Jamani haya ya Sitta ni ya kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani haya ya Sitta ni ya kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msongoru, May 8, 2009.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na Samson Mwigamba


  NAAM! Nimetaja Spika Sitta Group kwa kuwa si peke yake. Kuna kundi la wanachama wa CCM wanaoishi ndani ya CCM lakini kwa mtazamo wa juu juu wakionekana kana kwamba hawatendi matendo ya CCM. Ni kama vile wanatimiza ile kauli ya Yesu, aliyowaasa wafuasi wake kwamba waishi ndani ya ulimwengu lakini wasitende ya walimwengu.

  Ama wachangamane na watu wa mataifa lakini wasitende matendo ya mataifa. Ndivyo mtazamo wa juu juu unavyoweza kuwaonyesha hawa wana mtandao mpya ambao nimeupachika jina la Spika Sitta Group (SSG). Ndani wamo akina Harrison Mwakyembe, Anne Kilango Malecela, Lucas Selelii, Christopher Ole Sendeka, William Shelukindo, Said Nkumba, Lazaro Nyarandu, n.k, hawa ni wachache kwa idadi.

  Mapema mwaka jana, Richmond ilitegeka. Ikaanzia kwenye Kamati ya Biashara iliyokuwa ikiongozwa na William Shelukindo na baadhi ya wajumbe wake akiwemo Dk. Mwakyembe, ikadaiwa baada ya miaka mingi kwamba ni muhimu sasa kuundwa kwa kamati teule ya bunge ya kuchunguza mkataba wa Richmond. Bunge lote likaridhia na hatimaye kamati ikateuliwa. Majina yakawa ni yale yale yaliyotarajiwa Kazi ikawa ni moja, kumtafuta mchawi wa Richmond.

  Napenda nieleweke wazi mapema kabisa kwamba, katu katika makala hii silengi kuwatetea mafisadi wa aina yoyote ile. Wasomaji wanaonifuatilia sana ni mashahidi. Nimetumia nguvu nyingi mno kupiga vita ufisadi wa aina yoyote.

  Kupitia kalamu hii nimetamka maneno mengi yenye kuhatarisha maisha yangu kiasi cha wasomaji wengi kunitumia ujumbe wa kuniuliza “Hivi Mwigamba huogopi?”. Na kwa kupigana vita dhidi ya mafisadi, mara kadhaa nimetishiwa kushtakiwa mahakamani, achilia mbali vitisho kutoka kule kwenye ‘jumba jeupe’. Nawakumbusha pia wasomaji kwamba nilishaapa kwamba hata kama kwa sababu yoyote ile nitaacha kuandika leo, bado nitaendelea kupigania haki ya mnyonge wa nchi hii.

  Lakini wakati nikiwa na msimamo mkali kiasi hicho dhidi ya mafisadi, nawatangazia pia vita watu wa aina yoyote ambao hujifanya kupigana vita dhidi ya ufisadi wakati wakiwa na ajenda yao ya siri ya maslahi binafsi.

  Hawa nao dhamiri ya moyo wangu inanituma kuwatangaza kwamba nao ni mafisadi. Yaani wanazo sababu binafsi za kuchukiana na fulani na kwa kweli wakipata fursa ya kum-‘fix’ wanamfix kweli kweli lakini huku wakitangaza kwamba ni kwa maslahi ya taifa.

  Huu pia ni ufisadi na ni ufisadi mbaya kuliko. Bora ule ufisadi wa moja kwa moja maana ni rahisi kuugundua na kuushughulikia kuliko huu wa kuvaa ngozi ya kondoo kumbe ndani mbwa mwitu.

  Baada ya dokezo hilo, naomba turejee kwenye mada yenyewe hasa. Kama wewe ni mtunza kumbukumbu mzuri, utakumbuka kwamba bunge jipya lilipoapishwa tu, Spika Sitta aliongoza jopo la wabunge wenzake kadhaa kudai nyongeza ya kile ambacho wao hukiita ‘posho’ za wabunge na kuziepusha na kodi ya serikali wakati kimsingi ni kubwa mara elfu ya mishahara ya watumishi wengi wa serikali na sekta binafsi ambao hulipia kodi mishahara yao.

  Hatimaye sakata hilo likaisha kwa Sitta kukosana na baadhi ya wanahabari kwa kurusha hewani pilikapilika zao za kudai nyongeza ya mafao hata kabla hawajaanza kazi. Hii ni sehemu ya sura halisi ya Sitta anayedai kupigana vita dhidi ya ufisadi.
  Lakini pia wenye kumbukumbu watakumbua kwamba Richmond (ile kampuni feki ya kufua umeme wa dharura), iliingia mkataba na serikali mapema mwaka 2006. Na baadaye ikaonekana dhahiri kwamba ile kampuni ilikuwa imetuliza Watanzania kwa ajili ya ufisadi wa baadhi ya watendaji wa serikali.

  Kulikuwa na maneno ya chini chini ya kuihusisha kampuni hiyo na aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo. Na maneno hayo yakapata nguvu mara tu baada ya mvua kunyesha na mabwawa yakajaa, akakimbilia kuwatangazia wananchi kwamba achaneni na Richmond maana hatuna shida tena na umeme wake huku akijua kabisa kwamba Richmond ilikuwa inakula pesa ya wavuja jasho wa nchi hii ipatayo milioni 152 kwa siku tena bila kuzalisha umeme.

  Kukapigwa kelele kila kona ya nchi Watanzania tukidai mkataba wa kampuni hiyo ujadiliwe bungeni au sivyo, iundwe kamati teule ya bunge kuchunguza mkataba huo. Kila mkutano wa bunge ukifika ripoti ya Richmond ikawa hailetwi na badala yake Spika Sitta akawa wa kupiga tarehe ya kujadili Richmond bungeni kila kukicha na hatimaye ikatulia na ikawa imetoka!.

  Ajabu kubwa ikaja kutokea mara baada ya sakata la Reginald Mengi na Malima ambalo baadaye liligeuka sura na kuwa la Sitta na Malima. Yakawepo maneno kwamba Malima hayuko peke yake katika kumvaa Sitta. Kukawa na maneno mengi tu kwamba nyuma ya Malima kuna mtu mkubwa anayetaka kumtumia Malima na mbunge fulani wa CCM aliyezoea kulipua mabomu ili kumng’oa Sitta kwenye uspika.

  Wenye akili kulingana na mazingira yaliyokuwepo, tayari waliweza kugundua kwamba mkubwa huyo ni nani. Ni baada tu ya Sitta kulimaliza sakata lake na Malima kwa staili ambayo haijawahi kutokea katika bunge la Tanzania, ndipo kwa mshangao kamati ya Shelukindo ikaibuka na taarifa kwamba Richmond imeliibia taifa na kudai bunge liunde kamati teule (miaka zaidi ya miwili baada ya Watanzania kuidai hiyo kamati teule).

  Na kwa sababu spika anapewa mamlaka na kanuni za bunge akawateua wale wale (tunaweza kuwaita watu wake) kuunda kamati hiyo. Kwa baadhi yetu tulishajua matokeo ya kamati teule hata kabla ya ripoti yake kwamba itakwenda na kigogo. Na hata gazeti moja la kila wiki likaandika mapema kile kitakachotokea. Na ndicho kilichotokea.

  Ni gazeti hilo hilo ambalo liliwahi kuandika makala ndefu iliyotokana na mahojiano yake na Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) ambapo ilielezwa kwamba kulikuwa na ugomvi wa chinichini lakini mkubwa kati ya Spika Sitta na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

  Na kikubwa ilikuwa ni kugombea kumrithi Kikwete mwaka 2015. Ni gazeti hilo hilo pia lililowahi kuandika makala nyingine ambayo haikuwahi kukanushwa na Sitta mwenyewe wala mtu mwingine (nakala zote hizo ninazo) ikidaiwa kwamba Sitta alikuwa ameahidiwa nafasi ya waziri mkuu wakati wa kampeni lakini baada tu ya ushindi wa mtandao wa ‘kimbunga’ kama walivyopenda kuuita, Sitta aliitwa na kigogo mmoja na kutakiwa ajaze fomu ya kuomba uspika.

