GE2025 Ninachokiona katika jamii yangu baada ya uchaguzi kituko kwa dunia

GE2025 Ninachokiona katika jamii yangu baada ya uchaguzi kituko kwa dunia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Trayvess Daniel

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
705
Reaction score
1,369
Sio kitu cha kuumiza kichwa...
Yatakuja maandamano makubwa zaidi na umwagaji mkubwa zaidi LAKINI WENYE USHINDI.

Lini? Muda utaongea

Kwanini? Shida ni mwalimu mzuri sana.

Shida itatokana na nini?

Pesa nyingi itaenda kuendelea kutengeneza cartel ya kujilinda

Resources nyingi zitaenda kwa nchi zingine ambao wameshaona udhaifu wetu na watautumia huo kupata resources zetu kiulaini, ukianza na UAE (huwa hawana jema kila African country wanayoenda mfano mzuri SUDAN)

1. Kwa sisi watu wazima tuliopo tu(millenials sanasana), watu wa public sector walikua tayari wanakula shida hata kabla hatujaingia kwenye ukoloni mpya, posho posho, per diem na yanaendana na hayo havikuwepo ofisi nyingi....

2. Huduma za kijamii zilishakua shida, hospitali, shule, maji, umeme.... etc

3. Private sector uwezo wao wa kuajiri unategemea mzunguko wa pesa mtaani, kama mtaani hamna mzunguko hata wao ni mwendo wa kuminya ajira na kuhadaa vijana kwa internship ili wawalipe kiduchu

5. Government ndo kabisa, huko ajira ni mtihani, jobless wa zamani na wapya ni wengi sana. Na mambo hayaendi kuwa mazuri. Magufuli alitengeneza imbalance ya ajira na huyu Iddi Amin kazidi kuendeleza na kuharibu zaidi

6. Graduates wengi ni mawinga na bodaboda, miaka michache ijayo (sio hata mitano) mawinga na bodaboda watakua wengi kuliko wateja. Vurugu juu ya vurugu

7. Watu wenye biashara za kati, mzunguko hautokua kama mwanzo sababu wengi wanategemea watu wenye kipato stable wapate huduma au wanunue bidhaa so hata spending haitokua kivile so tayari ugumu wa maisha huo

8. Bomu kubwa kuliko yote tuna zaidi ya watu milioni 20 ambao walikua watoto chini ya 15+ sensa ya 2022, kuanzia mwaka huu kila mwaka kuna kundi la miaka 18 jipya, 7 years later tutakua na kundi kubwa la vijana 18-25 years wasio na muelekeo wa ajira wala kujiajiri. NI BOMU HILO

9. Kodi na tozo hizo sio habari mpya mjini, tutajua hatujui. Bado hatujasema

10. Akijichanganya aendeleze michezo ya kuprint hela, shughuli yake wengi tunaijua. Nchi ni itatank kuliko kawaida.

11. Nchi imeharibiwa na watu wachache wenye tamaa na uwezo mdogo wa kufikiri na kuona mbali, matokeo yake tutaanza kuyaona sasa na vizazi vingi vijavyo mpaka ukombozi wa kweli upatikane

12. Nje ya box, nguvu iliyotumika kupora haya madaraka, mimi ningekua yeye nisingeachia nchi mpaka kifo kinitenganishe. So kiutani utani bila kuchukua hatua tunaweza kuwa na M7 wa Tanganyika. Madam eternal president

13. Maendeleo hayaletwi na rasilimali sababu tunazo nyingi sana, ila yanaletwa na utawala bora, na kibaya zaidi tunatawaliwa na walafi wa madaraka wenye uwezo mdogo kiuongozi. Je unadhani kuna Tanzania ya nama na asali bila mabadiliko???? Amka usingizini buda, safari ni ndefu.

Mungu ibariki Tanzania, hakuna AMANI BILA HAKI.
MPAKA HAKI IPATIKANE HAKUNA TANZANIA BORA

Some will be dead when that happens and some will live to see it, no matter how long it is going to take.

Nchi imeharibiwa na watu wenye tamaa na uwezo mdogo wa kufikiri na kuona mbali, matokeo yake tutaanza kuyaona sasa na vizazi vingi vijavyo mpaka ukombozi wa kweli upatikane
 
Mbaya zaidi king'ang'anizi mwenyewe wa madaraka uwezo wa kuleta mabadiliko na tija, hana! Zaidi anaishi kwa kuwategemea wahuni na matapeli kumshauri!
 
Mbaya zaidi king'ang'anizi mwenyewe wa madaraka uwezo wa kuleta mabadiliko na tija, hana! Zaidi anaishi kwa kuwategemea wahuni na matapeli kumshauri!
Anauza taifa kwa nchi zingine zenye akili... mpaka kukuche nchi itakua tupu na machafuko. Walau wakoloni walituachia miundo mbinu huyu ataacha umasikini na unrest
 
Back
Top Bottom