Matukio yaliyopelekea kuaawa kwa marapa wakubwa Tupac na Biggie. Part 2

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,982
2,913
Inaanzia hapa Matukio yaliyopelekea kuaawa kwa marapa wakubwa Tupac na Biggie. (Pata kujua mhusika wa halisi wa mauaji hayo)

Kutokana na kuwa Tupac alikuwa kakosa ela ya kulipia dhamana ili atoke gerezani wakati mwanasheria wake akishughulikia rufaa, Suge aliona hii ndiyo nafasi pekee ya kumpata Tupac. Suge alimfuata Tupac akimtaka waingie mkataba amlipie fedha anayohitaji kwa ajili ya dhamana ila malipo ya Tupac itakuwa ni kurekodi nyimbo kwa ajili ya Death Row bure. Kwa watu wengi waliamini kwamba Tupac ni kama kauza roho yake kwa shetani (Suge), kwakuwa Suge knight alikuwa akifanya biashara ya muziki tofauti kabisa na wenzake akina Puffy kwa maana ya kwamba alikuwa akiifanya biashara ya mziki mfano wa kundi la genge la wauza dawa za kulevya. Na hapa ndipo Tupac alianza kuwa na muonekano wa kiharifu zaidi baada ya kuanza kujihusisha na Suge Knight na Death Row.

Wakati wa tafrija ya sikukuu ya Christmas ya mwaka 1995, mmoja kati marafiki na watu wa Puffy aliyejulikana kama Mark Anthony Bell, alidai kwamba alipelekwa ghorofani na kupigwa na wanachama wa Death Row akiwemo Tupac na Suge Knight mwenyewe. Aliendelea kudai kwamba alipofikishwa huko ghorofani alivamiwa na Suge Knight, Tupac na Dr. Dre pia wakiwemo watu wengine wanne ambao hakuweza kuwatambua.

Maelezo aliyoyatoa Bell kwa LAPD na kwa FBI, alidai kwamba Suge alikuwa akitaka apewe taarifa juu ya makazi wanapoishi familia ya Puffy huko Los Angeles au watu wake wakaribu. Hili tukio liliashiria kwamba Suge alikuwa amelenga kabisa kumdhuru Puffy.


Baada ya Tupac kuwa chini ya Death Row, alianza mashambulizi yake kupitia nyimbo zake, wakati huo huo Biggie yeye alikuwa tayari amekwishatoa wimbo ulikuwa unaitwa Who Shot You (Nani alikupiga risasi), ambao ulitafsiriwa kuwa ulikuwa ukizungumzia tukio la kupigwa risasi kwa Tupac huko Newyork. Katika kujibu mashambulizi Tupac alitoa wimbo uliojulikanakama Hit ‘Em Up mabao ni kati ya nyimbo kali za Diss katika historia ya mziki wa hip hop. Kwenye wimbo huo, Tupac alijitapa kuwa kalala na mke wa Biggie pia alitishia kuwaua wanachama wa wa Label ya Bad Boys. Hapa chini ni baadhi ya mistari inayopatikana kwenye huo wimbo wa Hit “Em Up

You claim to be a player, but I fu**ed your wife

We bust on Bad boys, nig**s fucked for life

Plus Puffyy trying to see me, weak hearts I rip

Biggie Smalls and Juniour M.A.F.I.A some mark ass b*tches

We keep on coming while we running for your jewels

Steady gunning, keep on busting at them fools

You know the rules.
Katika kipinidi cha majira ya joto cha mwaka 1996 miezi kadhaa baada ya tukio la kupigwa kwa rafiki yake Puffy, wanakikundi wa kundi lijulikanalo kama South Side Crips wakiwa katika jengo lenye maduka lijulikanalo kama Lakewood Center huko LA, walikutana na wanakikundi wa kundi pinzani lijulikanalo kama Piru Bloods na kuzuka mapigano. Kundi la MOB Piru Bloods lilikuwa na mahusiano ya karibu na Suge, na katika kundi hilo kulikuwa na jamaa anayejulikana kama Trevon Lane ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Suge na alikuwa kava mkufu wa Death Row ambao Suge alikuwa akiwapa marafiki zake wa karibu sana.
necklace.jpg

Nishni ya mkufu wa Death Row
trevon lane.jpg

Trevon aliyechuchumamaa

Mmoja kati ya wana kikundi cha The Crips aliyejulikana kama Orlando Anderson a.k.a Baby Lane, anaukamata mkufu aliokuwa amevaa Trevon na kuuioba. Greg anadai kwamba kutokana na taarifa walizozipata kutoka kwa mtoa taarifa wao (informer), inasemekana kwamba Puffy alikuwa ametangaza dau la dola 5,000 kwa wmanachama yeyote wa The Crips ambaye ataweza kumletea mkufu wea Death Row.
orlando.jpg

Orlando


Tarehe 7 mwezi wa 9 mwaka 1996 siku ya kuawa kwa Tupac

Siku hii kulikuwa na pambano la ngumi Mike Tyson. Kabla ya pambano baadhi ya wanachama wa kundi la MOB Piru walijumuika pamoja na wafanyakazi w Death Row katika tafrija iliyokuwa ikiendelea kwenye eneo la bar ya MGM GRAND HOTEL. Hii tafrija ilikuwa ni kabla ya pambano na waliokuwepo kwenye hiyo tafrija kutoka Death Row alikuwa Tupac, Mob James, Suge, MCDonald, Trevon, Kevin Woods and wengine wengi. Suge Knight, Mob James, McDonald na mwanachama mmojawapo wa kundi la “OutLaws” walikuwa wamebeba bunduki.

Baada ya tafrija, kundi la Death Row liliondoka eneo la bar na kuelekea kwenye ukumbi ambapo pambano lilikuwa likifanyika. Tupac alikuwa karekodi wimbo kwa ajili ya Tyson unaoitwa kama Mexican tha Don ambao ulipigwa pale Mike Tyson alipokuwa akiingia ulingoni. Suge Knight na Tupac wakiwa wamekaa eneo la ma VIP ambapo Tupac kwa muda huu alikuwa katika kilele cha umaarufu akiwa mmoja kati ya marapa wakubwa duniani.

Wakati pambano likiendelea, mmoja wa mashuhuda ambaye ni kachero wa FBI anadai aliona mabishano kati ya SUge Knight, MCDonald na baadhi ya waachama wa kundi la “Crip”. Shuhuda anadai kwamba alisikia mmoja kati ya wanachama wa the CRIP akimwambia Knight kuwa anahisi kuwa hawezi kamatika (Untouchable). Knight alimjibu kuwa yeye hakamatiki. Mmoja wa wanachama wa the CLIPS akamjibu kuwa Unaweza kukamatika,

Wakati Suge na kundi lake wakitoka ukumbini baada ya pambano, wakiwa bado kwenye neo la MGM Grand Hotel wanakutana na Orlando Anderson ambaye aliiba cheni ya Trevon Lane miezi kadhaa nyuma. Trevon Lane alikuwa na Tupac walipomuona Orlando akiwa katikati ya watu. Trevon anamng’oneza kitu Tupac na Tupac moja kwa moja anakimbia na kumvamia Orlando Anderson na mara kundi zima la Suge linamvamia Anderson na kumshushia kipigo. Tukio hili lilinaswa na kamera za hoteli. Walinzi w hoteli wanapoingilia ugomvi huo, wote wanakimbia na kuelekea nje ya ukumbi wa Kasino. Tupac akiwa mbele na Suge akiwa nyuma, watu wote wanamuona Tupac ambaye alikuwa ni maarufu sana kwa wakati huo na mara watu wanaanza kumfuata nyuma huku wakiita jina lake na wengine wakimshangilia.
orlando bet.png

