Jamani nifanye vipi nisimchukie?

Jamani nifanye vipi nisimchukie?

Ongeza muda wa kusoma katika lesson preparation zako pia mengine jitahidi kumwachia Mungu na kumshukuru kwa kila jambo, huwezi kujua Mungu amekuepushia nini kwa huyo mwanamke.
Ahsante nashkuru sana ila pia rafiki zake huwa wananipigia simu nahisi nao wananiongezea chuki tu
 
Habari za majukumu familia yangu na jf?
Natumaini ni wazima wa afya njema huku mkiendelea na majukumu yenu ya kila siku...
Back to the point
Mwenzenu nlikuwa na mpenzi wangu ambae nilimpenda sana nasema tena nilimpenda sana na nilijua yeye ndo atakuja kuwa mke wangu maana nilimtambulisha mpaka kwa baadhi ya ndugu zangu na yeye pia alinitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake... Mimi nlikuwa nimemtangulia kielimu maana wakati yeye anaenda kuanza chuo(diploma) mimi nlikuwa mwaka wa tatu(degree ) hivyo basi tofauti hizi za kielimu zilitufanya tusiwe karibu kwa muda mwingi maana wakati mimi nipo chuo yeye alikuwa nyumbani..
Tatizo lilianza taratibu baada ya binti kuanza vitabia vya dharau na kuwa busy sana na simu hususani wakati wa usiku.. Sikuweza kugundua haraka kinachoendelea ila nilianza tu kuhisi kuna kitu flani sasa hivi kipo kwa huyu binti...
Tuliendelea kuwasiliana tu kwa simu japo mawasiliano hayakuwa mazuri sana kama hapo awali..
Baada ya binti kuwa amechaguliwa kujiunga na chuo ilili bidi nisafiri niende kumtembelea hapo chuoni kwao maana ilikuwa ni muda mrefu sana tangu nimuache home akisubiri post za kujiunga na chuo...(vyuo vyetu vilikuwa vipi mikoa tofauti)
Nilikaa nae kama siku tatu then nikarudi zangu chuo..
Huwezi amini hata wiki moja haijaisha tangu nirudi chuo akanitumia message kuwa kapata mimba hizo siku tatu nilizo kaa nae..
Kwa kweli nilishangaa mimba gani ya kugundulika ndani ya wiki moja tu!!!
Nikamwambia asihofu azae tu mtoto atakaa nyumbani then yeye aendelee tu na masomo.. akakubali ila akasema akae kwanza huko chuoni wakati anafanya utaratibu wa kuwaambia kwao... Nikasema fresh
Huwezi amini yule binti kakaa kama wiki moja mbele akasema aliugua kichwa so akaenda kununua dawa alivo kunywa tu mimba ikatoka na alilia sana siku hiyo akanipa jukumu la kuanza kum bembeleza kupitia simu..
Siku moja nipo class binti akanipigia simu nikamwambia nipo class akantumia message "tuko nje tuongee jambo serious" kutoka binti ananiambia kuna jamaa anamsumbua na yeye hamtaki eti rafiki zake na yule jamaa wanasema watamdhuru kama hata mkubali rafiki yao akasema ana hofu sana na wale watu so akanipa namba za huyo jamaa alie mkataa...
Basi mi kwa hasira za demu wangu kutishiwa maisha nilimpiga mkwara jamaa nikamwambia ntamuua yeye kabla hajamdhuru demu wangu...kiukweli yule jamaa hakunitukana kitu alinambia yule ni demu wake pia ila walikuwa na mgogoro kwanini demu atoe mimba yake.. Na jamaa akanambia kuwa demu alisafiri kwenda kwake na waka kaa wiki mbili pamoja (huyu jamaa anakaa mkoa wa nyumbani kwetu) daaah aisee nilichanganyikiwa ikabidi nimpigie simu rafiki ake mmoja pale chuo nimuulize kama Jessica aliondoka chuoni...
Rafiki ake akanambia ni kweli aliondoka kwa wiki mbili..
Roho iliniuma sana kwa mtu niliempenda kujazwa mimba na jamaa mwingine... Na mbaya zaidi kunisingizia kuwa ni yangu..
Ilibidi jamaa nimuonbe msamaa kwa lugha chafu niliyotumia kwake.. Then nika komaa na binti kumhoji vizuri na baadae akakubali kuwa mimba haikuwa yangu roho iliniuma sana ndo nikaamini watu wengi sana wanaishi na watoto wasio wao kwa kusingiziwa tu
Nika kausha kama wiki mbili baadae nikaanza kuona profile picha yake ya whatsupp anamuweka yule jamaa na mpaka sasa nahisi wako pamoja