  Ingawa walibishana kidogo na kigogo huyo, hatimaye alisalimu amri na kuchukua fomu ambapo alishinda. Ikiwa yote haya tuliyoelezwa ni ya kweli, basi tunaweza kufanya muhtasari wa ugomvi kati ya Sitta na Lowassa kama ifuatavyo:

  Kwanza kugombea uwaziri mkuu wa awamu ya nne chini ya Kikwete, pili kitendo cha Sitta kuunda kamati ya kubadilisha kanuni za bunge ambazo zilikuwa zinambana zaidi waziri mkuu kwa kuwekewa kipindi cha kuhojiwa ‘live’ na wabunge bila kujiandaa kwanza. Tatu, kitendo cha Malima kudaiwa kutaka kutumiwa kumng’oa Sitta (nasisitiza kama ni kweli maana haikuwahi kuthibitishwa), Nne kitendo cha Sitta kuunda kamati teule ya ‘wafuasi wake’ kummaliza Lowassa kupitia Richmond.
  Ni baada ya ugomvi huu wa mwisho unaohusu Richmond ndipo sasa akina Sitta wakatangaza rasmi kuwa wapigana vita dhidi ya ufisadi na wakaamua kwa makusudi kuwanyang’anya vita hiyo waanzilishi wake akina Dk. Slaa na kujifanya wao ndio wapiganaji dhidi ya ufisadi. Ni hicho ninachokipinga kwa nguvu zote.

  Kwa kuainisha hivyo historia ya Spika wetu, napenda kusema kwa dhati kabisa ndani ya moyo wangu na nitakuwa tayari kabisa spika na watu wake wanipeleke mahakamani lakini kwa dhati nasema Sitta, Mwakyembe, Shelukindo, Kilango, Selelii, Sendeka, na wenzao wote, si wapiganaji wa vita dhidi ya ufisadi bali ni wapiganaji vita dhidi ya Lowassa na wenzake.

  Hakuna vita dhidi ya ufisadi huku akiongoza wabunge kumzomea na kumbeza Dk. Slaa bungeni eti kwa sababu tu kasema ni vema posho zao za siku zipunguzwe ili wafanyakazi wanyonge kama polisi, waalimu, madaktari na waaguzi, na watumishi wengineo wa umma waongezewe mishahara. Haiwezekani akawa mpiganaji wa vita dhidi ya ufisadi huyo.

  Na napenda niseme wazi kwamba, naamini kwa dhati wote tukiwachambua mmoja baada ya mwingine kuanzia kwa Mwakyembe, Kilango, Selelii, Sendeka, na wenzao wote wanaojidai kupigana vita dhidi ya mafisadi kila mmoja wao atakutwa tu na sababu binafsi ya kulichukia kundi la akina Lowassa.

  Hakuna hata mmoja anayeweza kunidanganya eti kweli anaumwa na hali duni za wananchi. Walikuwa wapi siku zote. Na ukweli wa maneno yangu unaweza kuthibitishwa kama leo watu hawa hawa watapewa vyeo serikalini. Sitta awe waziri mkuu, Mwakyembe awe waziri wa Nishati na Madini, na wenzao wote hao wapewe uwaziri. Mtawasikia kama kweli watakumbuka vita dhidi ya ufisadi.

  Nasema, ni vema Watanzania tukatambua ukweli. Ukweli kwamba hakuna hata mmoja anayewapigania wananchi ndani ya CCM. Nimemnukuu mbunge wa CCM katika makala yangu ya juma lililopita aliyesema kwamba ndani ya serikali ya CCM ni Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein peke yake ndiye mwadilifu. Wengine wote wameshaathiriwa na ufisadi.

  Wanaojifanya kupiga vita ufisadi, wanasukumwa na sababu binafsi tena mara nyingi za ugomvi na wenzao. Sikutarajia Lazaro Nyarandu aliyekuwa akifoka bungeni juu ya ufisadi unaomaliza raslimali za taifa kwa sauti hiyo hiyo anamfokea Dk. Slaa kwenye kipindi cha moja ya kituo kimoja cha televisheni hapa nchini kisa kuomba mafao ya wakubwa yaangaliwe upya ili watu wa chini nao wafaidi.

  Nasema sura halisi ya ‘group’ hili la Sitta linalojifanya kupigana na ufisadi ndiyo hii. Hawana lolote isipokuwa maslahi binafsi. Suluhisho ni kuwang’oa wote, mafisadi wa hadharani (wale tuliowabamba katika kashfa za EPA, Richmond, n.k) na hata wale mafisadi waliojificha (wanaojidai kupigana vita dhidi ya ufisadi kumbe wana ajenda yao binafsi).

  Naamini mmenielewa!
   
 2. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  thanks very much for your info lakini unahiaji kupitia baadhi ya hansard ili tuweze kwenda pamoja na maelezo yako.lisemwalo lipo kama halipo .......
   
 3. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Hatujakuelewa, kwani hakuna hata mtu mmoja katika dunia hii asiefanya jambo lolote bila ya kuwa na maslahi. Kwani hata ukifanya jambo, kwa kuwa tu ni muadilifu, basi uadilifu ndio maslahi yako. Hapa kuna vita, au uko na sisi, au haupo na sisi. Kama Sitta & Co wana maslahi yao binafsi, that's up to them at least 4 now. Tunachotaka kuona ni kwamba hawa mafisadi wanabanwa kwa sana. Na wala siwi mbaguzi kwa kusema wahindi mafisadi mnaiua nchi. Maana katika mabao yote wanayoyapiga, wanatoa asilimia isiozidi kumi tu hapa nchini, iliobaki yote wanapeleka nje. Katika hiyo kumi ndio mgao kwa viongozi wetu, pamoja na mtu kama wewe, ambae unachukua muda wako kutengeneza hoja ya kuwatetea, hata kama utalikataa hilo. Mungu atasaidia haya mapambano, hata kama msipolipa sasa hivi, basi watoto au wajukuu wenu watalipa. Wakati huo hawa magabacholi fisadi (sio wahindi wote ni mafisadi), watakuwa tayari wako Canada, Uk au USA, wakila kuku kwa mrija!!
   
 4. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Watanzania tuna matatizo makubwa sana na aambayo sijui kama tutatayamaliza Yesu akirudi !!!!! n Kama mtu mzima na akili zake anaweza kutumia muda mwingi namna hiyo akiandika pumba za kuwasifu Wanaoteketeza nchi!!! Yet akajiita Mtanzania, na wakati huo utamkuta analalamika hali mbaya ya maendeleo ya Taifa, na huku akisifu maendeleo ya nchi za Wazungu, Bila kujua kwamba nchi zimeendelea baada ya uadilifu katika ngazi zote za serikali na washiriki wao!!!.i BASI MTU KAMA HUYU IS BETTER THAN Mr. ZERO. Na adhabu yake ataipata kwa Mungu, na Mungu siku hizi anatoa Adhabu hapa hapa Duniani. Nakuhakikishia kama kweli unatetea FISADI huku ukijua ni kweli ni Fisadi, na kwa kuwa tu amekupa chochote basi subiri utakuja jua nini nimesema leo. Ubarikiwe sana
   
 5. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Gembe, tathmini yako inavutia sana tu.

  Ninavyojua mimi ni kwamba jitihada zozote zinazofanywa na binadamu yeyote ni lazima zizingatie maslahi yake binafsi kwanza kabla hazijaangalia maslahi ya wengine. Ni pale mtu anapoona hatari kwa ustawi wake 9binafsi) ndipo anapoanza mapambano. Mara nyingine mapambano anayoanzisha huwa na manufaa kwa wengine pia na kadiri uwigo wa manufaa unavyopanuka ndipo manufaa hayo huweza kuwa yenye maslahi kwa Taifa.

  Mimi ninachotamani si mchakato wa jitihada (kama ulivyouelezea hapo juu) bali matokeo yatakayokuwa na masilahi kwa wengi. Kama mafahari wakipambana, na hatimaye wanyonge/masikini wakafaidika kihalali, nadhani tutakuwa tumepata tunachokitaka.

  Si rahisi hata mara moja akawepo binadamu ambae atajitoa muhanga bila kujua atafaidikaje na kujitoa kwake. Na faida ni lazima iwe kubwa zaidi kwake kuliko kwa wengine ili aweze kuchukua hatua ya kujitolea namna hiyo. Kila kitu kina gharama zake.