Tupac, Suge n wanachama wa Death Row wakimshambulia Orlando

Baada ya hilo tukio Tupac anarudi hotelini aliko kuwa amefikia ambapo anakutana na mpenzi wake Kidada Jones ambaye ni mtoto wa mtayarishaji wa mziki ajulikanaye kama Quincy Jones. Tupac anawahadithia kilichotokea na anamtaka Kidada kutoambatana nao kwa kuwa ni hatari, hivyo Kidada anaamua yeye atabaki hotelini. Tupac hakuwa Gangsta aliyekubuhu ila alikuwa ameanzisha ugomvi na mwanachama wa The CRIP ambalo ni kundi hatari la uharifu. Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana alilolifanya.

kidada.jpg

Tupac akiwa na mpenzi wake

Tupac na Suge wanaamua kuongozana kwenye gari moja aina ya 750 BMW nyeusi, na walinzi wao wakawa kwenye magari mengine na ilitakaiwa waelekee kwenye Club iliyojulikana kama 662 ambapo kulikuwa na tukio la hisani na Tupac alitakiwa kuimba na baada ya hapo walikuwa wamepanga kula raha usiku mzima.
Biggie-Tupac.png


Kila mtu alijua kuwa Tupac atakuwa hapo kwakuwa matangazo yalitangazwa sana kwenye vituo vya redio, pia matangazo yalikuwa yamebandikwa kila mahali picha zake na karatasi zilikuwa zimesambazwa. Mike Tyson pia alitakiwa kutokea hapo 662, kumtazama Tupac akiwa anaimba jukwaani.

Msafara wa magari uliokuwa ukiwafuata akina Tupac na Suge ulikuwa na magari yasiyopungua sita. Wakati msafara ukiwa unakatiza barabara za Las Vegas ukielekea kwenye Club 662, Suge alikuwa anapiga mziki kwa sauti ya juu sana wakati huo Tupac akiwa kwenye siti ya abiria mbele wakiwa wanafurahia maisha na kusikiliza mziki wakiwa kwenye foleni. Askari wa Las Vegas wanasimamisha gari lao kwa kosa la kupiga mziki kwa sauti ya juu sana.

Wakati huo madada wawili marafiki Shelayne Turner na Ingrid Jonson walikuwa wamekuja nao kutembea Las Vegas wakiwa kwenye gari lao, ndipo walimwona Suge akiwa kasimama nje ya gari lake baada ya kusimamishwa na askari. Shelayne anaanza kupiga kelele akimwambia mwenzake muone Suge muone Suge na mara wanamuona pia Tupac.
Tupac anawaona akina dada anawambia kuwa njoo, njoo tuongozane pamoja, tufuate tunaelekea Club 662.
vlcsnap-2018-04-10-05h16m41s218.png


Wakati Suge aliporuhusiwa kuondoka, wakina dada hao wanachomeka gari nyuma ya gari lake hivyo wanakuwa kati ya gari la Suge na magari ya walinzi wa msafara.
tupac1.jpg



Msafara unaongozana kupita katika barabara za Las Vegas BLVD mpaka unapofika Flammingo ambapo wanakata kona kuelekea BLVD Club.
Wakiwa kwenye msafara wa akina Tupac, Ingrid anamwambia mwenzake kwamba wako kwenye msafara usiowahusu kwakuwa wao siyo wanachama wa Death Row wala hawahusiki kwenye msafara huo. Wanashauriana wajiondoe kwenye msafara kwakuwa wanajua unapoelekea basi wataenda wao peke yao bila kufuatana na msafara wa wakiina Tupac.

