Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 4,726
- 5,442
Sasa hivi huku mtaani matumbo ya wateule walioko kwenye nafasi ya ngazi ya Wilaya, yanapata moto kila siku. Wanasubiri kwa hamu ili wajue mbivu na mbichi. Hawana utulivu wa mwili na nafsi hasa wale ambao wanahisi nafasi ya kurudishwa ni finyu kwao.
Kwa upande mwingine, wale walio nje ya ulingo wanapiga jaramba, wakivizia kama fisi, ili kuona kama kocha atawapa fursa ya kuingia ulingoni wakati wowote kuanzia sasa.....
Naomba kuwasilisha.
NB: Mimi si miongoni mwao wanaovizia kama fisi au wale wenye matumbo moto. Mimi ni mpenzi mtazamaji..