Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,696
- 19,137
Habari zenu .
Tafuta maisha bora taratibu na Kwa heshima,jasho halali linalika na linaleta furaha kuliko rundo la mapesa ya dhulma.
Hata ukiwapa masikini mafungu ya Mali za dhulma bado haiondoi ukweli kwamba hutaishi Kwa amani.
Siku nyingi sana,tuliwahi piga dili ,naam dili tukiwa watu watano., but lile dili Kwanza lilikuwa haramu, halafu pili Sisi wawili tuliwazunguka wenzetu watatu tukapiga pasu ule mshiko ,na tukatoa vitisho kwamba hakuna wakutufanya chochote.
Ni kweli wale wanaume hakuna aliyehoji zaidi ya kunung'unikia moyoni.
Ila huwezi amini Ile pesa ndogo ilinielemea,yaani tofauti na zamani ilikuwa nikienda sehemu ya starehe watu hawaniombi pombe kama zamani.
Nilijaribu kujitolea ninunue geti la kanisa ,padri naye akasema subiri niongee na wanakamati maana Daniel ushatoa sana.
Haikuwa rahisi kuelewa ni jinsi gani naelemewa.
Hakuna aliyenipigia kuonesha ananiazima hata buku mbili kila mtu alikuwa kama kanishtukia.
Mtu pekee aliyekuja kwangu nimuazime pesa alikuwa Yule niliyegawana naye mgao wa dili na aliniomba kiasi cha robo tatu ya pesa tuliyogawana.
Hata baada ya kumuuliza Kwani yeye pesa amepeleka wapi alinambia pesa kazi yake matumizi na katumia zimeisha.sikumpa kwasababu ninazozijua .
Kwa kumalizia kila mradi niliouanzisha kupitia zile pesa ulisimama na sidhani kama nitaendelea.
Ishi vizuri ,siku za mwanadamu kuishi Duniani ni chache mno .tusidhulumiane