  Vita dhidi ya ufisadi ni ngumu sana. Kupambana na mtu (fisadi) anaeamini kuwa amepewa mamlaka ya kufuja rasilimali za nchi kwa kuwa alitumia fungu kubwa la mali zake kupata nafasi hiyo, ni jambo la hatari lakini ni lazima lifanyike. Yeyote atakaeweza kuongoza mapambano hayo, ni wakuunga mkono kwa nguvu zote.

  Wanasiasa duniani kote hupambana kufikia malengo yao kisiasa kwa nguvu nyingi. Haishangazi kusikia kuwa wapo wanaopambana ndani ya CCM kama ulivyoainisha hapo juu. Na hata hao wakimaliza muda wao, watakuja wengine watakaopambana vile vile.
   
 6. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  UKO SAWA MZEE
  Umeeleweka, katika Tanzania hii mtetetezi wa kweli wa wananchi ni Dk SLAA PEKE YAKE sio Mwakembe wala Mengi Fisadi Nyangumi

  nimekuelewa uko sawa kabisa
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  May 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Unamaanisha mwigamba ndio gembe ??
   
 8. r

  robinsv New Member

  #8
  May 8, 2009
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si amini kama kweli hapa duniani kuna mtu ambaye ni safi asilimia mia. tunachoakiwa watanzania ni kuwa makini kwa kila maamuzi tunayofanya hasa wakati wa kupiga kura kuchagua viongozi wetu la sivyo tutaendelea kuumia tuu.
   
 9. I

  Inkosikazi Member

  #9
  May 8, 2009
  Joined: May 5, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tunarudi pale pale kwamba mapambano yanayofanyika bila ya kuwa na itikadi iliyo wazi ina hatari ya kueneza na kuendeleza yale yale ambayo yanapigwa vita na baadhi ya washiriki wa mapambano yenyewe.
  Kwa nini Sitta na SSG yake hawaweki wazi itikadi yao mbele ya umma ili tujue kwamba kama wakiingia madarakani watatupeleka wapi kwenye ubepari mpevu au kwenye ujamaa mkongwe? Wote wanaona haya kusema hivyo kwa sababu hawana jipya wanalotaka kulileta kwa umma isipokuwa kukalia kiti na kutumbua kwa kwenda mbele...
   
 10. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kwa usemi wake Mwenyewe Spika Sita - ni siasa ya maji taka. Pamoja na wote kuogelea kwenye maji taka, wapo wanaowanyooshea wenzao vidole kuwa ni wachafu. Yanikumbusha mchezo wa watoto kwenye dimbwi la tope, huishia kugombana eti nani mchafu zaidi. Marehemu baba yangu aliwahi kunikanya kuhusu kuwalaumu rafiki zangu kwa uhuni wakati huo huo tunacheza pamoja, tunatembea pamoja na tunashirikiana kwa mambo mengi tu. Alisema, "Mwanangu huwezi kukaukia mtoni, lazima usogee kando".
   
 11. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Akina SSG ndiyo wale Hayati Mwl Nyerere alisema wanajidai wanapigania haki za wananchi (wako against mafisadi) lakini ukiwatazama unasema huyu nae yuko against mafisadi???????!!!!.... Yaani hawafanani kabisa, nia yao ni kwamba kwakuwa wako tofauti na mtandao wakina EL then watahakikisha wanawapinga! Lakini nia yao haina tofauti na ya akina EL et al katika kuwanyonya na kuwaibia wananchi wasio na hatia...
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wewe si unaona hapa wameandika SLaa peke yake ndio msafi na hana hata chembe ya ufisadi ,yaani ni shujaa kabisa.Lakini sikushangai maana una posti moja hujafahamu kuwa hapa tupo ukanda wa Gaza.
   
 13. I

  Inkosikazi Member

  #13
  May 9, 2009
  Joined: May 5, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bila ya kuwabana wote kwa umoja wao na katika makundi yao ipo hatari watu hawa nikiwa na maana ya wale wote wanaosikika zaidi katika siasa za TZ wakatupelekesha na hatimaye tukajikuta tunacheza mduara ngoma isiyokuwa na staili yoyote ili mradi unazunguka na kutingisha kiungo chako chochote.
  Vita ya kugombea viti vya kuzunguka, vita ya kugombea saluti, vita ya kugombea kupepeza bendera, vita ya kugombea magari makubwa, vita ya kugombea posho na marupurupu zaidi hata kabla ya kustaafu, vita ya kugombea kuitwa mheshimiwa..... hiyo ndiyo vita ambayo inaendeshwa si na wale ambao hawapo madarakani na wanataka kuingia la hasha, bali ni vita inayopiganwa na wale walioonja madaraka lakini wanahisi kwamba hayawatoshi na kwamba wanastahili madaraka zaidi.... yaani akina Sitta na Mwakyembe. Tusiwape nafasi hawa kwa sababu ajenda yao haotofautiani na ya wanaotaka kujinenepesha. Wanaolazimisha ukubwa ni hatari kushinda wale tuliowapatia uongozi kwa kuamini kwamba watatutumikia na baadae ikawa sivyo. Tujisahihishe na tujihadhari.
   
 14. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Lakini spika aliwekwa pale na ROSTAM na ile kazi haipendi kama kitu gani...si hivyo tuu na mkewe wakampa kazi nzuri tuu la kula malioni ya walalahoi lakini wapi...yeye alitaka uwaziri mkuu na mpaka leo he wants to settle some scores

  [​IMG]

  And who can forget how ROSTAM saved Mengi from public humiliation kwenye ile sakata la MENGI vs MALIMA

  kama mnabisha someni HANSARD za ile kamati ndio mtajua kuwa MENGI pamoja na matusi yote ambayo leo anamporomoshea ROSTAM lakini ukweli ni kuwa R.A alimsevu sana maana ile ingekuwa public hearing then sasa hivi hii mijadala ya MENGI vs everyone isingekwepo
   
 15. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapana wamekosea walioandika ni Slaa peke yake. watu wasafi ni wawili tu; Lipumba na Maalim seif
   
 16. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ama ni Kwa invinsible au moderators; huu utaratibu wa kuweka kila page kianzilishi cha thread unachosha kupindukia hasa kikiwa ni kirefu kama ilivyo kwenye thread hii. Ushauri wa bure kabisaaaaa, kama nia ni kuonyesha thread ilikoanzia inawezekana kabisa kuweka mistari michache halafu inayobaki ikawekwa kwenye link ili kila atakaye kuoa mwanzo anakong'oli tu hiyo link kuliko kuweka habari ndefu kila ukurasa.
   
 17. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Taarifa hiyo ni sahihi kabisa Tatizo hapa ni uwaziri mkuu. Mwalimu alieza kuwa ukimuona mtu amng'ang'ania kwenda ikulu kuna lake jambo.Kwa EL limedhihiri Sasa kwa mzee SS huko kwenye Tanzania Investment center sijui alifanya nini.Tatizo Bongo wababaishaji wako wengi sana sasa sijui nai tumuamini
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  May 9, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Game Theory,
  Mkuu wangu Mengi ni mfanyabiashara tu hana uhusiano wowote kiutawala na issue za CCM zaidi ya kuwa mwanachama..
  Matukio kama yake yako kila siku, sema ya watu wadogo kama sisi huwezi kuyasikia lakini kila siku ya Mungu tunapigwa virungu na viongozi waliobeba madaraka wakitumia cheo kama mtaji wa nguvu zao na sii dhamana waliyopewa na wananchi. Huyo Malima ni mmoja wao..

  Msongoru,
  Mkuu shukran kwa kuiweka historia hii vizuri na ikumbukwe na wengi maanake najua sana haitachukua muda watu tutasahau kabisa makubwa yaliyopita tukidai sii ndwele...
   
 19. Mussolin5

  Mussolin5 JF-Expert Member

  #19
  Nov 7, 2016
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 16,943
  Likes Received: 60,411
  Trophy Points: 280
  Apumzike kwa amani mzee sitta
   
 20. Jambazi

  Jambazi JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2016
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 14,445
  Likes Received: 12,628
  Trophy Points: 280
  Hatari sana
   
Loading...