Jamani nimetapeliwa

vika

Member
Apr 11, 2011
31
30
Kuna mzungu tapeli anayejita Gambler Erik number zake za simu +41779140475 tulikuwa marafiki kwenye mtandao wa LinkedIn kama marafiki wa kawaida akaonyesha kuja kuwekeza Tanzania.... Akasema kabla ya kuja Tanzania atanitumia machine zake za kutengeneza lotion na cream kwangu sikumbili kabla ya yeye mwenyewe kuja Tanzania. Na kwenye hiyo mizigo kaweka dola za kulipia pango la nyumba na maswala mengine

Akanijulisha wiki iliyopita atatuma mizigo kwenye ndege za UN na mara moja mzigo utanifikia kwangu kwa kupitia wakala.

Nilichoshangaa jumatatu ya wiki hii Kuna mwanamama kanipigia kwa number 0758392082 jina inasoma Emmanuel Tesha... At Mimi nilipe Kodi ya hizo bidhaa zilizokuja Tanzania kwa jina langu. Nikamwuuliza huyo Tapeli Gambler hivi Ni sahihi akaniambia wewe lipa nitakurudishia. Kumbe ndio nimeanza kuliwa kekundu hapo.

Hiyo ilikuwa Ni Kasulu Kigoma nikashangaa kwa Nini mzigo utuwe Kasulu na siyo DSM? Baada ya kulipa $ hiyo number haipatikani hewani. Nikajiuliza Toka jumatatu mpaka Alhamisi hakuna dalili yoyote ya kupokea mzigo ilikhali huyo mama Tapeli ananiaminia kwamba huo mzigo upo na utanifikia kwangu bila tatizo. Jana kaibuka Tapeli mwingine mwenye number 0758727527 jina la usajili Swaum Mena.

Akaniambia kiswahili kwamba mzigo umekwama Arusha ati nilipe $500 ili mzigo unifikie... Leo saa sita mchana.... Hapo ndio nikashtuka na kujuwa Kuna utapeli na hiyo pesa sijaituma. Na nikamtumia msg huyo mama kwamba Ni Tapeli anirudishie pesa zangu

Nimetuma ujumbe huu na hizo number za simu ili wengine yasiwapate kama Mimi yalivyonisibu
Nawatakia Ijumaa khereem

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu matapeli wapo kila kona huko LinkedIn ndo wamejaa wanatafuta watu wa kuwapiga.

Wanaomba connection, ukikubali wanaomba personal email wanaanza kukushawishi.

Nimeshakutana nao kama wawili LinkedIn wanawake ila stori ni zile zile tu za marehemu kaacha hela ndefu benki....mmoja kati ya hao 2 aliniambia Kuna jamaa kafariki kaacha $1.5m tufanye mpango tui claim mm niwe kama beneficiary nilimuuliza swali 1 akapotea hadi leo... Unafanya kazi hujui sheria za kutakatisha hela ?Akakimbia

ANYWAY KITU MUHIMU KWASASA JIFUNZE ULIPOKOSEA LIMESHATOKEA HILO SONGA MBELE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu hamtumiagi akili, we na exposure yote hii hadi leo hujui hizo mambo za kujidai sijui anataka wekeza blah blah, ila ndio ushajifunza, hamna uwekezaji wa mitandaoni sawa? Mtu akutumie eti mashine bila hata kukuona, kufanya utafiti, kupata vibali nk... Ushajifunza ila na hiyo hela jiesabie tu maumivu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia ya sasa unatapeliwa kijinga hivyo?

Ure still have time to learn in this world unaonekana umgeni hata washauri huna..
Mtu anapoingia kwenye anga za kupigwa huwa wengi hawatakagi ushauri. Hata kama ana rafikiake wa karibu,hawezi kumshirikisha. Hesabu anayopiga ni aje tu amshitukize huyo rafikiake ubilionea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole ila next time usipende vya bure ndugu, mtu umekutana nae mtandaoni hakujui humjui ghafla akataka akutumie mashine na hela ukamuamini kabisa?? Hta hukujiuliza why me?
Au ulivyoskia mzungu ukadata ukajua hela imelala hapo
Kuna mambo mbona hata haihitaji kwenda chuo kuyagundua
 
Ishu zozote zinazohusu UN epukana nazo
Ishu zozote zinazohusu biashara na mtu ambaye hamfahamiani epukana nazo
Ishu zozote za kutumiwa mzigo bila nyaraka kisha unaombwa kwenda kuutoa epukana nazo
Ishu zozote zinazohusu biashara za mtandaoni na mtu usiyemfahamu vema epukana nazo
Wengi wamelizwa na wengi bado wanalizwa na wengine wataendelea kulizwa
Duniani hakuna uaminifu kama huo

Jr
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom