Jamani hapa kuna mapenzi kweli?

huyo mwanamke unampenda na amejua unampenda, fyn si vibaya kumpenda mwanamke unaetaka kujabkuishi nae, swala linakuja hapo eti yeye bado hajapanga kuishi na mwanaume sasahivi, so anafurahia kuzini tu..
.
.
sasa umemchezea vipi sasa, maana wewe unataka usimchezee lakni yeye anakomaa mbaki kuchezeana..
.
.
huyo kuna kitu anakuficha, kama sio anamtu mwingine sijui, inawezekana kuna mtu anampenda ila hana uwezo wa kumhudumia,
.
.
akutambulishe kwa wazazi wake, hataki bro weka ndimu mdomoni nyosha goti, achana na huyo mwanamke, anza mahusiano kisisiri siri na mwanamke mwingine, taratiibu anza kumpotezea, unaanza kuacha kumtafuta siku nzima, baadae siku mbili, baadae wiki baadae mwezi, akikuambia humtafuti mwambie sikuhiz kaz zimekuwa ngumu... then kaoe pengine, maisha haya ni mafupi kutapanya pesa kwa mtu asie na malengo
 
Sasa kinachonisikitisha ninapompa taarifa za kuvunja uhusiano analalamika na kunilaumu nimemchezea na kumpotezea mda. Wkt in reality yeye ndio naona anataka kunipotezea mda sasa...

Unadhani atafurahi!? Ni kawaida ya wanawake kulalamika, suala liko wazi hapo…..uanaume ni pamoja na maamuzi magumu ya kulinda territory na heshima yako.
 
huyo mwanamke unampenda na amejua unampenda, fyn si vibaya kumpenda mwanamke unaetaka kujabkuishi nae, swala linakuja hapo eti yeye bado hajapanga kuishi na mwanaume sasahivi, so anafurahia kuzini tu..
.
.
sasa umemchezea vipi sasa, maana wewe unataka usimchezee lakni yeye anakomaa mbaki kuchezeana..
.
.
huyo kuna kitu anakuficha, kama sio anamtu mwingine sijui, inawezekana kuna mtu anampenda ila hana uwezo wa kumhudumia,
.
.
akutambulishe kwa wazazi wake, hataki bro weka ndimu mdomoni nyosha goti, achana na huyo mwanamke, anza mahusiano kisisiri siri na mwanamke mwingine, taratiibu anza kumpotezea, unaanza kuacha kumtafuta siku nzima, baadae siku mbili, baadae wiki baadae mwezi, akikuambia humtafuti mwambie sikuhiz kaz zimekuwa ngumu... then kaoe pengine, maisha haya ni mafupi kutapanya pesa kwa mtu asie na malengo

Ushauri mzuri huu kwa wenye mioyo soft ushauri wa kufaa huu kwa jamaa,eti anasema manzi king’ang’anizi,anajitafutia sababu ya kuendelea nae.
 
Huyu mwanamke nilikutana nae miezi mitatu iliyopita nikiwa katika harakati zangu za kikazi mkoa flani. Alinivutia muonekano wake na tabia (napenda wanawake wapole). Tukaanza mahusiano baada ya wiki mbili za kufahamiana. Mkoa aliopo anaishi kwa ndugu.

Umri ana miaka 25. Anafanya kazi kiwanda cha wahindi. Hawamlipi vizuri kutokana na maelezo yake na kazi anafanya siku sita za wiki, masaa 12 kwa siku. Hua anapewa siku moja tu ya kupumzika. Kwahyo ili tuwe tunaonana inalazimika mimi ndio niwe nasafiri kila napopata nafasi kwa vile tunaishi mikoa tofauti ni umbali wa masaa matatu kati yetu.

Tatizo binti shida hazimkauki. Binti anaomba sana ela. Kuanzia pesa ya nauli ya kwenda na kurudi kazini. Vocha. Kula. Mahitaji yake yote lazima aombe kubustiwa. Nimepiga hesabu kwa wiki pesa ndogo akiomba ni elfu 80, hua haipungui hapo. Sasa hivi ameomba nimpangie chumba nimnunulie na furniture ili tuwe tunakutana kwa uhuru tofauti na hivi tunavyokutana lodge kila nikija.

Kwahiyo nilimkalisha chini. Mshahara wangu haujui lakini ni zaidi ya mara tisa ya ule anaopokea yeye. Nikampa wazo anipe utaratibu nikajitambulishe kwao wanijue. Then aje tuishi wote huku tukitafta project iwe ya biashara au chochote ambacho ataweza kufanya akiwa huu mkoa niliopo mimi kuliko kuendelea kufanya kazi ambayo haimlipi huku akizidi kuniingizia unnecessary costs. Mipango ya ndoa then iendelee.

Amegoma katakata. Anadai kwa sasa kuishi na mwanaume ni mapema mno. Anataka kua independent awe na chumba chake, afanye kazi zake na maisha mengine. Nimemuambia kama haiwezekani basi kila mtu aendelee na maisha yake kuliko kupotezeana mda. Analia. Analalamika nimemchezea. Eti simpendi na simjali na nimebadilika! Binafsi nimeshindwa kumuelewa!
Piga chini CCM huyo na matozo yake, yeye anaomba kwa wiki si chini ya elfu 80 ×4= 320,000 inamaana unampa pesa zaidi ya mshahara wake, sasa hapo si bora umuweke ndani, na anataka umpangie chumba na umnunulie vitu ? Wanawake baadhi wajinga sana kwanini asiwaambie wazazi wake wamfanyie hivyo vitu au kaka zake, huyo mwanamke ana jiuza na hakupendi, lakini ndiyo Dada zetu awa na wana wapata misukule ya kuwafanyia mahitaji kama hayo aliyokuomba.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom