Jamaa anashangaza sana aisee, miaka 10 kauchuna kimya huku Watanzania tukipiga kelele za kutosha hili la Watanzania kulipa kwa dollar katika mambo mbali mbali nchini. Nakumbuka hapa kulikuwa na mjadala mzito kuhusu issue hii na magazeti mengi nchini yaliandika kwa kina, lakini akaendelea kuuchuna tu. Kabakisha miezi mitatu ndiyo anatoa kauli kama hii tena baada ya kuulizwa swali akiwa India. Hakustahili kabisa huyu kuwa kiongozi wa nchi yetu kaiacha katika hali mbaya sana kuliko alivyoikuta. Bado anaendelea na safari yake ya kuaga nchi za nje, pamoja kujua nchi haina pesa na safari zake zinaongeza deni la Taifa wala hajali anatanua tu.