Jamaa akaanza kuchonga kuhusu msosi..!

Jamaa akaanza kuchonga kuhusu msosi..!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
DSC00438.JPG

Ilikuwa ni ndani ya Daladala....

Jana majira ya asubuhi nilipanda daladala kutoka Gongo la Mboto kuelekea Posta kibaruani kwangu. Wanaonijua wanaweza kujiuliza imekuwaje nimelala Gongo la Mboto badala ya nyumbani kwangu. Msije nitoa roho bure, wala sikulala kwa nyumba ndogo, bali nilikuwa nimelala matanga kwenye msiba wa baba wa rafiki yangu, hata mama Ngina anajua. Nilipata siti, hasa ukizingatia kwamba, ilikuwa ni asubuhi na usafiri katika viunga hivyo ni wa kugombea kutokana na uwingi wa wakaazi wa maeneo hayo ukilinganisha na idadi ya daladala.

Sikumbuki hasa ilikuwa ni kwenye kituo gani, bali ilikuwa ni katikati ya safari. Awali nilidhani ni mzaha, lakini kadiri mambo yalivyokuwa yakienda, nilijua kwamba, haukuwa mzaha. Ni kwamba jamaa mmoja mwanaume ambaye alikuwa amekaa kiti kimoja kutoka kile cha nyuma alikuwa akiongea kwa simu. Kuongea na simu haikuwa tatizo, wala jambo la ajabu, lakini alichokuwa akiongea labda kilikuwa. Ni kwamba jamaa huyu alikuwa akibwata, badala ya kuongea. Kwanza alikuwa akiongea kwa kelele sana na pia alikuwa akiongea mambo ambayo naweza kusema kuwa ni ya ajabu na kukera pia. Inaonekana huyo mtu aliyekuwa akimwongelea alikuwa amemkera sana.

‘Nani alimwambia aje, kwani tulimwita. Wewe mtu anakomba mboga kiasi kile nani atakubali . Mtu anajua kabisa usawa wenyewe ulivyo lakini anakula kama yuko kijijini, mimi alinikera sana.'

Halafu aliendelea bila kujali. ‘Unajua nini? Niliona tangu mwanzo kabisa wakati msosi unawekwa, nikajua hapa kuna shughuli. Nasikia ndivyo alivyo. Wanasema, hata kule kwa uncle alifukuzwa kwa sababu ya kula. Mimi aliniudhi sana.'

Halafu aliendelea… ‘Kuna yule mdogo wake, naye hivyohivyo. Kuna siku aliniabisha kweli ukweni, Kipalang'anda. Tulienda kuwaona tukapewa msosi. Nakwambia, tonge-nyama ile mbaya, hadi mkwe wetu akaguna. Nadhani kwenye familia yao wana tatizo la kula kiaina……'

Halafu ilionekana kama vile mada ya kula ilikuwa imeisha. Ghafla ikazuka mada nyingine.

‘Hapana, sikumpa, naona alichukua mwenyewe. Ukiweka nguo tu lazima atazivaa. Kuna ile chupi yangu ya Boxer ya bluu, ile nilinunua siku ile wakati tunapita mtaa wa Narung'ombe Kariakoo, basi hiyo hiyo……'

Abiria walianza kuvutiwa na sauti ya abiria huyo ambaye kwa huku mjini tunasema alikuwa ameulamba, yaani kavaa vizuri.

‘Basi siku hiyo naitafuta niivae siioni. Usiku naona mtu kaitinga. Kwa kweli sikumsemesha, niliamua kumziria. Hebu fikiria, mtu atachukua vipi chupi ya mwanaume mwenzake…..!'

Huyu abiria alikuwa anaonekana kabisa kwamba, amejisahau kupita kiasi.

‘Dawa yake ni moja tu, ni kumwambia kwamba hapa mjini hana nafasi. Hivi ushawahi kuliona likimega matonge, yaani dizaini ya kijijinijijini kabisa. Kwa kweli kuna siku nilikuja na mheshimiwa wetu yule……, aliniangusha sana. Wewe mtu unakula, mamchuzi yanadondokea hadi kwenye viwiko na kila mahali, ndiyo nini. Nilicheka siku ile ya msiba wa …(Anataja jina ), aisee aliadhirika kweli. Kaingia kwa wapishi kaibuka na finyango. Kumbe ya moto bwana, ile anaitia mdomoni, kutoka anakutana na msafara wa kusindikiza maiti, ikabidi aiteme mbele ya watu…'

Halafu alitulia kidogo, ilionekana kama huyo mwenzake alikuwa kizungumza.

‘Ni kweli kama mtu anaweza kumega mitonge kama ile ni kwa nini ashindwe kujitegemea. Kajitu kadogo hata mkononi hakajai, lakini kanakula kama vile kametoka Dafur….'

Abiria waliangua kicheko mle ndani ya daladala baada ya jamaa kutoa kauli ile. Abiria yule alishtuka na kutazama pande zote akakutana na macho ya abiria wote wakimwangalia. Jamaa alishtuka sana, na inaonekana wazi kwamba alikuwa amejisahau. Alizima simu hapo hapo na basi lilipofika kituo kilichofuata alishuka huku uso wake ukiwa umesawajika kwa aibu kubwa. Sina uhakika kama alikuwa mefika mwisho wa safari yake maana alishukia pale njia panda ya Jet…………..
 
Naomba nichangie baadaye bro Mtambuzi ...manake kwa sasa NIMECHEKA hadi nimepaliwa....lol
Ama kweli the 'world' is 'universe' ...hasa pale tonge-nyama!!!
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahaha...kaka Mtambuzi huishi visa wewe!!!!

duh, ila mjini bajeti kali jamani...lol!


