dracular
JF-Expert Member
- Dec 24, 2013
- 769
- 1,061
Habari za majukumu familia yangu na JF?
Natumaini ni wazima wa afya njema huku mkiendelea na majukumu yenu ya kila siku.
Back to the point
Mwenzenu nlikuwa na mpenzi wangu ambae nilimpenda sana nasema tena nilimpenda sana na nilijua yeye ndo atakuja kuwa mke wangu maana nilimtambulisha mpaka kwa baadhi ya ndugu zangu na yeye pia alinitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake.
Mimi nlikuwa nimemtangulia kielimu maana wakati yeye anaenda kuanza chuo (diploma) mimi nlikuwa mwaka wa tatu (degree ) hivyo basi tofauti hizi za kielimu zilitufanya tusiwe karibu kwa muda mwingi maana wakati mimi nipo chuo yeye alikuwa nyumbani.
Tatizo lilianza taratibu baada ya binti kuanza vitabia vya dharau na kuwa busy sana na simu hususani wakati wa usiku. Sikuweza kugundua haraka kinachoendelea ila nilianza tu kuhisi kuna kitu flani sasa hivi kipo kwa huyu binti. Tuliendelea kuwasiliana tu kwa simu japo mawasiliano hayakuwa mazuri sana kama hapo awali.
Baada ya binti kuwa amechaguliwa kujiunga na chuo ilili bidi nisafiri niende kumtembelea hapo chuoni kwao maana ilikuwa ni muda mrefu sana tangu nimuache home akisubiri post za kujiunga na chuo (vyuo vyetu vilikuwa vipi mikoa tofauti)
Nilikaa nae kama siku tatu then nikarudi zangu chuo. Huwezi amini hata wiki moja haijaisha tangu nirudi chuo akanitumia message kuwa kapata mimba hizo siku tatu nilizo kaa nae. Kwa kweli nilishangaa mimba gani ya kugundulika ndani ya wiki moja tu! Nikamwambia asihofu azae tu mtoto atakaa nyumbani then yeye aendelee tu na masomo akakubali ila akasema akae kwanza huko chuoni wakati anafanya utaratibu wa kuwaambia kwao nikasema fresh.
Huwezi amini yule binti kakaa kama wiki moja mbele akasema aliugua kichwa so akaenda kununua dawa alivokunywa tu mimba ikatoka na alilia sana siku hiyo akanipa jukumu la kuanza kumbembeleza kupitia simu. Siku moja nipo class binti akanipigia simu nikamwambia nipo class akanitumia message "tuko nje tuongee jambo serious" kutoka binti ananiambia kuna jamaa anamsumbua na yeye hamtaki eti rafiki zake na yule jamaa wanasema watamdhuru kama hata mkubali rafiki yao akasema ana hofu sana na wale watu so akanipa namba za huyo jamaa alie mkataa.
Basi mi kwa hasira za demu wangu kutishiwa maisha nilimpiga mkwara jamaa nikamwambia ntamuua yeye kabla hajamdhuru demu wangu kiukweli yule jamaa hakunitukana kitu alinambia yule ni demu wake pia ila walikuwa na mgogoro kwanini demu atoe mimba yake.
Na jamaa akanambia kuwa demu alisafiri kwenda kwake na waka kaa wiki mbili pamoja (huyu jamaa anakaa mkoa wa nyumbani kwetu) daaah aisee nilichanganyikiwa ikabidi nimpigie simu rafiki ake mmoja pale chuo nimuulize kama Jessica aliondoka chuoni.
Rafiki yake akanambia ni kweli aliondoka kwa wiki mbili. Roho iliniuma sana kwa mtu niliempenda kujazwa mimba na jamaa mwingine na mbaya zaidi kunisingizia kuwa ni yangu. Ilibidi jamaa nimuonbe msamaa kwa lugha chafu niliyotumia kwake.
Then nikakomaa na binti kumhoji vizuri na baadae akakubali kuwa mimba haikuwa yangu roho iliniuma sana ndo nikaamini watu wengi sana wanaishi na watoto wasio wao kwa kusingiziwa tu. Nikakausha kama wiki mbili baadae nikaanza kuona profile picha yake ya whatsupp anamuweka yule jamaa na mpaka sasa nahisi wako pamoja.
Tatizo langu ni kwamba nimejaribu sana kumsamee huyu kiumbe ili aende zake kwa amani lakini nashindwa. Najikuta natumia muda mwingi kumuwazia vibaya tu. Hata mimi sitaki kuhifadhi chuki juu yake lakini najikuta tu namchukia automatic. Msanii Fd Q anasema "chuki umchoma zaidi anae iifadhi"
Jamani sitaki kuhifadhi chuki naombeni ushauri jinsi ya kumsamee huyu binti ili hata nikimuona niwe na amani tu.
Maana nimeshaanza kuona wanawake ni viumbe hatari sana katika maisha yangu. Mpaka huwa nawaza hata huyo mwingine ntakae kuja kumpata siku akinambia ana mimba yangu sijui nitamwambiaje.. Tukapime DNA au? Maana kusingiziwa mimba nje nje tu.
Ushauri wenu jinsi ya kuondoa hii roho ya kinyongo inanitesa sana