Los santos
JF-Expert Member
- Jan 14, 2021
- 1,190
- 2,657
Mike Ilishebo (44) mwanaume wa nchini Zambia amedaiwa kumuua mke wake huyo kwa kutumia waya wa umeme pia kumchoma visu tumboni kisha na yeye kujiua kwa kunywa sumu chanzo kikidaiwa ni mgogoro wa ndoa wa muda mrefu baina yao.
Tukio limetokea huko Lusaka tarehe 3 April hii 2024, baada ya polisi kutaarifiwa na mmoja wa majirani kwa jina la Alice, polisi walipofika eneo la tukio walimkuta mke kashafariki karibu na kitanda na mume amekutwa sebuleni kashafariki akiwa anatoka vitu vyeusi mdomoni.
Mume alikuwa anafanya kazi bank, wanandoa hao wameacha mtoto wa miezi 8.
Baada ya tukio hilo la kushtusha wanaowajua wameibuka kuomboleza mtandaoni kwa kujawa na simanzi.