Jamani nimetapeliwa

Watu wengine wanaonewa wanaitwa popoma,lakini wewe ukiitwa popoma,ushangilie na umnunulie hata kasoda aliyekuita popoma, maana umestahili
 
Kinachotuharibu sisi waafrika ni kupata dili halafu hushirikishi watu wako wa karibu wakupe ushauri. Unataka ufaidi peke yako.

Wakati nasoma primary miaka hiyo, kuna rafiki yetu aliletewa chakula na mama yake wa kambo. Yule dogo alituita tule wote, katika kukifungua chakula, tukagundua kuna chenga chenga nyeusi mle ndani. Wale wanafunzi wakubwa wakasema hiyo itakuwa sumu.

Tukapeleka huo msosi kwa mwalimu na kweli akasema hiyo ni sumu ya panya. Mwalimu akaruhusu shule imsake huyo mama kabla hajapanda basi kwani alivyoleta chakula akawa amesepa. Kumbuka, kutoka shule mpaka kwenye kituo cha basi ni kama KM 3. Wanafunzi tulikimbia na hatimaye kumpata huyo mama.

Kumbe yule mama alikuwa amegombana na mume wake na alitaka kumkomesha kwa kumuua mtoto.

Somo: ukipata dili usiwe mchoyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama kuna nyaraka kama unaona unapewa PESA ndefu bila kutolea JASHO STUKA mapema, Wazungu wanasema "The deal is too GOOD to be...". Watu waligushi paylist ya benki wakitaka kumtapeli muuza bia za jumla itakuwa BL, wanatengeneza kirahisi kabisa, Wamelizwa wengi sana
 
Aksante nimejifunza kitu
 
Sikupewa pesa ndefu km unavyofikiri bali hiyo pesa ilikuja ili aweze kufanya investment yake na pia nilimwamini kujuwa ni mtu gentlemen kumbe ni tapeli la kimataifa
 
Sikupewa pesa ndefu km unavyofikiri bali hiyo pesa ilikuja ili aweze kufanya investment yake na pia nilimwamini kujuwa ni mtu gentlemen kumbe ni tapeli la kimataifa
Wala mimi sikulaumu bali ninatoa tahadhali kwa kila mtu humu, ukiona mtu anakuletea deal rahisi STUKA hasa kama humfahamu. Haiwezekani from no where mtu akuletee deal nzuri jiulize kwa nini hajawapa marafiki zake. Anyway sometimes unaweza win lakini kuwa makini
 
Siku za karibuni wadada wengi wa kibongo wamepigwa na matapeli wanaoshirikiana na wazungu au wanaigiza wazungu.
Wanaanzisha urafiki kwenye mitandao kisha whatsapp unamuona kabisa.

Mdada anaongopewa kapendwa na mzungu anataka amuoe.
Anamwambia kamtumia zawadi kama mleta mada, kisha anaambiwa mzigo upo Zanzibar au mbali na mji wa mtapeliwa, anaambiwa alipie pesa za kuondoa mzigo na kodi kisha aende akachukue mzigo.

Wadada kwa tamaa wanawaonesha wenzao wamepata mchumba mzungu na picha za zawadi.
Pesa ya kulipia mzigo wanakopa madeni makubwa na kuuza vitu. Mwisho aibu kubwa huko ugenini Zanzibar wanapojikuta wamepigwa, hawana nauli ya kurudia wala mahali pa kuishi.

Jamaa yangu kawasaidia wadada watatu siku kama 7 zilizopita.
 
Titicomb,
Yote hayo ni matokeo ya kupenda slope na tamaa. Saiv teknologia imekua na watu wamekua wajanja sana so usipokua makini inakula kwako.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…