Jamani niende au nisiende? msaada....

Jamani niende au nisiende? msaada....

unaambiwa hiv siku zote mwanzo huwa ni mgumu ndugu yangu yawezekana huko mbeleni utakuja kuongezeka kulingana na ufanyaji wako wa kazi so, nenda tuu ukaanzie na huo kwan ajira siku hizi ni ngumu sana hata kama umesoma mpaka chuo kikuu.
 
Nenda kaanze kazi kama utataka kubadilisha ubadilishe acha kudeka wewe,laki tano ni ndogo?unayo?
 
:spit:Inaonekana unapenda maisha ya juu ndugu unataka upange chumba cha laki ununue kitanda.tv,kabati na kila kitu?????....kwa mtu mwenye akili asiye na kazi hiyo laki tano unaanza kwa kupanga chumba cha bei rahisi na pia unaweza anza kwa kulalia godoro tu pole pole vingine utapata na maisha yataendelea....we mtoto wa mama kweli unataka uwe na ndugu ndo uende??????Ungeambiwa kazi Ulaya na mshahara laki tatu ungesema huna ndugu????
Go FIGURE!!!!!!:spit:
 
Nimepata kazi mwanza, kama accountant, ndo kwanza wanaanza business, tatizo ni salary, wanatoa 500,000 kama take home. imenivunja nguvu, niko njia panda, kwenda au kutokwenda.... msaada.

Maisha popote ndugu yangu, mi mwenzio na ka degree kangu nimeanza kazi na salary ya 300,000 lakini hadi leo hiyo 500,000 unayoikataa haijafika, nina familia na ninatarajia kununua kiwanja na kuanza ujenzi kwa mshahara huo mwaka huu,na ninatamani nipate kazi itayonilipa mshahara wa 500,000 lakini bado sijapata, pole sana kijana nenda kafanye kazi.
 
Nimepata kazi mwanza, kama accountant, ndo kwanza wanaanza business, tatizo ni salary, wanatoa 500,000 kama take home. imenivunja nguvu, niko njia panda, kwenda au kutokwenda.... msaada.
Mbona hujatuambia deliverable zako ku justify hata hiyo laki tano?! Enyi vijana mnaotoka vyuoni siku hizi tena kwa bora elimu mna ndoto nyie!!
 
inategemea na mazingira nduguuu ya hiyosehemu yenyewe, may b pango la nyumba ni ghali, na huduma nyenginezo so mia 5 elfu ni kidogosana
 
then nikifika mwanza naanza kukaa kwa demu wako au? mi shida yangu ntaanzaje maisha mwanza mpaka ntapokuja kusimama kabisa ....
inaonekana unakejeli watu wewe mchezozo wako kacheze na huko
 
Unataka uolewe wewe watu tunafanya kazi hadi 90 elfu kwa mwezi
 
Nna hasira na haka katoto!!!
Hebu sogea nikutwange makofi kwanza inaonekana kichwa chako ni ......
'shake well before use'
 
Kuna mwingine analalamika hapa eti kapata kazi serikalini but wamempanga wilaya ya masasi..

Anaogopa hadi panyabuku amesikia huko watu wanakula panya anataka kulia halafu ni Mwanaume eti.. Yaani nimecheka hadi nimetaka kuanguka.Kizazi cha dijitali kina vituko mbaya
Huyu huna haja ya kumsikitikia...masasi kwa sasa ni kama ilivyo kibaha town.Kwanza usafiri ni masaa7-8 toka dar..na pia ni mji unaokua kwa kasi sana.habari za panya ni za wenyeji..ni sawa na hbr za wamasai na kula nyama mbichi..je angepangwa BIHALAMULO kama sie wengine angesemajje?
 
then nikifika mwanza naanza kukaa kwa demu wako au? mi shida yangu ntaanzaje maisha mwanza mpaka ntapokuja kusimama kabisa ....

unataka uanze maisha ukiwa na nyumba ,gari,sofa,dstv,laptop,shamba?au ?....aisee baki tu usiende...inaonekana ulipo sasa una kipato zaidi ya hicho...kule utaenda kupoteza tu muda wako.
 
Kapige kazi! Watu tulianza kazi kwa kujitolea bure sembuse laki tano!!! Kama umelizika kugombania vipande vya sabuni na rimoti na wadogo zako endelea kuchana sharubu nyumbani, lakini laki tano Mwanza unaishi tu! kwa kuanzia siyo mbaya wakati unaendelea na michongo mingine
 
yani wewe mwenzio 2011 nlianza na take home ya laki tatu. Cha muhimu tafuta chumba kisizidi 50000 nunua godoro weka chini trust me life itaji adjust tu. Tena yani mimi ni kizazi cha dijitali lakini nina uwezo wa kufikiri huo mshahara ni mkubwa sana. Kama vpi ni pm nikuconsult maana life was very simple to me utadhani likuwa napokea milioni na starehe nlikuwa nafanya
 
Nimepata kazi mwanza, kama accountant, ndo kwanza wanaanza business, tatizo ni salary, wanatoa 500,000 kama take home. imenivunja nguvu, niko njia panda, kwenda au kutokwenda.... msaada.

Acha bangi wewe, mbona unatupandisha hasira? sisi tunatafuta hata ya 200000 na videgree vyetu inashindikana wewe unaomba ushauri wa take home ya 500000. basi bana Mungu akusaidie.
 
uliza watu wenye degree zao DAR hapa wana take home laki 3 mie shahidi wa hili
 
yani wewe mwenzio 2011 nlianza na take home ya laki tatu. Cha muhimu tafuta chumba kisizidi 50000 nunua godoro weka chini trust me life itaji adjust tu. Tena yani mimi ni kizazi cha dijitali lakini nina uwezo wa kufikiri huo mshahara ni mkubwa sana. Kama vpi ni pm nikuconsult maana life was very simple to me utadhani likuwa napokea milioni na starehe nlikuwa nafanya

Kaka mwaga maujuzi hapa wote tufaidike,, maana wengine mishahara tunayopata mara kazaa ya hiyo na tukisema hapa tutaonekana tunakufuru lakini daily njaaa mambo hayaendi,,

Hebu tupe tips za kujibana kama vipi tuziapply
 
Nimepata kazi mwanza, kama accountant, ndo kwanza wanaanza business, tatizo ni salary, wanatoa 500,000 kama take home. imenivunja nguvu, niko njia panda, kwenda au kutokwenda.... msaada.

hapo penye red patamu. kampuni ndio kwanza inaanza kazi wewe huoni kwamba kampuni hata bado haijaanza kutengeneza faida. sasa wewe unataka ulipwe Tsh. 1.5m eti? halafu ndo kwanza huna uzoefu (may be fresh frm college / university) unataka salary kama mtu mwenye uzoefu? nenda wewe kapige kazi mambo yatajipa hado hado hadi unakuwa na salary nzuri. pili usiache kazi wakati huna kazi ingine!
 
Back
Top Bottom