Tatizo langu ni kwamba nimejaribu sana kumsamee huyu kiumbe ili aende zake kwa amani lakini nashindwa
Najikuta natumia muda mwingi kumuwazia vibaya tu.. Hata mimi sitaki kuhifadhi chuki juu yake lakini najikuta tu namchukia automatic.. Msanii fd Q anasema "chuki umchoma zaidi anae hiifadhi"
Jamani sitaki kuhifadhi chuki naombeni ushauri jinsi ya kumsamee huyu binti ili hata nikimuona niwe na amani tu..
Maana nimeshaanza kuona wanawake ni viumbe hatari sana katika maisha yangu
Mpaka huwa nawaza hata huyo mwingine ntakae kuja kumpata siku akinambia ana mimba yangu sijui ntamwambiaje.. Tukapime DNA au?? Maana kusingiziwa mimba nje nje tu
Ushauri wenu jinsi ya kuondoa hii roho ya kinyongo inanitesa sana
HAHAHAHA DA NGOJA NIFANYE KAZI KWANZA
 
Ahsante nashkuru sana ila pia rafiki zake huwa wananipigia simu nahisi nao wananiongezea chuki tu
Tena hao watakufanya uzidi kuzunguka kwenye duara hilo, unahitaji kuvunja huo mnyororo, wakipiga kuwa makini kuwauliza wanataka nini? Ukiwa makini sana mtu anajitafakari kabla hajapiga simu.
 
Pole unapaswa kutendwa kama mara tatu then utakuwa perfect, chukulia hio kuwa ni test number 1, subir test nyingine 2. Then oa utakuwa vizuri tu.
Huwa najiuliza kuhusu hawa watu wanao ishi pamoja mpaka wana zeeka sijui huwa wana tumia mbinu gani kuishi na wanawake... Wazo la kuoa lime yeyuka kwa speed sana
 
Ninakumbuka once upo the time, nilimpenda kaka mmoja, sikudhani kama nitaweza kuishi bila yeye. Alipoamua kusitisha mahusiano nilisikia kabisa maumivu fizikia ya moyo sio hisia tu. Sasa hivi tunaongea kama watu tunaofahamiana na huwa ninacheka hivi huyu alinifanya niumie huyu.
 
Huwa najiuliza kuhusu hawa watu wanao ishi pamoja mpaka wana zeeka sijui huwa wana tumia mbinu gani kuishi na wanawake... Wazo la kuoa lime yeyuka kwa speed sana
Ukikutana na mtu sahihi mapenzi si kifungo, matatizo ni pale unapokutana na mtu ambae hamwendani ni mtihani wa maisha.
 
Mimi niliwahi kuamua kua kila nikijihisi nina hasira naenda kupiga gita na ni lazima nikapige.
Gita lilipo na ninapoishi ni mbali, halafu sijui vizuri hivyo hua naona "Dah natembea mpaka huku kisa gita ambalo siliwezi vizuri?" Njiani hua napima ishu zilizosababisha kilichotokea na hua naona nakua sawa.
Ugumu wa kulifuata na kulitumia gita umenifanya niwe mwangalifu katika maamuzi ili nisije kujikuta nimekasirika ghafla na kutakiwa kulifuata gita.
 
Tena hao watakufanya uzidi kuzunguka kwenye duara hilo, unahitaji kuvunja huo mnyororo, wakipiga kuwa makini kuwauliza wanataka nini? Ukiwa makini sana mtu anajitafakari kabla hajapiga simu.
Ni kweli kuna vimaneno huwa wanavileta mara ooh mtu wako likizo kaenda kwa mshikaji.. Natakiwa kweli kuwa mbali nao
 
Mimi niliwahi kuamua kua kila nikijihisi nina hasira naenda kupiga gita na ni lazima nikapige.
Gita lilipo na ninapoishi ni mbali, halafu sijui vizuri hivyo hua naona "Dah natembea mpaka huku kisa gita ambalo siliwezi vizuri?" Njiani hua napima ishu zilizosababisha kilichotokea na hua naona nakua sawa.
Ugumu wa kulifuata na kulitumia gita umenifanya niwe mwangalifu katika maamuzi ili nisije kujikuta nimekasirika ghafla na kutakiwa kulifuata gita.
I like this mkuu.
 
("Huwa tunasema "Chuoni njoo na akili zako tuu Tabia zote utazikuta chuoni")anonymous... "Tatizo mi bado nilipokosea kakosa sitambui? Mpaka kafunga virago na kaamua kuondoka sitambui...ila kinachoniuma maneno neno maneno "
_______________________________
Song-Ukimuona
 
Mwanaume kuumizwa na mwanamke ni uzembe. Haya maua yamejaa tele... hili likinyauka unachuma lile.

Ndo ujinga huu wa watu kujifanya wasafi. Mwanaume unapaswa uwe na mademu watatu angalau... Huyu akileta fyoko unakuwa tayari una back up.
Unaongea kirahisi rahisi kama wewe unao hao watatu.
 
Mimi niliwahi kuamua kua kila nikijihisi nina hasira naenda kupiga gita na ni lazima nikapige.
Gita lilipo na ninapoishi ni mbali, halafu sijui vizuri hivyo hua naona "Dah natembea mpaka huku kisa gita ambalo siliwezi vizuri?" Njiani hua napima ishu zilizosababisha kilichotokea na hua naona nakua sawa.
Ugumu wa kulifuata na kulitumia gita umenifanya niwe mwangalifu katika maamuzi ili nisije kujikuta nimekasirika ghafla na kutakiwa kulifuata gita.
Haaa haaaa mkuu hiyo style yako nimeipenda sana... Vip bado tu hujajua kupiga gita??
 
Ukikutana na mtu sahihi mapenzi si kifungo, matatizo ni pale unapokutana na mtu ambae hamwendani ni mtihani wa maisha.
Sasa huyo sahihi sijui ntamjuaje maana hata huyu mwanzo alinipenda sana.. Nlikuwa nashangaa kwanini watu wengine hawataki kuoa.. Sasa nahisi na mimi naelekea huko huko
 
Haaa haaaa mkuu hiyo style yako nimeipenda sana... Vip bado tu hujajua kupiga gita??
Hadi leo sijui na sidhani kama nitajua kwakua kulifuata ni mpaka nikasirike na nimekua sikasiriki so nipo nipo tu hata chords nishazisahau.
 
Hadi leo sijui na sidhani kama nitajua kwakua kulifuata ni mpaka nikasirike na nimekua sikasiriki so nipo nipo tu hata chords nishazisahau.
Chanzo cha hasira zako ni nini??
 
Haya matatizo bwana ni rahisi mtu kukwambia piga chini lakini ni wewe na moyo wako ndiyo unajua unaumia vipi. Time is the best healer.
asee kweli kabisa muda pekee ndio mponyaji. Haya mambo yanaumiza saana asikuambie mtu, ni rahisi kushauri usiombe yakukute. Mimi yalinikumba january 2014 nilikuchua mwaka kupona, ila mpaka leo moyo haujafunguka kupenda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom