Jamani huku mlimani kuna DR mmoja wa Sociology (jina lipo) amekuwa na tabia ya kukamata wanafunzi wengi sana hasa finalists. haina maana hawasomi ila ni kama kuwakomoa tu. mfano mzuri ni mwaka huu kakamata wanafunzi 88 kati ya wanafunzi 190. mimi pia ni mwathirika na nilikuwa nasoma sana kwa kadri ya uwezo wangu. masomo yote nimefaulu vizuri ila yeye tu ndo kanikamata. naombeni tushauriane kwa hili kwani sasa niko mkoani sins kazi, je hiyo naulu ya kuja kufanya supplementary nitapata wapi? maisha yamshakuwa magumu ndugu zangu. aksanteni
Pole sana
Sipo, kwa mambo anayofanya huyo Dr was Sociology. Ni kweli baadhi ya lecturers wana majivuno na wanafikiri kum'felisha' mwanafunzi ndiyo kutukuka kwao. Ni ujinga tu!
Rafiki yangu mmoja ni lecturer hapo UDSM. Naye ni Dr lakini ni 'fair'. Huwa ananiambia lecturers wenzake wanamlaumu kwa vile wanaona kwenye masomo yake wanafunzi wanapata maksi nzuri. Walikuwa wanamshinikiza naye aanze kuwapa maksi ndogo ili aonyeshe 'solidarity'. Ila aliniambia, yeye hawezi kufanya upuuzi huo kwani anatoa maksi kulingana na jinsi mwanafunzi anavyojibu au kufaulu kuliko wenzake wanavyotaka afanye. Nami nilimsihi asilegeze msimamo.
Huyu Dr (rafiki yangu) tulisoma kwenye mazingira yanayofanana. Masomo yalikuwa magumu sana na mengi, ila yanayojenga uwezo wa kufikiri na kufanya uamuzi sahihi.
Kwa upande mwingine, wanafunzi wengi wanataka kusoma bila kuhangaika. Wanataka ikiwezekana wafundishwe majibu ili wapate maksi za juu. Walau mimi sikusoma katika mazingira hayo. Mfano, walimu wetu walikuwa wanakazia zaidi uelewa wa mtu kuliko maksi. Mfano, mwalimu anaweza kutoa swali ambalo halina jibu moja na anataka maelezo yako ndiyo yafanye akupe maksi nzuri kuliko kujua, mfano, maji yanachemka katika nyuzi ngapi usawa wa bahari.
Kusoma kwa kukariri majibu ndiko kunakoleteleza wanafunzi wengi washindwe kufanya vizuri kwenye masomo yao. Ningekuwa mwalimu wa chuo kikuu, hakika wanafunzi wangu wasingeshindwa. Chuo nilichosoma mimi (siyo hapa Tz, of course) katika mwaka wetu lowest ilikuwa BA (Honours) ya 2.2. Hakuna aliyepata chini ya hapo. Ila wa first class - haikutegemea tu maksi za darasani lakini pia jopo la walimu ambao licha ya maksi waliweza kujadili kama kweli mwanafunzi fulani anastahili first class.
Cha kufanya katika nchi yetu, hasa katika vyuo vyetu ni kubadilika wote - wanafunzi na walimu. Yaani, namna yao ya kufundisha ibadilike kabisa na vilevile wanafunzi wabadilike katika kujifunza. Sisi mwaka wetu wa 1 tulifanya 'memory test' ili kujua mwanafunzi ana uwezo kiasi gani wa kukumbuka katika masomo magumu na pia rahisi. Baadaye tulipata ushauri kulingana na 'performance' ya kila mmoja wetu - kujua strong na weak points za mwanafunzi.
Kwa bahati mbaya sana, katika vyuo vyetu hakuna huo mpango na pia wanafunzi hawajifunzi 'study methodology'. Mimi nilipoanza mwaka wa kwanza, tulifanya 'induction week'. Yaani, unapata 'introduction' ya kila facility chuoni kabla ya kuanza rasmi masomo.
Muda huo ilikuwa inaruhusiwa pia kubadilisha masomo, hasa baada ya kupata 'introduction' ya kutosa kuhusu 'programmes' zinazotolewa chuoni. Pia, pamoja na masomo tuliyokuwa tunafundishwa, ilibidi tuendelee kujifunza lugha - Kiswahili (kwa wale wasio kifahamu vizuri), Kifaransa na Kiingereza na pia lugha ya watu waliotuzunguka.
Hali hii ilinipa mwanzo mzuri katika elimu na hadi sasa bado najiendeleza kwa kununua vitabu na kusoma mwenyewe. Sasa hivi nachukua masomo ya sheria, lakini hata kama nashindwa kuhudhuria tuition, najisomea nyumbani na napata maksi nzuri zaidi hata kushinda wale wanaohudhuria tuition.
Kwangu kuibiwa mtihani ni kufanya 'intellectual masturbation'. Kwa kifupi, kuanzia elimu ya sekondari nilijitahidi kujifunza peke yangu bila kumtegemea mwalimu. Siyo kwamba nawadharau walimu ila nasema kwamba hata kama mwalimu hafiki darasani bado nasoma mwenyewe na kuelewa.
Nilikuwa najitahidi kusoma chapter moja zaidi ya wenzangu katika kila somo na hii iliniwezesha kufanya kama marudio wakati mwalimu alipokuwa anafundisha.
Mtu mwingine anaweza kufkiri mimi ni genious, la sivyo. Mimi ni mtu wa kawaida tu ila nimejiendeleza sana katika kutafuta njia mbalimbali za kujifunza karibu katika kila mazingira (including concentration skills).
Nilijizoeza, mfano, wakati nafanya kazi library kuazimisha wanafunzi wenzangu vitabu bila kuandika majina yao na nilijua nani kaazima nini, tarehe gani na anatakiwa kurudisha nini. Inanisaidia pia mtu akikopa hela kwangu siandiki kwenye daftari ila nitaweka kichwani tu na kujua ni kiasi gani na tumekubaliana arudishe lini.
Kwa kifupi, Mungu ametujalia vipaji vingi sana na inabidi tu'explore' talents zetu na kuzitumia. Mara nyingi tunakata tamaa tukiona mambo yanakuwa magumu. Anza leo kujitahidi na utaona utakuwa na mabadiliko mengi tu katika masomo yako na katika maisha yako pia.
Jitahidi kujifunza mambo mengi kwa muda mfupi na utaona unafanikiwa! 'Programme your brain and you'll see wonders' na hata utaweza kuwaelimisha watu kama hao akina Dr wa Sociology. Sisi bwana tulikuwa tunasoma na hata kukosowa walimu katika uelewa. Yaani, mtu aki'argue' hata mwalimu haoni ndani.