jamani hofu ya nini interview dodoma?????

Feb 8, 2011
14
2
Mi naona tatizo ni ukosefu mkubwa wa ajira na uongozi mbovu wa chuo kuita watu wote tulioapplly.
Tufanye nini basi: kwa wale wenye nauli zao waende huko kwa tusionazo kukopa kwa ajiri hii uwezewekano wa kudaiwa/kutolipa mkubwa.
muhimu: Ikiwemo tanzania soko la ajira linatanuka sana tutaanza kuitwa kwenye interview za dunia nzima tuanze kusoma hizi nyakati na kujiandaa na mashindano hayo hasa soft skills ambalo ni tatizo kubwa kwetu graduate wa tanzania.

SAFARI NJEMA MNAOELEKEA HUKO...MAOMBI YANGU NI KWAMBA WALE WENYE SIFA NA SIO BAHATI AU VINGINE!!!!!!!!
WENYENCI NDO TUTAKAO IJENGA TANZANIA.
 

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Interview ya watu 1000, ndiyo mara ya kwanza kuona mie! Hapa najiuliza, inakuwaje watu wote hao wawe na sifa zinazolingana sana mpaka screening imeshindikana?

Hata hivyo nimeambiwa leo na kesho wanaenda kufanya mtihani wa kuandika, nadhani baada ya hapo huenda ikafuata ile face to 'face interview'.
 
Feb 8, 2011
14
2
labda wameona kuchagua kwa cv tu haitoshi/haiwi na matokeo mazuri so wakapigwe pepa ndo wafanye 1st screening...Looo kazi!!!!!
 

Jeff

JF-Expert Member
Sep 26, 2009
1,290
194
labda wameona kuchagua kwa cv tu haitoshi/haiwi na matokeo mazuri so wakapigwe pepa ndo wafanye 1st screening...Looo kazi!!!!!

watu 1000? Huko dodoma hali ikoje ya malazi na usafiri? Mana jana nilishuhudia usafiri wa dodoma ulivyokuwa mgumu kwa baadh ya maeneo kama Chalinze na Moro,mi nikaona ujinga huu sikuenda,walioenda watujuze hali halis ya huko jaman,ili tujifunze
 

Kwetu Iringa

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
355
88
Interview ya watu 1000, ndiyo mara ya kwanza kuona mie! Hapa najiuliza, inakuwaje watu wote hao wawe na sifa zinazolingana sana mpaka screening imeshindikana?

Hata hivyo nimeambiwa leo na kesho wanaenda kufanya mtihani wa kuandika, nadhani baada ya hapo huenda ikafuata ile face to 'face interview'.

Siyo 1000, ni 2500!!!

Hapa dodoma pana shida kubwa sana ya kupata pa kulala maana wanafunzi (kama 20,000 hivi) wameingia jana pamoja na hao wanaotafuta kazi. Wanafunzi wamefikia mjini siyo chuoni kamma miaka yote!!
 

Parachichi

JF-Expert Member
Jul 22, 2008
511
98
duu!hiyo ni balaa!kwani nafasi zipo ngapi wakuu hadi wachukue sample yote hiyo?polen aisee
 

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,888
1,326
duu!hiyo ni balaa!kwani nafasi zipo ngapi wakuu hadi wachukue sample yote hiyo?polen aisee

Mi nimeona nisiende kwenye hiyokitu maana kama jina ni la 600 na kitu kuna watu 1400 na kitu unaona possibility ni ndigo...........
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
13,325
10,612
Du paper ni kali hasa na si ya kutgemea maana watahiniwa ni 1580 na msimamizi anakuambia wanatakiwa 10 tu.
Sasa kwa wale ambao tumesomea vyuo tofauti na vya kulala maana Warden unaulizwa iwapo mwanafunzi anataka kutoka kwenda town na ndani ya semister anafanyaje?
kuna tuliotoka majumbani au vyuo km Moshi ushirika enzi hizo unafunga mlango na kusepa zako, sasa sijui UDOMunakabidh9i funguo, godoro, sanduku au unampa chochote warden kweli kufeli kupo tutawajuza kesho kuna accounts na supplies & procu
 

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
Jana nilisema kwenye thread moja hapa kwenye jukawaa hili,kwenye Human Resource Recruitment and selection practices hakuna kitu kama hiki,mfano kwenye nafasi ya Administrative officers/HR wanataka watu 12 lakini nilichokiona leo kulikuwa na watu zaidi ya 2000..Tafuta ratio hapo.Ni kweli kwamba HR principles zinasema ili kupata competent applicant ni vema ukawa na reasonable number of applicants depending on the number of vacancy you have..sasa kwa UDOM hii ni kituko,ki-ukweli kuna tatizo kubwa sana la kiutawala pale UDOM..na nachelea kusema HR wao na wasaidizi wake ni buree kabisa.....
 

Mama ibu

Member
Aug 28, 2011
31
9
Mi ndo niko njian narud dar toka uko dodoma kiukwel wa2 walikuwa wengi sana na huo mtihan wa Hr ulikuwa balaa jamani kilichonifurahisha nimekutana na classmates wangu kibao tangu wa primary, secondary na chuo lkn cna hata hope ya kufuzu na hata ikitokea cwez poteza naul yangu bure
 

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,735
1,195
Du paper ni kali hasa na si ya kutgemea maana watahiniwa ni 1580 na msimamizi anakuambia wanatakiwa 10 tu.
Sasa kwa wale ambao tumesomea vyuo tofauti na vya kulala maana Warden unaulizwa iwapo mwanafunzi anataka kutoka kwenda town na ndani ya semister anafanyaje?
kuna tuliotoka majumbani au vyuo km Moshi ushirika enzi hizo unafunga mlango na kusepa zako, sasa sijui UDOMunakabidh9i funguo, godoro, sanduku au unampa chochote warden kweli kufeli kupo tutawajuza kesho kuna accounts na supplies & procu

hahahahaaaa,,,,,mdau umenchekesha,,,,ile pepa nouma,,,,mi nipo mlandiz narud
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,133
17,099
mi nimeona nisiende kwenye hiyokitu maana kama jina ni la 600 na kitu kuna watu 1400 na kitu unaona possibility ni ndigo...........

nasikia mkifungana maxi wanaanza kiuanga alphabetic a-z kama babazenu waliwaita zawazdi,zilipendwa zakiemu shuguli mnayo mkizaa andrew,allaan,alia bado yana manufaa kwenye maisha ya watoto wenu wa baadae muwe makini kutoa jina
 

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,711
3,658
Hahaaaaa et what does it mean when client is nodding a head during cancelling?,who are the co workerz of a warden?what are the duties of Jeniters?what is try and error?kudadadadeki walai sasa mi aya nayajulia wap mie?..yamenitoa kapa kudadeki...yan uhaba wa ajira huu unantesa ivi?imekula kwangu...duh ndo nipo Mpunguzi narud zangu Mibikimitali nkalime Vinyungu..haikuwa na maana ya shule kama kaz ndo magumashi ivi...nasbir wakutngza barabara nibebe mtutu
 

Kampini

Senior Member
Jul 15, 2011
140
28
Mie nilikabidhiwa ofc leo Admin,nyie wengine mlikuwa mnatusindikiza tu watoto wa wenye nchi. Bakieni tu kuwa wananchi mtapigwa mapaper hadi basi.
 

adoruta

Member
Apr 25, 2011
5
1
According to human resources recruitment and selection precedures, the number of interviewee should be short listed depending on the number of position available. Hivyo, siasa imefanyika badala ya kutumia utaalamu. Kwa hali huyo naona kuwa zoezi zima ni batili, warudie upya!!!!!
 

POLITE MAN

Member
Oct 14, 2011
41
7
muraaaaa, mi nimenda lakini tulicho kishuhudia pale udo ni aibu tupo, sidhani kama serikali inatake siliazi na usimamizi wa mambo yake, wakati tupo pale yule msimamizi wa mitiani amesema kama kuna watu walishafanya ile mitiani basi wasifanye tena, tukajiuliza kinanani ambao walishafanya, baadae nikapati nafasi ya kuongea na jamaa mmoja wa pale amesema ndio watu walishaitwa na walifanya ile interview ivo awaluhusiwi kufanya tena, je kama walishaita watu wachache mara ya kwanza kwanini walituita tena mara ya pili tena kwa wingi sana, baadae nikambiwa kumbe kunawatu ambao walikuwa wanafanya kazi kwa mkataba wameambiwa waombee na ndio watawakonsida kwanza,
SISI MAZEE TUMENDA KUFANYA TOUR TU PALE UDOM
 

POLITE MAN

Member
Oct 14, 2011
41
7
UDOM wasanii wa hali ya juu kumbe walishaita watu sasa inaonekana baada ya wanajamii kulalalmika na kuulizia sana kuusu kazi ambazo zilitangazwa pale wakaona watuite tena mara ya pili tena kwa fujo, asa we angalia ushindani gani ambao wameutaka , nafasi 2 wameita watu 307, je uyo HR amesomea kweli kazi yake au ndio nae alikuwa amewekwa tu ameokotwa mtaani alikuwa anauza vitunguu na nyanya, WOTE TUNA HAKI YA KUFANYA KAZI KATIKA SERIKALI HII LAKINI BAADHI YA WALIOPEWA MADARARKA WANAONA WAO WANAHAKI ZAIDI
 

kaygeezo

Senior Member
Jul 31, 2008
193
10
Tumerudi salama from Udom ,nime enjoy self driving ,maana usafiri wa basi ulikuwa utata ,na pia kuonana na class mates wengi ,issue ya ajira nsha ipotezea ,watu wengi post chache pepa ngumu.ova!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom