Jamaa yangu - Yaki

Jamaa yangu - Yaki

Joined
Nov 8, 2018
Posts
28
Reaction score
29
JAMAA YANGU

Msanii: YAKI
Producer: Amba

Intro

Yoh Amba it's Yaki again
Babi this song special dedicate to ma best friend

---
Verse I

Tumeishi kama ndugu moja wa kuzaliwa/
We kushoto mi kulia mtaani walitushuhudia/
Unapoonewa lazima ntaingilia/
Ndivyo ilivyokuwa na kwa upande wako pia/

Ulinipa moyo na maneno mazuri/
Mziki sio Bagamoyo ila tu nikaze msuli/
Nimwombe Mungu nisiache kusali/
Ipo siku tutawapiku tu wanaoendesha magari/

Rafiki wa kweli maisha yangu uliyajari/
Ulisema niwe makini kuna ugonjwa hatari/
Nimweshimu demu wangu/
Ukasema yuleyule ndiye nije kufunga naye pingu/

Ukasisitiza kamwe nisije kumwacha/
Siku ntakayomwacha na ushikaji wetu umekwisha/
Love na Peace mchizi wa uhakika/
Kwa mdomo hadi maandishi mtaani ulikubalika/

Haukuwa mbishi kama ilivyo sasa/
Na unavyoshinda na nguo mbichi unaonekana kama kibaka/
Ulikuwa smart bonge la mtanashati/
Leo upo Vagrant yote sababu ya Brant/

Hauna noma nao hauko safi kama Fashi*/
Wakijitahidi kukuokoa halafu wewe ukawacrash/
Ukawaona wabaya kumbe unajisariti/
Kutwa nzima wewe na kaya ushauri wao hautaki/

Haulali nyumbani ukionekana usiku tu unachungulia uwani/
Mwana umenipa mtihani/
Kwenu wanajua upo kwetu kwetu haupo hawaniamini/
Nafanya jitihada kondoo urudi kundini/

Ajabu maskani kwenu wote wananishutumu mimi/
Wanasema mimi ndiye niliyokudatisha/
Wanasema mimi ndiye ninayekupotosha/
Nimekutorosha hadi unalala kwa mapusha/
Mnaviwasha tu vya Arusha/

---

Kiitikio

(Jamaangu) Yes
(Jamaangu) Ungeniskiliza yote yasingetokea

(Jamaangu) Yes
(Jamaangu) Ona nimekaa kimya kilichokuja kutokea

(Jamaangu) Yes
(Jamaangu) Ungeniskiliza yote yasingekuja kutokea

(Jamaangu) Yes
(Jamaangu) Ona nimekaa kimya kilichokuja kutokea

---

Verse II

Mtaani story ndio hizo mwana umepatwa na Nini/
Watakaoambiwa chanzo baadhi yao hawaamini/
Maana hata demu wako ananiuliza umeanza lini/
Eti ile kitu hautumii labda umekumbwa na jini/

Unakumbuka shule ulianza kama masikhara/
Day Moja nilikuotea class na pakti ya sigara/
Ukajitetea kuwa unafanya biashara/
Leo umesha lose brain kila kitu kwako ni hasara/

Umesha change life umeshakuwa dhaifu/
Unafunga mk jwi kiunoni bonge la knife/
Unajichora tattoo majina yake za watu/
Mchana kwako usiku usije kugeuzwa ndafu/

Umekuwa wa ma bif chuki na kila mtu/
Linanihuzunisha nikikumbuka maisha ya shule ndio yanasikitisha/
Hesabu sio sana ila Geography ulikuwa kichwa/
Na ukaniahidi siku Moja hata ndege utakuja kuirusha/

Umepoteza future ndege tena hutorushusha/
Kichwani imejaa moshi hata baiskeli tu unaangusha/
Mama analia mwanae anaumwa hakuna wa kumsaidia/
Mi nia yangu ni nzuri ila tu hamjanishtukia/

Maana tayari watu flani walishasema nakuharibia/
Kwa nguvu napinga mi nakujali mwanangu na nakupenda/
Si unaona niko peke angu hata demu wako amekutenga/
Amekuona kenge akiulizwa anadai hakufahamu hata chembe/

Ila mwana usikonde/
Ingawa home utata wanajadili wapi uende/
Wengine kwa Mganga wengine Milembe/
Wengine labda Kakobe aje home aombe/

UTAPONA USIKONDE

---

Kiitikio

(Jamaangu uuuh wewe wewee jamaangu) Yes
(Jamaangu wewe wewe) Ungeniskiliza yote yasingetokea

(Jamaangu) Yes
(Wewe wewee) Ona nimekaa kimya kilichokuja kutokea

(Jamaangu) Yes
(Wewe wewee) Ungenis
1788811236504.jpg
kiliza yote yasingetokea

(Jamaangu) Yes
(Wewe wewe) Ona nimekaa kimya kilichokuja kutokea

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
 
Back
Top Bottom