KakaJambazi
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 18,724
- 12,086
Umnunulie dawa "ya mswaki" afu mwambie awe anatumia.Habari!
Ni mshkaji niliefahamiana nae mwaka jana na tuna miezi kama tisa kwenye urafiki, ila mdomo wake unatoa harufu mbaya tukiwa katika katika mazungumzo. Sijajua shida ni hapigi mswaki vizuri, huwa hapigi mswaki kabisa au anapiga kwa matukio.
Hii hali nilikuwa najitahid kuivumilia kwa kumkwepe kwepa akinielekezea mdomo lakini leo katika story za hapa na pale kuhusu mwenendo wa UEFA naona harufu imekuwa kali zaidi ikabid nipunguze stor ili maongezi yasiwe mengi sana.
Hali kama hizi huwa mnapambana nazo vipi? Maana naona aibu kumwambia ila natamani sana awe na kinywa kisicho na harufu, isitoshe sisi bado ni vijana kabisa.
Naomba Ushauri wenu wakuu.
Natanguliza shukrani.