SIDE NOTE: Rejea maongezi yetu ya simu yenye kumb. na. AIRTEL/078/1902HRS y
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaahahaaaa! huyo mgeni wake atakuwa ametokea '' KANDA YA ZIWA" maana wanakata tonge moja kubwaaaaaaaa! halafu wanaligawa mara tatu , "konda, dereva na utingo" la kwanza linamezwa bila kutafunwa, la pili linaenda na nyama na la tatu linamezwa bila kutafunwa. SASA hapo muweke ale na wadada wa hapa Dar wanaojifanya wanarembua wakati wa kula akijakugeuka sahani nyeupeeeeeeeeeeeee!!!!!! .
 
Miaka fulani ya nyuma huko Mbeya, kulikua na muungwana fulani anaitwa DAMDA....Huyo bwana yeye zake ilikua ni misiba tu. Ukiacha majonzi na vilio, misiba ya Mbeya huambatana na misosi bandika bandua, ni utamaduni uliojengeka kwa kila familia iendayo msibani kupeleka chakula ama kimepikwa au vinginevyo.
Sasa huyo bwana DAMDA kazi yake kubwa ilikua ni kupitia kwenye misiba kwa shughuli maalumu tu, ya "kupeleka Pwani". Huyo mtu alikua anakula sahani zisizo na idadi, kama mnafahamu masinia fulani hivi yenye michoro ya maua ya Tausi, basi huyo muungwana alikua anafuta sinia zima.

R.I.P DAMDA a.k.a "Nisile bha'mama" - Nimekuja kina mama.
 
Hahahahaahahaaaa! huyo mgeni wake atakuwa ametokea '' KANDA YA ZIWA" maana wanakata tonge moja kubwaaaaaaaa! halafu wanaligawa mara tatu , "konda, dereva na utingo" la kwanza linamezwa bila kutafunwa, la pili linaenda na nyama na la tatu linamezwa bila kutafunwa. SASA hapo muweke ale na wadada wa hapa Dar wanaojifanya wanarembua wakati wa kula akijakugeuka sahani nyeupeeeeeeeeeeeee!!!!!! .

Mgeni msukuma sio?lo where is Kongosho ?????/
 
Last edited by a moderator:
http://www.google.co.tz/url?sa=t&rc...degMCbtpeLrGACJoRgjwQ&bvm=bv.1355534169,d.d2k

Msinisemee ah 4x
Kwamba anapenda kula
Msinishangae 4x
kwamba anapenda kula
Msinitengee 4x
Kwamba anapenda kula
VERSE(1)
Asi hivi juzi juzi
Kulikuwa na shuguli
Utawa birika na simali
Kulikuwa na pilau na wali
Basi nami nikajiunga
Pale pale kupiga mvunga
Watu wakajipanga
Nikaanza kwa tonge na nyama
Jamani ninamatonge*4
Mpaka wakanifukuza
Nikasema sijali
Nikatoa pesa mfukoni
Nikanunua mayai
Nilijofuata watu wa wakai
CHORUS
Msinisemee ah 4x
Kwamba anapenda kula
Msinishangae 4x
kwamba anapenda kula
Msinitengee 4x
Kwamba anapenda kula
VERSE (2)
Ilikuwa juma pili
Siku ya watu wenye ufahali
Kujirusha sehemu mbali mbali
Nami nikasema sikubali
Wacha niendee*4
Ila pesa sina natadani kali
Nikapita sokoni
Nikaomba embe sokoni
Nikaelekea baharini
Nikawaona wengi ufukweni
Hakika na embe jiutani
Nakula ili watamani
Mate yalwaijaa mdomoni
Wakaanza kuniomba
Msinisemee ah 4x
Kwamba anapenda kula
Msinishangae 4x
kwamba anapenda kula
Msinitengee 4x
Kwamba anapenda kula
 
Khaaaaaaaaaaaaaaaaaah! sikutegemea kama The Boss utanichonganisha na Kongosho, mm nimesema KANDA YA ZIWA zijataja kabila, Hahahahaahahaha! Loh!

Hahahah unalo leo....
 
Mtambuzi rocks, yani kuna mshikaji wangu kanichekesha mida ya lunch, then nikawa nasoma hii stori kwenye mchina wangu nikajikuta machozi yananitoka tu kwa kicheko.... thumbs up mwalimu Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaahahaaaa! huyo mgeni wake atakuwa ametokea '' KANDA YA ZIWA" maana wanakata tonge moja kubwaaaaaaaa! halafu wanaligawa mara tatu , "konda, dereva na utingo"la kwanza linamezwa bila kutafunwa, la pili linaenda na nyama na la tatu linamezwa bila kutafunwa. SASA hapo muweke ale na wadada wa hapa Dar wanaojifanya wanarembua wakati wa kula akijakugeuka sahani nyeupeeeeeeeeeeeee!!!!!! .

Lisa Lisa Lisa...... hebu tutake radhi watu wa kanda ya Ziwa.... Umechekesha kweli hapo kwenye red yaan nimecheka kwa sauti!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Lisa Lisa Lisa...... hebu tutake radhi watu wa kanda ya Ziwa.... Umechekesha kweli hapo kwenye red yaan nimecheka kwa sauti!!!!!

Hahahaahahaaaaaaaaaaaa! hiyo dada yangu niliiona LIVE ! nikabaki nashangaa kuja kuangalia sahani nikakuta nyeupeeeee! Hapo ndipo nilipo zidi kushangaa kuwa chakula kimeenda wapi, nisianze kulalamika nimenyimwa chakula, nikashushuliwa na Mama kuwa nakula kwa kulemba acha nionyeshwe jinsi ya kula, ilibidi niwe mpole.
 
Back
Top Bottom