umemvua chupi,
  sasa alipoanza fujo zake ilibidi umwache haraka sana,
  kosa lako kaka ulinogewa na ukajikuta umerudi tena,
  lazima ukubali kosa lako kaka!!!!

  unastahili lawama kwa kuzidi kumkaribisha katika himaya yako,
  huyo dada alikuwa na lengo mahususi ambalo ni kuiteketeza familia yako,

  jaribu kumpotezea sasa, badilisha line ya namba ya simu unayotumia!
  acha kumuendekeza, kwani waweza jikuta unatumbukia tena!
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ninng‘ang‘anie mwanaume nimezaliwa nae mie!???
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Labda ni mtu mmoja kapika story zote mbili...
   
 10. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  mmh!haya mama
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Niwe muwazi tu ndugu yangu, hivi lazima kila uhusiano au urafiki wa mvulana na msichana uelekee kwenye ngono? Hamuwezi kuwa marafiki bila ngono? Ngono ni mapenzi au zinaa tu? Unaweza kusema unampenda mtu kweli wakati unaogopa asikuue au asikuharibie maisha? Vyovyote vile mkuu hata kama umesevu huo msala bado sijafurahishwa na zinaa uloifanya. Nimeufunua moyo wangu!
   
 12. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Umefanya la maana kujitambua..
   
 13. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kumbe ulishaona
   
 14. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #14
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Mh. pole sana kwa yote yaliyokukuta, fews things may help:
  1. Ulitenda dhambi by going out of your marriage.
  2. Ulimkaribisha shetani,ulikula na shetani na uliishi na shetani mara nyingi.
  3. Umepoteza heshima kwa kanisa lako ambako huyo dada alienda kutoa habari ya kulazimisha ndoa, na hata jamii yako inayokuzunguka.
  Ushauri: Okoka,Mwambie mkeo huo uchafu uliofanya,pia huna sababu ya kublock line coz msimamo wako wa kutokuwa naye utakusaidia.
   
 15. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...pole sana kaka. Ushauri wangu "acha kumuahidi ahadi zisizotekelezeka"
  Kwa faida yako, majibu yote utayapata kwenye thread hii
  ; https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/144222-natamani-kujiua.html ...soma post ya mwanzo mpaka mwisho, kuna mahala utakuta majibu matatu muhimu kwako.
   
 16. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nawashukuruni nyote mliotoa ushauri kwangu.
  Najia nimeruhusu tamaa kunitawala nahivyo huyu dada kupata upenyo.
  Natanguliza kuwa mimi ni mkristo na si mwislamu kama katika thread iliyopo kama hii ya dada mwingine.
  Pamoja na yote najutia kurubuniwa na huyu dada ili kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi, lakini ni muda sasa sina mahusiano kabisa(mwaka mmoja na zaidi)
  Kwa wale ambao hamuamini kuwa kuna wanadamu mapepo basi huyu dada ni mmoja wapo maana kwa uhakika nimejisikia kuwa na nia ya kumdhuru kwa mikono yangu mpaka nikawa na hisia na hasira za za ajabu kwa kuingiwa na mkenge na dada huyu.
  Naamini kuwa wote mlionishauri Mungu yupo pamoja na mioyo yenu na nitaendelea na msimamo wa kutojibu simu/msg zake.
  Wengine mnafikiri hii ni hadithi ya kutunga la, ni kweli kabisa na uhusiano huu umeitesa sana roho yangu.
   
 17. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Uko makini kijana
   
 18. k

  kisukari JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,759
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  ni bora umekubali makosa.wote ni binaadamu hakuna asiekosea.ila makosa yanatofautiana.nina amini kwa somo ulilolipata,ndoa yako utazidi kuidumisha,wanawake wengine wana frustration zao za kimaisha,wee endelea kumu ignore usipokee simu yake au kama utaweza,badilisha namba
   
 19. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  mwezi wa sita huu kaka...msimu wa mavuno.nakutakia mavuno mema.
   
 20. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,853
  Likes Received: 629
  Trophy Points: 280
  Lizzy,mwenzio kaomba ushauri bana. Mpe ushauri mbona ghafla umekuwa mkali like this na una mahasira povu linakutoka mdomoni like the woman in question? Or are U the one?
   
Loading...