Msafara unapofika kwenye makutano ya barabara ya Flammingo na Koval, Ingrid anaondoa gari kutoka kwenye msafara wa Tupac kasha anaisogeza mbele na kupishana na ile BMW aliyokuwemo SUge na Tupac na kuzidi kulisogeza pembeni ya gari lilikuwa mbele kabisa

tupac3.jpg

tupac4.jpg

Mara nyuma yao wanaona gari nyeupe aina ya Moto Ford cardillac inayokuja na kusimama pembeni kulia kabisa ya gari la SUge upande alikokuwa kaka Tupac. Mtu aliyekuwa kaka nyuma ya hilo gari anatoa bunduki na kumuelekezea Tupac kasha kuachia risasi tisa, ambapo risasi nne ndizo zinazompata Tupac.

tupac6.jpg

Baada ya akina Ingrid kushuhudia tukio hilo, Ingrid anaamua kuondoka eneo hilo kwa kuingia barabara ya Koval kulia kwake na wakati akifanya hivyo lile gari jeupe nalo linaondoka hapo kwa mwendo mkali kuelekea upande huo huo alimanusura ligongane na gari la akina Ingrid ambapo gari hizo mbili zinaelekea upande wa kulia wa barabara ya Koval.

tupac10.jpg

Frank ALexender aliyekuwa mlinzi wa Tupac anaruka kutoka kwenye gari na kuanza kushambulia lile gari kwa risasi, huku Suge anaamua kupiga U-Turn na kumwacha Frank peke yake eneo la tukio akiwa katika mwendo wa kasi anagonga kingo za barabara na baadhi ya matairi yanapasuka hivyo kuilazimu gari kusimama.
tupac11.jpg


Wanachama wawili wa kundi la Piru ambao wameongozana na msafara wa Tupac wanaamua kuikimbiza ile gari nyeupe na kunatokea mashambulizi ya kukimbizana kwa magari lakini lile gari linafanikiwa kukimbia na kuwaacha.
Tupac anakimbizwa kwenye hospitali ya karibu ya hapo Las Vegas ambapo anafariki baada ya siku sita. Wakati akiwa hapo makundi ya watu wanajikusanya maeneo ya hospitali wakijaribu kupata taarifa juu ya hali ya Tupac. Kati yao kuna watu maarufu kama MC Hammer na mama yake Tupac Afeni Shakur.
afeni.jpg

Mama yake Tupac

Pia kati yao alikuwemo askari wa kituo cha Compton Unifies School huko Los Angeles anayejulikana kama Kevin Hackie ambaye alikuwa akifanya kazi kama afisa ulinzi wa Death Row, huyu anaanzisha vurumai hapo hospitali akidai kwamba yeye ni afisa wa FBI. Walinzi wa hospitali wanamtoa nje na kumzuia kukanyaga pale tena.

Huyu Hackie alikuja kusababisha kuibuka kwa tuhuma nyingi akidai alisikia hiki na aliona kile na kusababisha uwepo wa dhana nyingi juu ya uhusika wa serikali kitengo cha FBI katika mauaji hayo. Lakini wakati akihojiwa na gazeti la Los Angeles Times alidai ana tatizo la kupoteza kumbukumbu, pia polisi wanadai maelezo yake yabadirika badirika hivyo hawezi kuaminiwa.
Tarehe 13 mwezi wa 9 mwaka 1996, Tupac anafariki kutokana na majeraha yaliyosababishwa na zile risasi nne zilizompata. Watu moja kwa moja wanaanza kudai kwamba Orlando Anderson ndiye aliyempiga risasi Tupac kwakuwa tukio la kupigwa risasi kwa Tupac lilikuwa limetokea masaa mawili baada ya ugomvi wa Tupac na Orlando. Lakini kutokana na sababu ya kwamba Suge na rafiki zake hawakutaka kushirikiana na polisi kuhusu tukio la ugomvi baiona ya Orlando na Tupac, polisi wa Las Vegas walishindwa kumfungulia kesi Orlando kwa kuhusika na mauaji ya Tupac.

Kwa Suge Knight kifo cha Tupac ni pigo kubwa, siyo kwamba alikuwa kampoteza tena rafiki yake mwingine kwa mauaji ila pia alikuwa amempoteza mtu aliyekuwa akimuingizia pesa nyingi. Kutokana na uhusika wake katika ugomvi ule wa kumsambulia Orlando, Suge alijikuta akiwa kavunja masharti ya msamaha aliopewa na alikamatwa na kurudishwa jera alikokaa miaka mitano.

