Daudi1
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 14,563
- 22,839
- Thread starter
- #141
JAMANI KWANI LAZIMA?-31
ILIPOISHIA
"Mimi ni mtu mzima wewe," alijibu mwanaume huyo.
Stela, ile anageuka ili afunge mlango kwa nyuma, Paulina anatokea…
"We ndiyo unaamka muda huu?" alisema Paulina huku akichungulia ndani ya chumba chake baada ya kuona miguu ya mtu…
JIACHIE MWENYEWE SASA…
"Na huyo chumbani nani Stela?" aliuliza Paulina huku presha ikianza kumpanda. Kwa ufahamu wa harakaharaka aligundua miguu ile ni ya mumewe, Mozie.
"Iko wapi?" Stela aliuliza kama hajui kitu na yeye alihitaji kuoneshwa…
"Unaniuliza iko wapi Stela wakati unajua iko wapi!" alisema Paulina na kusukuma mlango kwa kasi mpaka chumbani.
"Haa! Mozie," alisema kwa sauti na kuanguka chini akapoteza fahamu.
"Stela kimenuka," alisema Mozie…
"Ni kweli kimenuka, sasa itakuwaje? Kwani kafa?"
"Hapana, huyu kapoteza fahamu tu."
"Sasa tumkimbize hospitali au?"
"Hapana, atazinduka tu. Angekuwa ameanguka bila sababu hapo sawa lakini si inajulikana kuwa amepata mshtuko!"
"Sasa itakuwaje?" aliuliza Stela.
"Nimekwambia atazinduka tu," alisema Mozie huku akimshikashika Paulina sehemu mbalimbali za mwili na wakati mwingine akimpima…
"Nikwambie kitu baby?" alisema Stela…
"Unasemaje?"
"Hili ni tatizo kubwa, mimi naomba niondoke zangu. Huyu akiamka mimi sitakuwa na masikio."
"Hakuna kuondoka Stela, mimi ndiye baba mwenye nyumba hii."
"Mh! Haya," alikubali Stela akiwa ameweka mikono tumboni.
Muda ulizidi kwenda, dalili ya Paulina kuzinduka haikuwepo. Mozie alimuaga Stela kwamba anakwenda kwa baba Riziki kuomba msaada wa gari japokuwa hakuwa na amani na familia hiyo…
"Karibu jirani," baba Riziki alikaribisha.
"Asante. Samahani bwana, mke wangu ameanguka na kupoteza fahamu, sasa nilihitaji kumkimbiza hospitali mara moja."
"Tatizo nini?"
"Hata najua basi."
"Au mambo yake yale? Maana da! Unajua bwana mkeo anataka kukuzalia mtoto haramu, unatakiwa kuwa makini na eneo hilo.
"Mimi nakumbuka aliniambia anataka nilale naye nimpe mimba kwa sababu wewe una matatizo ya uzazi ndiyo maana alipopata ile mimba niliamua kudai mtoto wangu maana hata mimi mke wangu ana matatizo ya kizazi," alisema baba Riziki bila kuonesha kuwa anajali tatizo la mwenzake…
"Sasa baba Riziki ungempataje mtoto kwa mwanamke mwenye mume wake?"
"Si ndiyo maana tulimsainisha kwenye fomu akubali kuwa mimba ni yangu," alisema baba Riziki huku akifuata fomu moja iliyokuwa ndani ya bahasha juu ya kabati la vitabu sebuleni.
Aliitoa fomu hiyo na kumwonesha Mozie ambaye aliikubali kuwa sahihi aliyoiona ni ya mke wake bila wasiwasi wowote ule.
"Hodi wenyewe…baby mama kaamka," alisema Stela baada ya kupiga hodi na kuingia bila kukaribishwa…
"Baba Riziki ngoja niende. Unaniruhusu kwenda na hii fomu?"
"Nenda nayo tu, kwetu haina kazi tena."
Mozie na Stela waliondoka mbiombio hadi nyumbani. Walimkuta Paulina amekaa sebuleni. Alipomwona Stela alisimama na kutaka kumvamia na mimbamimba yake ili amtandike mabao ya usoni…
"Baby mkeo anataka kuniua," alilia Stela…
"We Paulina acha ujinga wako. Tulia huko."
"Mozie mimi nakwenda kujinyonga, hakyamungu vile. Leo hii Stela anakuita baby," alisema Paulina na kuanza kulia.
"Hebu kaa kwenye kiti hapo."
Paulina alikaa…
"Na wewe Stela kaa kwenye kiti kile."
Stela alikaa…
"Hivi we Paulina ni kwa nini unajifanya wewe ndiyo una nyama sisi wengine tuna mwili wa chuma? Hivi kwa uliyonifanyia wewe leo hii ni mtu wa kujifanya unajali maisha yangu?
"Hebu pitia mkataba huu wa wewe na baba Riziki kukiri kwamba ile mimba iliyotoka ilikuwa ya kwake. Angalia na sahihi yako, sahihi ya baba Riziki na sahihi ya mama Riziki kama shahidi," alisema Mozie na kumtupia bahasha miguuni…
"Mimi nilifanya vile ili kuondoa ung'ang'anizi wa baba Riziki."
"Upi?"
"Kusema mimba ni ya kwake."
"Una maana hujawahi kulala naye? Hata kama mimba haikuwa yake."
Hapo Paulina alinyamaza kwa muda kisha akainua uso kumwangalia Stela…
"Mama ungejibu maswali ya kwa baby kule, usiniangalie mimi," alisema Stela huku macho yake yote yakiwa kwa Mozie japokuwa alimsemesha Paulina…
"Stela iko siku nitakuua ujue."
"Huwezi kuniua…"
"Huwezi kumuua bwana, umuue mimi nitakuwa wapi?" alisema Mozie kwa sauti iliyotoka ndani ikiwa na kukwaruzakwaruza kwa jazba ya kuiona ile fomu ya makubaliano ya umiliki wa mimba kuwa ya baba Riziki badala ya yeye…
"Mozie kwa hiyo unataka kuniambia kuwa Stela ndiye mkeo kwa sasa?" aliuliza Paulina macho yakimtoka pima na mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi akisubiri jibu ambalo kama angeambiwa achague yeye lazima angechagua jibu lenye kumpendeza akilini mwake…
"Haswaa! Na hata mimba aliyonayo ni ya kwangu mimi. Sasa chagua mambo haya Paulina, wewe uendelee kuwepo hapa mimi na Stela tuondoke au wewe uondoke mimi na Stela tuendelee kubaki hapa."
STORI INATOKA KILA JUMATATU NA IJUMAA TUWE WAVUMILIVU KILA IKITOKA NITAIWEKA HAPA, TUONANE J3