Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,570
- 19,447
Nilipokuwa hapo UDSM miaka ya themanini, tulikuwa tunatumia term system badala ya semester. Kati ya mambo ambayo sikupendelea wakati ule ni kwamba University Exam ilikuwa inafanyika mwisho wa mwaka baada ya term tatu na ilikuwa inahusisha mambo yaliyofundishwa mwaka mzima! Kule Engineering kulikuwa na masomo ambayo yalikuwa yanafundishwa mwaka wa pili na wa tatu kabla ya kupata University Exam, kwa hiyo mwanafunzi anakumbana na mambo aliyofundishwa miaka miwili iliyopita. Supplementary Exam ilikuwa ni kama lifeline pekee kwa mwanafunzi aliyefeli somo ambapo alikuwa anapewa miezi mitatu kujiandaa tena na kurudia mtihani aliofeli kabla hajalazimika kurudia mwaka wote ikiwa ni pamoja na yale aliyopasi. Tuliupigia kelele mfumo ule na leo nasikia kuwa higher education system yote Tanzania wanatumia mfumo wa semester.
Chini ye semester system, nina imani kuwa mwanafunzi akifeli somo anatakiwa arudie tena kusoma somo hilo alilofeli kwa semester nzima, siyo kupewa supplementary exam. Kama bado UDSM inatoa supplementary exam chini ya mfumo wa semester, basi wanawasaidia wanafunzi wao sana. Kwa vyuo vingi vya marekani hasa nilikosoma na nilikowahi kufanyia kazi, huwa hakuna kabisa kitu kinaitwa supplementary exam. Unafeli somo, basi inabidi ulichukue tena semester ijayo hadi utakapopasi. Kuna chuo kimoja kilikuwa na utaratibu wa kuonyesha lwenye transcript kuwa ulirudia somo mara ngapi.
Ni muhimu sana wanafunzi mnapokuwa mashuleni mzingatia masomo yenu na kupasi masomo yote bila kuchagua. As long as somo liko kwenye list yako, ni lazima ulichukulia kwa maanani sana somo lile na uhakikishea unalipasi bila kujali unalipenda au la. Kumbukeni kwa waalimu wote hupenda wanafunzi wao wapasi kusudi wafanikiwe maishani mwao, hasa kwa kutumia mambo waliyowafundisha. Binasi, niliwahi kukutana na mwalimu wangu aliyenifundisha hesabu form 2, na aliposikia kuwa wakati huo nilikuwa mwalimu wa engineering, aliita waalimu wenzake wote pale shuleni kuwatambia kuwa hesabu alizonifundihsa ndizo zimenifanye nami niwe mwalimu wa engineering. Kila mwalimu huona ufahari sana anapokutana na mwanafunzi wake wa zamani aambaye amefanikiwa maishani, na vile vile huona aibu sana kukutana na mwanafunzi wake aliyeshindwa mwaisha. Unapoona mwalimu anakukazania usome na kutaka upasi mtihani aliokupa kwa kiwango fulani, ni kwa sababu anajua kuwa hutakuwa mjuzi wa mambo aliyokufundisha bila kufikia kiwango hicho. Unapokuwa shuleni, zingatia sana shule yakeo. muda wako shuleni ni mfupi sana, miaka mitatu au minne tu; baada ya hapo utakuwa na muda wote kiuutumia upendavyo, kama utakuwa na bahati hiyo.
Kumbukeni tena, chuo kikuu siyo kama chooni ambako kila mtu anaweza lkwenda.