Siku iliyofuata baada ya kifo cha Tupac yani tarehe 14, mwezi 9 mwaka 1996, wanachama wa MOB Piru Blood ambao walikuwa washirika wa Suge Knight, walikutana kwenye bustani huko Compton inayojulikana kama Lueders Park. Walijadiri kuhusu mauaji ya Tupac na ushiriki wa wanachama wa The Crip hasa Orlando Anderson. Katika majadiriano hayo walikubariana kurudisha mashambulizi dhidi ya South Side Crips. Vita inaibuka kati ya makundi haya mawili ya Compton ambayo ni South Side Crips na Pirus kutokana na mauaji ya Tupac.
lueders.jpg


Miezi kadhaa baada ya kifo cha Tupac, Biggie Smalls na kundi lake la Junior Mafia wanaanza kurudi tena katika jiji la Carlifornia kutengeneza video na album yake. Kwa wakati huu ulinzi kwao halikuwa jambo la msingi maana Tupac alikuwa amekwishafariki na Suge alikuwa gerezani hivyo hawakuambatana na ulinzi wa maana. Jambo ambalo hawakulijua ni kwamba walikuwa wamejileta wenyewe kwenye nyavu ya mvuvi.

Tarehe 7 mwezi wa 3 mwaka 1997, Puffy na Biggie wanaudhuria tunzo za Soul Train Music Award huko Los Angeles na wao ndio wanaomkabithi tunzo ya wimbo bora kwa wanamuziki wa kike kwa upande wa R&B na Soul. Wakiwa steji wakati wa kukabithi, wanakumbana na kelele za kushangilia na kuzomea.

Huko nyuma ya ukumbi kunatokea mabishano na kutoelewana baina ya walinzi wa Bad Boys na wanachama wa jumuiya iliyojulkana kama National of Islam wanaodai kwamba Bad Boys wanwadharau kaka zao wa East, ugomvi huo unaisha baada ya Puffy kufika na kumwambia Mustapha Farrakhan ambaye ni mtoto wa Louis Farrakhan (Kiongozi wa Nation of Islam) kuwa wako poa hawana ugomvi au siyo. Mustapha anamaliza mvutano huo kwa kuwataka wenzake watulie.

Siku iliyofuata yani tarehe 8 ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya Biggie kuwa hai, aliwasiliana kwa simu na mama yake Voletta Wallace ambaye anaonyesha wasiwasi juu ya usalama wa mwanae huko Los Angeles. Biggie anamtoa wasiwasi mama yake kwa kumwambia kwamba ana askari wa kukodi wanaomlinda.

Usiku wa siku hiyo, Puffy na Biggie wanaelekea kwenye tafrija iliyokuwa ikifanyika katika makumbusho ya Petersen Automotive ambapo tafrija hiyo ilikuwa imeandaliwa na jarida la Vibe. Tafrija hiyo iligeuka na kuwa vurugu baada ya watu wengi kujitokeza mara mbili ya namba iliyokuwa inatarajiwa, huku kukiwa na walinzi kumi tu katika ukumbi ilikokuwa ikifanyika tafrija. Pia wasanii wapya ambao walikuwa wameanza kuwa maarufu wengi walihudhuria tafrija hiyo akiwemo Witney Houston pamoja na wacheza kikapu mashuhuri wa ligi ya NBA.

Baada ya ukumbi kujaa milango ya ukumbi ilifungwa na ambao hawakupata nafasi ya kuingia walijikusanya nje ya ukumbi na hali ilianza kuchafuka hapo nje maana kati ya watu waliokuwa nje kulikuwa na wanachama wa makundi hasimu. Ndani ya ukumbi wimbo mpya wa Biggie uliokuwa umeshika chati ulikuwa ukirudiwa mara kwa mara wimbo huo unajulikana kama hypnotize. Kama ilivyokuwa siku ya Tupac alipokuwa Vegas, Biggie siku hiyo alikuwa katika kelele cha dunia.

