Jamani mbona vitu vimepanda ghafla

Huyu Arthur Lucifer ameongea ukweli
 
Mbona ccm walituambia budget ya mwaka huu imekuja kumkomboa mnyonge.
Ila kinachonishangaza ni kuwa tangu 2005 kila budget nasikia imekuja kumkomboa mnyonge, namshangaa huyo mnyonge sijui ni kwanini hataki kukomboleka

Unyonge ni mtaji wa wanasiasa mkuu,hawana cha kuombea kura zaidi ya hilo
 
Wewe utakuwa mpiga dili.. Ukiwa unapiga kazi kwa bidii mambo yatakuwa murua tu..kwasasa mnajengewa msingi ili mje muishi vizuri..majizi na wauza unga ndio wanaolalamika awamu hii..
Wachimba Makaburi na watu wa Mochwari hamuwezi kulalamika huu ni wakati wenu
 
Duh! Kila mwaka serikali inapotangaza bajet zake mfumuko wa Bei unaibuka. Hivi mm nashangaa Sana Hawa wafanyabiasha kwani hawaoni Kuwa mishahara haijapanda.?
 
Hao kuku sio wa kienyeji tena, hao kuku wa geti kali.
Ili aitwe wa kienyeji lazima akazurule ajitafutie riziki yake mwenyewe, wewe jukumu lako kumpatia malazi tuu
Mfuko wa 50kgs chakula cha kuku umepanda toka 40,000/- hadi 45,000/-.Halafu kuku wangu wa kienyeji nimewazoesha kuwapa chakula hawajui kudanga !
 
Tunaenda Mombasa
Jamani mmesahau nyanya, imepanda sana juzi nimenunua nyanya 1 shs 200 adi 300 yani nakula mboga chukuchuku na kitunguu tu tunaenda wapi jamani
 
Mimi mvutaji wa sigara nilikua nanunua paketi ya SM 2600 ika jana nimenunua 3400. Yaani imepanda shilingi 800. MATAGA
Kwa wewe naomba iuzwe hata elfu hamsini. Tunakupenda ndugu yetu na hatutaki utumie mabidhaa yanayodhuru afya yako.
 
Hahahahha
Hao kuku sio wa kienyeji tena, hao kuku wa geti kali.
Ili aitwe wa kienyeji lazima akazurule ajitafutie riziki yake mwenyewe, wewe jukumu lako kumpatia malazi tuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…