Jamaa akaanza kuchonga kuhusu msosi..!

Jamaa akaanza kuchonga kuhusu msosi..!

I+m+watching+you_b2923a_3701467.jpg

I am watching YOU................!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mtambuzi na we unatuonea bure, umezidi kutoa thread za kuvuta watu hadi thread zako zimekua makutano ya member humu, shauriyako
 
Hakuna mtu asopenda kula jamani...sema sisi watu wa ziwa hatunaga kulemba..tonge linajengewa hadi chumba...lol

me nna mfano wa pande zile kwenye masamaki basi we utakula samaki ugali upo palepale , ukipewa utajiri wa msosi raha sana huna presha,mtambuzi we are bak, muondoe huyo mwenye cha moto and relax
 
Ila nadhani watu wengi wa mjini wanadhani kuishi mjini ni kujinyima kula..na kwamba anayekula ugali mwingi basi mshamba..sasa wewe kipato kidogo utajiachiaje??...nimewaona wenye hela zao na wako mjini wanakula sana..and most of them wanakula mtaani wakija home wanafanya kubrush tu...ukiwafuatisha mwenzangu na mie ulieshinda home...unabaki vifupa tu..when comes to eating myself i don't give a shit!

me nna mfano wa pande zile kwenye masamaki basi we utakula samaki ugali upo palepale , ukipewa utajiri wa msosi raha sana huna presha,mtambuzi we are bak, muondoe huyo mwenye cha moto and relax
 
mbontafo clemeeee huku jamvini porojo sana usiniogope Mentor nakuja huko nipokeeeeeeee sikukuu hiiii .mimi bwana nilisikia madereva hapa ofisini wakiadithia wanavyofanyiwa kila mmaja alikiri hilo hapo ndio raha yao ilipo nisamehe lol hata mimi nilishangaa.

tsicha kapisa monomae..iyo ofisi kama sio ya kupigania haki za mashoga sijui!??? (unisameheee..)

Pili, imagine mi siendi kuhesabiwa..hii itakuwa mara ya pili in a row...uniwakilishe vyema! wafika adi kijiji gani nkutume salamu!??
 
Ila nadhani watu wengi wa mjini wanadhani kuishi mjini ni kujinyima kula..na kwamba anayekula ugali mwingi basi mshamba..sasa wewe kipato kidogo utajiachiaje??...nimewaona wenye hela zao na wako mjini wanakula sana..and most of them wanakula mtaani wakija home wanafanya kubrush tu...ukiwafuatisha mwenzangu na mie ulieshinda home...unabaki vifupa tu..when comes to eating myself i don't give a shit!

hahaha kumbe wanawarubuni wanaobaki home, sasa maisha ya kuigiza hadi lini, wajiachie bana kama kipo, unajua tunajitafutia matatizo ya vidonda kwa kuamini kula sana ni ushamba,
hafu mtambuzi we unaona huyo anayekula ndio mshamba me naona huyo anajifanya ye wa mjini then bado hajui kuongea na cmu in public place ndio mshamba asiyejijua
 
naishia pale hai bomang'ombe
 
Daaaaah!Angalau leo nimecheka!Tonge nyama!Tonge nyama,daaaah!
 
Ila nadhani watu wengi wa mjini wanadhani kuishi mjini ni kujinyima kula..na kwamba anayekula ugali mwingi basi mshamba..sasa wewe kipato kidogo utajiachiaje??...nimewaona wenye hela zao na wako mjini wanakula sana..and most of them wanakula mtaani wakija home wanafanya kubrush tu...ukiwafuatisha mwenzangu na mie ulieshinda home...unabaki vifupa tu..when comes to eating myself i don't give a shit!

Mimi pale kwa mama ntilie ninapokulaga huwa nikifika anajua ninavyokula.Lazima aweke ugali mkubwa wa udaga na samaki mkubwa au mboga yoyote.Na ugali ukiisha na mboga imebaki nanyanyua bakuli na kuunywa mchuza halafu lazima nilambe vidole.Sisi waafrika bana!!
 
ryooo nilikua nataka kuanzisha thread ya kutafuta mke wa kimachame...sasa sijui niahirishe tuingie pm au unasemaje!??

mimi sio mmachame ndugu yangu NAONA UNATAKA KUWA TAJIRI GHAFLA Mentor
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ni yupi kwenye hiyo picha?
DSC00438.JPG

Ilikuwa ni ndani ya Daladala....

Jana majira ya asubuhi nilipanda daladala kutoka Gongo la Mboto kuelekea Posta kibaruani kwangu. Wanaonijua wanaweza kujiuliza imekuwaje nimelala Gongo la Mboto badala ya nyumbani kwangu. Msije nitoa roho bure, wala sikulala kwa nyumba ndogo, bali nilikuwa nimelala matanga kwenye msiba wa baba wa rafiki yangu, hata mama Ngina anajua. Nilipata siti, hasa ukizingatia kwamba, ilikuwa ni asubuhi na usafiri katika viunga hivyo ni wa kugombea kutokana na uwingi wa wakaazi wa maeneo hayo ukilinganisha na idadi ya daladala.

Sikumbuki hasa ilikuwa ni kwenye kituo gani, bali ilikuwa ni katikati ya safari. Awali nilidhani ni mzaha, lakini kadiri mambo yalivyokuwa yakienda, nilijua kwamba, haukuwa mzaha. Ni kwamba jamaa mmoja mwanaume ambaye alikuwa amekaa kiti kimoja kutoka kile cha nyuma alikuwa akiongea kwa simu. Kuongea na simu haikuwa tatizo, wala jambo la ajabu, lakini alichokuwa akiongea labda kilikuwa. Ni kwamba jamaa huyu alikuwa akibwata, badala ya kuongea. Kwanza alikuwa akiongea kwa kelele sana na pia alikuwa akiongea mambo ambayo naweza kusema kuwa ni ya ajabu na kukera pia. Inaonekana huyo mtu aliyekuwa akimwongelea alikuwa amemkera sana.

‘Nani alimwambia aje, kwani tulimwita. Wewe mtu anakomba mboga kiasi kile nani atakubali . Mtu anajua kabisa usawa wenyewe ulivyo lakini anakula kama yuko kijijini, mimi alinikera sana.’

Halafu aliendelea bila kujali. ‘Unajua nini? Niliona tangu mwanzo kabisa wakati msosi unawekwa, nikajua hapa kuna shughuli. Nasikia ndivyo alivyo. Wanasema, hata kule kwa uncle alifukuzwa kwa sababu ya kula. Mimi aliniudhi sana.’

Halafu aliendelea… ‘Kuna yule mdogo wake, naye hivyohivyo. Kuna siku aliniabisha kweli ukweni, Kipalang’anda. Tulienda kuwaona tukapewa msosi. Nakwambia, tonge-nyama ile mbaya, hadi mkwe wetu akaguna. Nadhani kwenye familia yao wana tatizo la kula kiaina……’

Halafu ilionekana kama vile mada ya kula ilikuwa imeisha. Ghafla ikazuka mada nyingine.

‘Hapana, sikumpa, naona alichukua mwenyewe. Ukiweka nguo tu lazima atazivaa. Kuna ile chupi yangu ya Boxer ya bluu, ile nilinunua siku ile wakati tunapita mtaa wa Narung’ombe Kariakoo, basi hiyo hiyo……’

Abiria walianza kuvutiwa na sauti ya abiria huyo ambaye kwa huku mjini tunasema alikuwa ameulamba, yaani kavaa vizuri.

‘Basi siku hiyo naitafuta niivae siioni. Usiku naona mtu kaitinga. Kwa kweli sikumsemesha, niliamua kumziria. Hebu fikiria, mtu atachukua vipi chupi ya mwanaume mwenzake…..!’

Huyu abiria alikuwa anaonekana kabisa kwamba, amejisahau kupita kiasi.

‘Dawa yake ni moja tu, ni kumwambia kwamba hapa mjini hana nafasi. Hivi ushawahi kuliona likimega matonge, yaani dizaini ya kijijinijijini kabisa. Kwa kweli kuna siku nilikuja na mheshimiwa wetu yule……, aliniangusha sana. Wewe mtu unakula, mamchuzi yanadondokea hadi kwenye viwiko na kila mahali, ndiyo nini. Nilicheka siku ile ya msiba wa …(Anataja jina ), aisee aliadhirika kweli. Kaingia kwa wapishi kaibuka na finyango. Kumbe ya moto bwana, ile anaitia mdomoni, kutoka anakutana na msafara wa kusindikiza maiti, ikabidi aiteme mbele ya watu…’

Halafu alitulia kidogo, ilionekana kama huyo mwenzake alikuwa kizungumza.

‘Ni kweli kama mtu anaweza kumega mitonge kama ile ni kwa nini ashindwe kujitegemea. Kajitu kadogo hata mkononi hakajai, lakini kanakula kama vile kametoka Dafur….’

Abiria waliangua kicheko mle ndani ya daladala baada ya jamaa kutoa kauli ile. Abiria yule alishtuka na kutazama pande zote akakutana na macho ya abiria wote wakimwangalia. Jamaa alishtuka sana, na inaonekana wazi kwamba alikuwa amejisahau. Alizima simu hapo hapo na basi lilipofika kituo kilichofuata alishuka huku uso wake ukiwa umesawajika kwa aibu kubwa. Sina uhakika kama alikuwa mefika mwisho wa safari yake maana alishukia pale njia panda ya Jet…………..
 
hahaha kumbe wanawarubuni wanaobaki home, sasa maisha ya kuigiza hadi lini, wajiachie bana kama kipo, unajua tunajitafutia matatizo ya vidonda kwa kuamini kula sana ni ushamba,
hafu mtambuzi we unaona huyo anayekula ndio mshamba me naona huyo anajifanya ye wa mjini then bado hajui kuongea na cmu in public place ndio mshamba asiyejijua
Suprise, mie sija comment kuhusu Bwana Misosi, bali nimesimulia tu yale yaliyojiri...........
 
Last edited by a moderator:
kuna jamaa mmoja nilisoma nae O-level alikuwa na uwezo wa kula mpaka akawa maarufu shule nzima....ilifika kipindi akabatizwa jina la chatu kwa uwezo wake wa kumeza bila kutafuna....sikuwahi kujua jina lake halisi.
 
Hahaha...lol, Mtambuzi u remind me of mshikaji mmoja pande za chuo wakati ule,akiwasimulia kitu mtakusanyika kama kuna mkutano vile! :laugh:
 
Back
Top Bottom