Majira ya saa tano usiku, askari aliyekuwa hapo anatoa wito kwa LAPD kufika eneo hilo kwakuwa watu wamekuwa wengi sana na watu waliofungiwa nje wameanzisha vurugu ambayo ulinzi uliopo hauwezi kumudu wingi wa watu hao. Usiku wa manane, askari anaamua kuzima mziki na kufunga tafrija iliyokuwa inaendelea baada ya kuhisi vuruga zinaweza kuwa kubwa zaidi. Wakiwa wamekaa ukumbini kwa masaa manne, Puffy na Biggie wanaamua kuondoka. Lakini kutokana na wingi wa watu na kuzongwa zongwa, iliwachukua karibu dakika 14 kufika kwenye magari yao.

Mnamo saa sita na dakika tano usiku, mashuhuda wanatoa taarifa ya kusika kwa milio ya bunduki maeneo ya kona ya Orange Grove iliyoko kwenye kona kusini mashariki mwa makumbusho ya Petersen. Mashuhudi waliweza kutaja mpaka namba za gari lilihusika pamoja na muonekano na aina ya hilo gari. Aina ya gari lilionekana lilikimbizwa kutoka eneo la shambulia ilikuwa gari jeusi aina ya Ford Blanca, ambapo baadae ilikuja kukisiwa kuwa tukio hili huenda ilikuwa ni kuwauza walinzi wafuatilie lile gari ili wauaji wapate nafasi ya kumuua Biggie.

Baada ya dakika zipatazo 30, Biggie na Puffy wanafanikiwa kutoka nje kabisa ya makumbusho hayo na walikuwa tayari kwa ajili ya kuondoka eneo hilo. Mmoja kati ya watu waliokuwa kwenye msafara wao anagundua kwamba kuna mtu anayetia mashaka yuko upande wa pili wa sehemu ya kuegesha magari akiwa anawatazama kwa kuibia ibia. Wakiwa wanasubiri magari yao yafike kuwachukua, aliyekuwa mlinzi wa Puffy ajulikanaye kama Eugene Deal ambaye alikuja kuwa mmoja kati ya mashuhuda wazuri wa tukio la kuawa kwa Biggie, anagundua kuna kijana mweusi mwingine anayewatazama jambo linalomtia mashaka zaidi baada ya kuona mtu huyo akiwa na mavazi sawa nay a wanachama wa Nation of Islam ambapo alikuwa kava suti ya blu, shati jeupe na bow tie ya blu pia.

Magari yanafika na kabla ya kuondoka Biggie akiwa kakaa siti ya mbele akizungumza na rafiki yake ajulikanaye kama Damion Butler aliyekuwa kasimama nje ya gari dirishani huku Daniel akisikika akijisifu “tumerudi Biggie, Tumerudi”(We are back Biggie, we are back). Biggie maneno yake ya mwisho kwa Damion ni “Tutaonana kwenye tafrija inayofuata”.

Kwenye msafara wao wa magari matatu ambapo kwenye gari lilitangulia Puffy alikuwa kaka mbele kwenye siti ya abiria huku nyuma ya gari kukiwa na walinzi watatu akiwemo Eugene Deal. Gari linalofuata lilikuwa likiendeshwa na Gregory G-Money Young, huku Biggie akiwa kwenye siti ya mbele ya abiria. Nyuma ya gari alikuwa kakaa mwanachama wa Junior M.A.F.I.A anayejulikana kama Lil Cease ambaye alikuwa binamu yake Biggie na vijana wengine wawili.

