Jakaya Kiketwe Kazi imemshinda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jakaya Kiketwe Kazi imemshinda!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mstahiki, May 7, 2008.

 1. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mh Rais aiahidi kazi Milioni je zikowapi?
  Ameshindwa kuwawajibisha Lowassa,Chenge,Karamagi na waiofanya uozo wotee.
  Hatoi maelezo yoyote kuhusu hali mbaya ya uchumi..
  Kila siku yupo safarini haonekani kujali kabisa matizo ya wananchi....

  Mh Rais unataka KUPENDWA na watu unaowagandamiza na kuona wanazulumiwa kila siku...USIPO BADILIKA cha MOTO UTAKIONA
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  vitisho vya namna hii havina msingi na vinaweza kutafsiriwa vibaya. Hatuko hapa kumtishia Rais wa nchi kuwa "cha moto" atakiona wakati kichwa cha habari kinasema "kazi imemshinda".
   
 3. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi simtishi ila nnaueleza kwamba asipobalisha muenlekeo ADHABU YA MUNGU ataiona..NiMungu yule anaowatetea Wanyango ndio anamuwajibisha ipasavyo.
   
 4. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii ni kweli kabisa MKJ
  lakini inawezekana vitisho hivi visivyo na msingi vinakuja kutokana na jazba, baada ya kuona kuwa Mh. hana anachofanya kazi ni kuzunguka tu
  Poleni vijana, tutafute njia ya kufanya maana hali ni mbaya na watu wana jazba vibaya sana
   
 5. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hali ni hatari sana,mkapa huyu....
   
 6. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mstahiki nasikia bado anaplan, nafikiri akimaliza plan yake tutaona kama ameshindwa kabisa au la.

  Siku moja mwanzoni alisha sema wabunge ni watu wazima wameelewa.

  Sasa tunafikiri na yeye ni mtu mzima ameisha sikia kilio cha wananchi 80% waliompa kura. Tunafikiri kuzungtuka kwake labda si bure anajipanga.

  Matatizo yaliyopo nchini sasa yanajulikana hata kwa watoto wa nasale school.

  KItakuwa kitu cha ajabu kama yeye mwenye uwezo wa kuwa RAIS ya nchi kama atashindwa kutambua hili.

  TUnahitaji MAFISADI wafikishwe pale panapo stahili.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimesikia watu wengi wakifanya udhalimu wa hali ya juu kwa "jina la Mungu". Huyu Mungu anatumiwa na watu wengine hata wanasikia sauti kuwa Mungu kawatuma kufanya jambo hili au lile.

  Hofu yangu naogopa JF kuonekana kama sehemu inayoruhusu, kulea na kuchochea mawazo ya matumizi ya nguvu dhidi ya serikali halali. Haya maneno "adhabu ya Mungu" yasipotafsiriwa yanaweza kuwa ni "code message" ya vitendo viovu na vyenye madhara kwa watu.

  Jazba peke yake ikiruhusiwa kutawala akili ya mtu inaweza kumfanya mtu afanye vitendo vibaya. Tunawaona watu walio na jazba wanavyowatia watu mafuta na kuwachoma moto na wanavyowapatia kibano wezi wa karanga!

  JF is more than that, tunaongozwa na akili na siyo hisia na vionjo (labda wachache wetu). Kama Kikwete ameshindwa, basi tumia nafasi uliyo nayo au shirikia katika mapambano haya ya fikra ili kuhakikisha aidha:

  a. Anakuwa impeached (which is the regular way of removing a president who is in office)
  b. Hakikisha hachaguliwi tena kugombea 2010.

  Nje ya njia hizo mbili nina hofu unaweza kuwa unapendekeza njia nyingine ambayo ni nje ya njia za sheria.

  Hili ni angalizo tu ili nijue kama tuko kwenye ukurasa mmoja au mwenzetu kutokana na jazba unaweza kuwa kwenye ukurasa mwingine kabisa.
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,637
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Kamanda jaribu kutembelea bongo mara kwa mara, kama hiyo inashindikana basi jaribu kujikumbusha namna ya kuandika kiswahili vizuri katika forums mbalimbali katika mtandao,blogs n.k

  Hapa JF kuna kona ya lugha ya kiswahili, si vibaya ukawa unapita pita huko ili kupiga brashi kiswahili chako..

  Huu ni ushauri tu ..Kamanda
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kibunango, labda jazba imemzidia..
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,637
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Inawezekana...Na hasa katika kipindi hiki JK yupo katika kila mdomo wa mwananchi ni kazi kweli kweli... Unaweza kupata jazba na mbaya zaidi kupandisha mori.

  Tatizo ni pale jabza inapotulia na unapoangalia ulisema nini/kuandika nini....
   
 11. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kibunango

  Nafikiri mstahiki amekosea ktk neno la mwisho. Lisemalo "cha mto utakiona".

  Hilo neno ni kubwa mno na lina maana nyingi sana siyo vizuri kulitumia hata siku moja maneno yanayolenga katika vitisho.

  Mstahiki anatakiwa tu aeleze hicho cha moto kina maana gani na abadilishe na kuweka neno sahihi.
   
 12. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kibunango

  Nafikiri mstahiki amekosea ktk neno la mwisho. Lisemalo "cha mto utakiona".

  Hilo neno ni kubwa mno na lina maana nyingi sana siyo vizuri kulitumia hata siku moja maneno yanayolenga katika vitisho.

  Mstahiki anatakiwa tu aeleze hicho cha moto kina maana gani na abadilishe na kuweka neno sahihi.
  Mimi simtishi ila nnaueleza kwamba asipobalisha muenlekeo ADHABU YA MUNGU ataiona..NiMungu yule anaowatetea Wanyango ndio anamuwajibisha ipasavyo.
   
 13. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2008
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,006
  Likes Received: 2,223
  Trophy Points: 280
  YEYE HATAKIONA CHA MOTO KWA VILE TAYARI ALICHOKITAKA KWA KUTUPUMBAZA WATZ AMESHAKIPATA. ALAIAHIDI MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, YAKO WAPI!!!!! ARI MPYA, KASI MPYA ZIKO WAPI!!! KINACHONIPA FARAJA MWANA WA NCHI HII NI KWAMBA ITAKUWA NI FARAJA KUU HATA WAFU WATATUSAIDIA KUSHANGILIA KWANI NAONA USHINDI MKUU WA WAPENDA MAENDELEO NA WATZ WENYE MAPENZI MEMA NA NCHI HII KAMA ATAENDELEA HIVI TUHESABU CHAMA CHA MAJAMBAZI HAKINA LAO 2010. TUJIPANGE WAPENDA HAKI WA NCHI HII, USHINDI UKO WAZI. TUSIMUAMSHE ALIELALA, ATAKUJA KUOMBA TUMPUNGUZIE MAFUTA ILI NAYE AMLAKI BWANA HARUSI. WE ARE ABOUT TO WIN GUYS!!!
   
 14. M

  Mutu JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Kasomeka vizuri tu ,ilaanatakiwa awe makini na maandishi nadhani ilikuwa ni typo tu.Hata hiyo hapa watu wana chapia sana kingereza lakini wana eleweka na hawaambiwi chochote.Wewe umeacha kuchangia alichosema umesahiha kiswahili wakati hiyo ungeweka kama NB.

  Kuhusu alichosema ni sawa hatujaona ahadi zake rais ingawa ukweli ni kwamba mimi sikutegemea mabadiliko sasa ila nilijua leo itakuwa afadhali kuliko jana matokeo yake kila kukicha afadhali ya jana.

  mstahiki Amekuja kuharibu mwisho ndugu imeonyesha kuwa una plan mbaya vitisho vya kutumia nguvu ingawa umejaribu kueleza unachomaanisha kuwa "Mungu atamuhukumu" still don't use that kind of words next time you will not be in safe side.
   
 15. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mhh!!.... Kuku mgeni Bandani utamjua tu!!
   
 16. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #16
  May 8, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280

  ...mstahiki wakati tunalalama..mustafa mkullo jana anatetea utawala wa kikwete anasema uchumi unapaa..na pato la mtanzania limekuwa kufikia dola 525$ kutoka dola 300$ mwaka 2005....

  ..wakati yeeye anasema hayo ...mifukoni hatuna pesa...na bora mifukoni tungekosa pesa tukaona ujenzi wa miundombinu ukiendelea na kumalizika kwa kasi...hiyo yote hakuna ...sasa kama mkuloo anasema pato limeongezeka na atuambia pesa zinaenda wapi??
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,637
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Kamanda Mutu;
  Awali ya yote nilifikiri kuwa ni jazba lakini hebu soma tena hapa chini, kama alikosea hapo awali iweje tena akosee katika bandiko lake la pili. Msimamo wangu unabaki pale pale kuwa anahitaji kukisafisha kiswahili chake..

  Na huu ni ushauri tu, kwa faida yake binafsi na kwa wasomaji wa hapa JF kutopata shida ya kusoma mara mbilimbili ili kuelewa/kufahamu anazungumzia nini...

   
 18. M

  Mutu JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Kweli anatakiwa kuwa makini maana kukosea mfululizo sio mwake itabidi nikubaliane na wewe.Watu tunakosea ila sio kila post inamakosa itabidi afanye proof reading yeye mwenyewe kabla ya post.
   
 19. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #19
  May 12, 2008
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Umesema yote! Lakini pia labda ni njia yake ya kutoa maoni. Tuangalie anasema nini badala ya lugha anayotumia. Ila muhimu kuheshimu Urais kama huwezi mheshimu Rais!
   
 20. Nyama Hatari

  Nyama Hatari JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 221
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wacha mikwara yako wewe! Eti Kikwete "asipobadilisha mwelekeo Mungu atamuwajibisha ipasavyo". Wewe ni mwoga tu na mnafiki. Jee Mungu atawawawajibisha lini Rais Bush na mwenzake Blair waliolowa damu za watoto na wanawake wasiyo na hatia kule Irak na wanaoendeleza mauaji, unyama na uharibifu kila kukicha?
   
Loading...