Jamaa abaka hadharani

Makoba

Member
May 25, 2009
10
7
Jamaa anayetajwa kuwa ni mwanajeshi (mstaafu au bado anafanya kazi) amembaka mwanamke hadharani eneo la Magomeni Makanya (Dar es Salaam) mchana huu kwenye mida ya saa 6.

Kwa simulizi ya shuhuda aliyekuwepo kwenye eneo la tukio, ambaye pia anamfahamu huyo mjeshi mpaka nyumbani kwake kasema kuwa jamaa kakutana na huyo mwanamke karibu na gereji bubu ya barabarani makanya, mara akamshika kwa nguvu huyo mwanamke na kumvua kwa nguvu hadhari na kumtenda hicho kitendo cha aibu mbele ya macho ya watu wengi waliokuwa wakipita hapo. Mpaka anamaliza kitendo hicho, kulikuwa na watu wengi waliofurika hapo wakiwa wameduwaa. Kwa nini hawakumpiga? Ni jamaa wanayemfahamu (kwamba ni mjeshi, pia ni mbabe), na anaishi maeneo ya karibu (Mwananyamala Kisiwani-ambapo si mbali na gereji hiyo).

Shuhuda mmoja aliyetaka kumtetea huyo dada alijikuta akionja hasira ya huyo mjeshi. Jamaa kamvunjia vioo vya gari yake kwa hasira; kisha akasogea karibu kucheza mchezo wa pool.

Muda mfupi; walifika askari polisi na difenda yao-wakiwa na bunduki zao. Huenda walipigiwa simu na wananchi. Polisi hao wameshindwa kumkamata mjeshi huyo; ambaye walikuwa wanamuona na yeye wala hakuwakimbia.

Binafsi nimefika eneo hilo la tukio takriban nusu saa baada ya tukio na kuukuta huo umati wa watu, polisi wakiwepo na difenda lao. Kama vile haitoshi, mjeshi huyo kawazonga polisi na kuwaambia kuwa hawana UBAVU wa kumkamata wala nini. Ndiyo hayo yaliyotokea muda mfupi uliopita.

Kwa vyombo vya usalama na vyombo vya habari:
Ukiweza kufika hapo Magomeni Makanya utapata mkanda mzima. Watu walioshuhudia ni wengi na wanaelezea wenyewe; na wanamfahamu huyo mjeda. Binafsi baada ya kuona polisi walishajulishwa na wamekwishafika; nilifanya jitihada za kupigia simu vyombo viwili vya habari na kuwaelekeza eneo la tukio. What a shame!

Namba yangu ni 0764600170.
 
Mh tumefika huko?
Haya mabo ni makubwa, atakuwa kabaka sana na ni tabia yake.

Sasa mbona hatari na gonjwa hili la ukimwi!
 
yani watu hawakujichukulia sheria mkononi? kwa nini? yani wanamuogopa kwa sababu ni mwanajeshi au? :A S angry:
 
Really? What a disgrace...............ina maana mjeshi yuko juu ya sheria? au let me rephrase that ina maana watu wote wa Magomeni makanya ni macoward kiasi gani?
 
Hana 'Mania' huyo mJeshi?...kutokana na hiyo stori nadhani huyo mJeshi anaweza akawa na ugonjwa wa akili aina ya 'Bipolar Disorder'..especially Mania, ndio huwa wana tabia za ajabu ajabu kama hizo.
 
Hana 'Mania' huyo mJeshi?...kutokana na hiyo stori nadhani huyo mJeshi anaweza akawa na ugonjwa wa akili aina ya 'Bipolar Disorder'..especially Mania, ndio huwa wana tabia za ajabu ajabu kama hizo.

ur rit he is sick!
 
That can not be. Kweli watu watazame mtu akifanya ujahili wa namna hiyo?
Hata mi napata taabu kuamini... hivi mtu unawezaje kuwa na nguvu za kiume za kujamiiana mbele ya kadamnasi? Kundi kubwa la watu linawezaje kushindwa kumdhibiti mtu mmoja-hata awe mbabe vipi? Askari na silaha zao nao wanashindwa kumkamata, kivipi? Ni ngumu sana kuamini
 
Yaani sijapata kusikia mijitu mdebwedo kama mijitu ya makanya!yaani hawakumtendea haki huyo ndada ina maana walikuwepo pale wakiangalia porno live?wantia kichefu chefu ,ingekuwa huku ile kukamatwa tu ni bahati yake maana angechinjwa na nyumba yake ingechomwa moto!
 
Mkuu Makoba!

Kwa kuthibitisha ebu leta picha mkuu hata kama ni Cm ya mchina!
 
Duh!

Hii haitoi mshangao kwa huyo mtendaji, bali kwa sisi jamii nzima. Kweli tunaweza kuona tukio la kinyanyasaji namna hiyo na tukaacha tu kwa vile ni mwanajeshi?

Haiingii akilini hata kidogo
 
Hata mi napata taabu kuamini... hivi mtu unawezaje kuwa na nguvu za kiume za kujamiiana mbele ya kadamnasi? Kundi kubwa la watu linawezaje kushindwa kumdhibiti mtu mmoja-hata awe mbabe vipi? Askari na silaha zao nao wanashindwa kumkamata, kivipi? Ni ngumu sana kuamini
Mimi mwenyewe najiuliza, hivi ina maana hata mawe hayakuwepo? Unawezaje kushuhudia ukatili wa aina hii halafu ukanyamaza kimya? Na huyo mama alikuwa anapiga kelele au ilikuwaje? Mmh, ni vizuri kufuatilia, unaweza kukuta ni mkeo ndiyo amebakwa, na kwa hali hiyo kama jamaa ni mgonjwa, basi ni kuandika tu maumivu.
 
Haiwezekani umati wakusanyike kushuhudia tu jambo la kinyama namna hiyo. Kama ni kweli basi hao watazamaji watakuwa na matatizo makubwa zaidi ya akili.
Mkuu, kama ni kweli hiyo sasa ni laana! Biblia inatufundisha kwamba nchi kama imelaaniwa mojawapo ya dalili ni hizi; utatiwa woga hata ukiona unyasi utafikiri nyoka utatoka mbio! Mkeo atachukuliwa machoni kwako hutii neno! Kondoo wako atachinjwa machoni pako utachekelea tu! Utajenga wewe wataishi wenzio!
 
tumefika pabaya sana! sasa condom alivaa saa ngapi? au ni mwendo wa kujilipua tu?
 
Back
Top Bottom