Gari la tatu ilikuwa nyeusi ikiendeshwa na askari polisi wa kituo cha Inglewood School huku kwenye siti ya abiria akiwa kaka mkuu wa idara ya ulinzi wa Bad Boy ajulikanaye kama Paul Offord. Wakati gari alilokuwemo Puffy likiondoka, Puff alikuwa kageuka nyuma akitazama gari ambalo Biggie alikuwemo huku gari la tatu likiwwa limezuia magari mengine yasipite ili gari la Biggie lipate kuingia barabarani. Wakati gari la Biggie likianza kuondoka, gari la Puffy linaongeza mwendo likielekea Kaskazini mwa Wolshire, gari la Biggie linaongeza mwendo pia ili lifikie gari alilokuwemo Puffy huku nyuma ya gari la Biggie gari la tatu likwia linajiandaa kuondoka pia. Mara ghafla gari jeupe linatokea na kupita pembeni gari la tatu lilikuwa na ulinzi kasha linaingia mbele yake na kuwa kati ya gari lenye ulinzi na gari la Biggie. Gari lenye ulinzi lasogea kushoto na kwa mwendo wa kasi linalitangulia lile gari jeupe na kuingia mbele yake likizuia kulikaribia gari la Biggie. Watu wengi wanahisi hili gari jeupe lilihusika pia katika mauaji ya Biggie.

Wakati haya yote yakiendela gari jeusi linatokea na kuelekea pembeni ya gari la Biggie na aliyekuwa akiendesha gari hilo anayedaiwa kuwa alikuwa Africast anatoa bunduki aina ya Semi-automatic Pistol akiwa kaishikiria na mkono wa kulia huku mkono wake wa kushoto ukiwa umeshika usukani wa gari anaanza kurusha risasi kuelekea kwenye mlango wa gari upande aliokuwa kaka Biggie. Baada ya kufanya shambulizi hilo, mshambuliaji anageuza gari haraka na kuelekea uelekeo wa Wolshire BLVD (BLVD maana yake ni barabara kubwa inayopita katikati ya mji).

Gari lililobeba walinzi wanajaribu kumfukuzia lakini anafanikiwa kuwatoroka na kuwaacha. Wakati huo gari lililokuwa limembeba Biggie lilikuwa limesimama na gari lilikuwa limembeba Puffy linageuza na kurudi ili wajue ni kitu gani kimetokea. Puffy anateremka na kukimbilia kwenye upande aliokaa Biggie ambapo anagundua kwamba Biggie kapigwa risasi, anafundua mlango huku akimuita lakini Biggie haitiki. Inawachukua karibu dakika tano kumkimbiza mpaka Cedars-Senai Medica Centre iliyoko Baverly Hills. Mnamo muda wa saa saba na dakika 15 usiku, madaktari wanamtaarifu Puffy na Faith Envas aliyekuwa mkewe Biggie kuwa Biggie amekwishafariki.

Ripoti ya daktari inaonyesha kwamba alipigwa risasi nne na risasi iliyomjeruhi sana na kusababisha kifo cha ni risasi iliingia kupita ubavuni inaharibu mapafu yake na kuingia kwenye moyo. Madaktari walisemakwamba kuwa Biggie atakuwa alikufa muda mchache tu baada ya kupigwa risasi.

Kesho yake habari ya kuawa kwa Biggie inasambaa, nadharia nyingi zinaibuka watu wengi wakihusisha mauaji ya Biggie na mauaji ya Tupac miezi sita iliyopita.
Tarehe 18 mwezi wa 3 mwaka 1997, mazishi yake yanafanyika huko New York. Watu walijipanga barabarani wakati msafara wa kupeleka mwili wake huko Brooklyne.
vlcsnap-2018-04-10-04h50m53s74.png

Wiki moja baadaye albamu yake iliyoitwa Life after Death (Maisha baada ya kifo) inaachiwa, ambapo ilichaguliwa kuwania kuwania tunzo tatu za Grammy na iliuza zaidi ya nakala 10,000,000 huko Marekani pekee.
vlcsnap-2018-04-10-04h53m44s79.png


******************Itaendela********
 
Sawa sawa ni hadithi nzuri ila ni ndefu, weka audio au video, mtu anasikiliza au anaangalia mara moja paap
Tafuta documentary inaitwa "who killed Tupac?" Ndio jamaa kaitoa huko..kuna theories 5 kuhusu nani alimuua PAC ila zote ni zina Dead end hivyo aliyemuua PAC wala hatajulikana hadi mwisho
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom