Kila mtu analijua hilo swali ni kwamba una suluhisho gani bora au unashauri nini?????
Ukijua kusoma jibu lako lipo katika post hiyo hiyo.
Mfumo wa elimu Tanzania umejengwa katika system ya "exclusivity". Mwalimu wa Sociology hana incentive ya kukupasisha, ana incentive ya kukufelisha kwa sababu.
1. For some reason mwalimu anayefelisha wengi ndiye anaonekana mzuri.Kwamba somo lake "gumu" na ni vipanga tu ndio wanaweza kupasi.Wakati ukweli ni kwamba ukifelisha watu zaidi ya 50% wewe mwalimu na mfumo wako wote inabidi mji re-evaluate.I was typing this while Kiuyajibu was typing the above post, baada ya kupost naona tumeandika swala moja, kwamba mwalimu anayefelisha anaonekana anafanya vizuri kuliko mwalimu anayepasisha.Kiuyajibu ameweza hata kutoa mfano wa Mholanzi, lazima alichoka na system yetu.Vizee vinaogopa kuondolewa.
2. Kutokana na exclusivity yetu, na ufinyu wa ajira, priofession zinakuwa ni kama "guild" fulani.Walimi hawataki watu wengi wapasi halafu kuje kuwa na competition kubwa katika industry, tena wengine wanaona vijana wanakuwa wakali kuliko wao wanaona ni bora wawe na pre-emptive strike.
Having said that a good number of the 50% ni watu wenye matatizo ya lugha and all ambao somo kama Sociology ukiwa Maimuna unashindwa hata kufeki inakuwa mambo si mambo.Lakini naamini michujo ya form 4 na six imewaondoa wengi hawa na hata waliobaki wanaweza kuboronga tenses lakini wakabaki na mantiki.Sasa hapa ndipo inategemea Prof ni strict kiasi gani, anaweza kumlima mtu kwa sababu ya lugha very fairly, lakini wengine wanaweza kusema mtu kama ana point na matatizo ya lugha anapeteshwa.
Tunahitaji ufumbuzi kwenye mfumo mzima wa elimu, kuanzia na kuandaa uchumi utakao consume hii elimu.Ikiwa kuna projects za kiuchumi za kutosha za ku demand wasomi kutakuwa hakuna haja ya kufelishana kwa kuogopa kuzibiana nafasi chache za kazi.
Pia walimu wanahitaji kuwa monitored na reviewed more closely.Sina uhakika kama walimu wanakuwa reviewed na wanafunzi UDSM.lakini ni muhimu.
Halafu mfumo wa elimu unahitaji kumuandaa mtu kuongea na kuandika kiingereza tangu madarasa ya chini kabisa ili akifika juu hili swala lisimtatize.
Kuna maswala mengine pia, kama culture nzima ya usomi na usomaji, kuthamini watu, empathy, principle, equanimity (which would call for a curve in this particular case) and the likes.