mamaye Balali alindwa

lidoda

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
641
574
Mamaye Ballali alindwa
na Kulwa KarediaHALI ya ulinzi mkali imeimarishwa nyumbani kwa mama mzazi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) marehemu Daudi Ballali.

Habari za kuaminika zilizopatikana jana nyumbani kwa mama huyo Boko, Dar es Salaam, zinasema kuwa ulinzi huo umewekwa na serikali kupitia BoT tangu kutangazwa kwa kifo cha Ballali wiki iliyopita.

“Tumesikia ulinzi huu umewakwa na serikali kwa kushirikiana na BoT kwamba hakuna mtu yeyote kuingia hapa, tunashangaa sana kuona hata sisi ambao tumekuwa naye hapa tumebaki kuwa watazamaji tu,” alisema Seif Omar, mkazi wa Boko.

Alisema kitendo kilichofanywa na serikali si cha kiungwana, kutokana na ukweli kwamba msiba huwa hauchagui maskini au tajiri wa kwenda kuzika mwenzake au jirani yake.

Tanzania Daima jana ilipofika nyumbani kwa mama huyo anayeishi nyumba namba BNJ/BOKO/1081, ilishuhudia hali ya ulinzi mkali, kitendo kilichosababisha hata mwandishi wa habari hizi kuzuiwa kuingia ndani.

Baada ya kuwasili nyumbani, mmoja wa walinzi wa Kampuni ya Regimental Security aliyekuwa getini, alikataa katakata kufungua geti hilo kwa madai kuwa amepewa maelekezo kutoka ngazi za juu serikalini na BoT.

“Nikusaidie nini, unaitwa nani na una shida gani ndugu…tafadhali nionyeshe kibali chako cha kuingia humu ndani kutoka BoT, na kama huna, nakuomba uondoke eneo hili,” alisema mlinzi aliyekataa kutaja jina lake.

Alisema yeye amepewa maelekezo hayo na maofisa wa juu wa BoT, ambao hakuwa tayari kuwataja majina na kusisitiza kuwa anatekeleza majukumu yake ya kazi.

“Nashindwa jinsi ya kuwasaidia…jamani nawaomba sana muondoke hapa,” alisema mlinzi huyo na kuendelea kufunga geti hilo, kitendo kilichoashilia kuna shinikizo kutoka juu.

Juhudi za gazeti hili kumuona mama mzazi wa Ballali ziligonga mwamba kutokana na hali ya ulinzi iliyopo.

Wakati huo huo, baadhi ya wananchi waliohojiwa na Tanzania Daima kuhusiana na kauli ya serikali juu ya kifo cha Ballali wamesema serikali inapaswa kueleza ukweli baada ya kuuficha.

“Tumeshangazwa na kauli ya serikali, tunaelewa wazi kwamba Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, atakuwa ameelewa ukweli, sasa kwa nini atufiche?” alihoji Dickson Juma.

Alisema kama kifo hicho kisingekuwa cha siri, kwanini serikali ilipata kigugumizi kusema ukweli kuanzia ugonjwa wake hadi anafariki, jambo ambalo linazua maswali mengi.

“Sisi tunasema umefika wakati sasa wa kuelezwa ukweli na kama sivyo, basi iundwe tume haraka kabla ya mambo haya hajapoa, maana tunajua yakipoa, ndiyo yamekwisha,” alisema Juma.

Naye Mwanakombo Hussein alisema kitendo cha serikali kushindwa kushiriki katika mazishi ya Ballali kinaonyesha wazi kwamba kuna matabaka ndani ya viongozi wa serikali.

Aliwataka wananchi wote kuungana na kuishinikiza serikali ili kuhakikisha inaunda tume huru kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina na majibu yatolewe haraka.

Marehemu Ballali alifariki dunia Mei 16 jijini Washington, Marekani, alikokuwa akipata matibabu tangu mwaka jana, baada ya kufukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete, baada ya kuhusishwa na ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), ambako zaidi ya sh bilioni 133 zinadaiwa kupotea.
juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 21 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Kama serikali ilisema Balali sio mtumishi wa serikali iweje leo itumie pesa za kodi zetu kulinda nyumbani kwa mama yake Balali? serikali hii lakini ipo siku itakoma mwisho wake

na Emanuel - 27.05.08 @ 08:43 | #13507

Ufisadi mwingine huu bwana, hata mpaka ktk kumjulia hali mtu aliyefiwa na mtoto wake nako taabu? Hapa serikali inajizihirishia uhusika ktk kifo hiki.

Hapa wamewekwa walinzi wa kampuni binafsi ili baadaye ukija kuhoji watageuka na kusema ilikuwa ni suala la familia yao kumlinda mama yao.

na Ufunuo, Basra, Iraq, - 27.05.08 @ 08:48 | #13508

Jamani nikiwaambia hapa hakuna cha nini au laa!! Hivi ni hii serikali inatufanya sisi ni vilaza sana au wajue tumeamka haya na tuone huo ulizi utakuwepo mpk lini mwisho wa siku itakuwa je?

Inatisha jamani na inatia huruma makubwa haya yako km filamu tena filam ambayo wanaigiza ndoo kwanza wanajifunza uigizaji natusubiri

Nimechoka hata kusikiliza na kusoma habari za Daudi Balalli

na Herieth, TZ, - 27.05.08 @ 08:57 | #13509

Mbona serikali inazidi kujichanganya na kutuaminisha kwamna imehusika na kifo cha Balali? Kwanza mama Balali analindwa na BoT na serikali kwa wadhifa gani? maana hadi Balali anakufa alikuwa sio Gavana BoT? Mbona wakati Balali anaumwa huyo mama hukuwekea ulinzi kama ilivyo sasa? Tunataka kufahamu pesa hizi zinazotumika kumlinda mama Balali ambazo ni kodi yetu zinatumika kwa kigezo gani? Mbona wakati Ditto anafariki mama yake hakuwekewa ulinzi kama huu wa mama Balali? SERIKALI ISITUNDANGANYE HAPA KUNA KITU KINAFICHWA.

Wakati Balali anaumwa serikali ilituambia ni mtu huru ambaye ana haki ya kuishi sehemu yeyote. Sasa kwanini huo uhuru wasimpatie pia mama yake Balali ili ndugu, jamaa na majirani wawezi kufika kumfariji? Kwanini mpaka kibali cha kumuona mama Balali kitoke serikalini au BoT?

Pia tunataka kufahamu kabla Balali hajatimuliwa kuwa gavana wa BoT serikali ndiyo iliyompeleka Marekani kutibiwa. Je ni kiasi gani cha pesa ya kodi zetu kilitumika kugharamia matibabu yake? Je, hizo pesa zililipwa wapi, wakati serikali ilidai kwamba haijui hata hospitali aliyolazwa Balali?

Mafisadi wengine mjue, huu ndio mchezo wa MAFIA na wewe Chenge kama ulikula pesa hizo na wengine bora utuambie sasa maana MAFIA watakuua tu kabla hujafika mahakamani, ili kuficha ukweli. Chenge, the choice is yours, utuambie ukweli na ufe kama shujaa au ufiche ukweli na ufe kama mwovu/fisadi, Believe me your days are numbered soon you will be silinced take my words.

na Ron, TZ, - 27.05.08 @ 09:04 | #13514

Ditto hakuwa fisadi, hakuiba pesa zetu, alifanya kosa la kuua na kujiwasilisha penye vyombo vya sheria. Mchezo mbaya ulifanywa na wapambe, lakini kwa uhalisi wa Ditto, kitendo cha kuua kilimsumbua hadi kufa. Hii ya ulinzi ni kali, hivi kumbe BOT na serikali wana pesa nyingi kiasi hicho! Wanalinda nini?? Ni nani atamudhuru mama Balali, kikongwe cha watu! Kuweka ulinzi ni upuuzi, ni bora wangegharimia kurudisha mwili wa Balali ili bibi huyu amzike mwanawe.

na ros - 27.05.08 @ 09:37 | #13523

Mnaotoa maoni jiangalieni sana,mafisadi ni hatari kuliko hata bomu la nyuklia,wanaouwezo wa kumjua adui popote pale alipo hata kama yuko kaburini.
Kikwete,Rostma,Lowassa,Masha,Karamagi,Membe,Sitta, Rashid Othman,Cornel Apson,Chenge hawa ndo balaa,na ili nchi itulie inabidi hawa tuwaue mmoja baada ya mwingine ikibidi hata kwa nguvu za jadi maana kifedha hkuna awezae kupambana nao hata kidogo.

na kachuska, Tanzania, - 27.05.08 @ 09:41 | #13524

Kuna mtu mmoja aliniambia kuwa hata Benno Ndullu si mtu safi nikambishia,lakini sasa hata mimi napata wasiwasi kuwa inawezekana naye ni walewale!
kama anatumia hazina yetu kwenda kulinda kwa marehemu daudi balali eti hili tu waandishi wa habari/wananchi wasipate habari yeye naye ni fisadi!
muda unaweza kumfanya naye akaja kuwa kama huyu marehemu!

na benno ndullu naye vipi? - 27.05.08 @ 09:52 | #13526

Hayo maajabu sijawahi kusikia katika hisotira ya waafrika especially watanzania kuwa mtu akifiwa kuna kuwa na ulinzi wa aina huu au mpaka upate kibali ndio uruhusiwe kwenda kumpa mfiwa pole. Hata kifo cha baba wa Taifa hili watu tulikwenda bila kibali wala masharti yeyote iwje Balali yawe hivi.
Msitudanganye mtuaumbuka vibaya sana serikali ya CCM.

na gilda, Dsm, - 27.05.08 @ 10:06 | #13527

Unajua Mm nimefurahishwa sana na jinsi ndugu na jamaa na wa aliyefichwa katika visiwa vya malta Balali kwenda kwenye msiba na Card hii ndio inavyotakiwa kwa mtu mwenye hela kama waombolezaji wanakuja hawana vibali hakuna haja ya kuingia Big up Balali mmeonyesha njia hata wakina Chenge,Lowassa,Karamagi wafuate hii mbinu na huko kwa Baba Mola mtakuwa mpo viti vya mbele,walalahoi nao viti vyao Big Up BOT

na mkula, Namanga, - 27.05.08 @ 10:10 | #13528

Hata kama umezaliwa bila akili ya kutosha lakina hapa utashituka kidogo(1)Kwa nini sasa huyu mama alindwe ili iweje mbona wakati mwanae yuko serikalini alikuwa halindwi WATOWE SABABU (2)Kwenye msiba serikali haikuhusika sasa ndugu wanakuja kwa mama mzazi kwa maongezi ya msiba huu walinzi wanawakataza kuingia ndani na nyumba hii siyo yao na siyo kawaida ukienda kwa nduguyo lazima uwe na kibali..MBONA WENYEWE HAWANA..Je sasa watalinda hadi lini na kwa pesa toka mfuko upi.HAPA MNAZIDI KUANUA MAVITUUS.(3)HUYO ALIYETOA AMRI YA ULINZI HUU AKIBANWA ANAJUA SIRI YOOOOOOOOOOTE(sumu aliyopewa na nani alimtegeshea yote anayajua)HEBU MWANGALIENI KWANZA ANAVYOANGALIA CHINI CHINI nyumbani anapesa kibao za ufisadi.

na radi, Tanzania, - 27.05.08 @ 10:25 | #13533

Mmmmhhh sasa hii kali kwenda kuhani msimba mpaka upate kibali,inatisha sana.Thaadhari kwa MAFISADI na hicho CHAMA CHA MAFISADI(CCM).Iko siku mtakuja kulia na kusaga meno.Mungu ibariki TANZANIA.Amen

na Kutiki, Dar, - 27.05.08 @ 10:30 | #13535

CCM sasa ndo mnae,lekea kaburini.kikwete na wewe sasa umepoteza mwelekeo hivi hujui mpaka sasa haujafanya lolote la maana katika hii nchi zaidi ya kupeana michongo.najua swala sii ulinzi ila ni percent itakayotumika kuilipa kampuni ya ulinzi.hatutashangaa kusikia imetumika shilingi bilion moja kwa kuweka ulinzi.kwani wewe kiwete hutaki kula nadiriki kukuita kiwete na sipo tayari kukuita kiwete kwani wewe ni mlemavu wa kufikiri.na watanzania tunajuta kumkabidhi mlemavu kama wewe utuongoze.kimsingi tulidhani tunatoa nafasi kwa makundi maalumu yaani(special group)ili tuitambue michango yenu lakini tunaishia kujuta na skuzote majuto ni mjukuu.sasa subiri uchaguzi ujao ndo utajua njano na nyeupe.wewe sikupendi kutokana na utawala wako wa kifisadi kwanini umlinde mamawa balali wakati yeye ndo aliyetuzalia mafisadi au ndo kule kulindana

na richmand, tz-dodoma(UDOM), - 27.05.08 @ 10:36 | #13536

mmmm jamani miminashindwa kuamini kama huyu balalikweli amekufa siligani kati ya balali na silikali mbona watanzania tumewekwa njiapanda kifocha balali hebu tuambieni ukweli

na jonh, dsm , - 27.05.08 @ 10:50 | #13539

na jonh, dsm , - 27.05.08 @ 10:50 | #13540

na jonh, dsm , - 27.05.08 @ 10:50 | #13541

Mama Balali ni afadhali asisumbuliwe na watu wengi wa kumwongezea majonzi na hasa maneno ya uchochezi na ushirikina.
Sio vizuri bibi huyo kuambiwa mwanao hajafa, au kauawa na serikali, na umbeya mwingine. Ni rahisi kuathirika kisaikolojia. Ukweli anahitaji usalama tutake tusitake. Bibi mzee kusumbuliwa na watu kila siku kwa nini?

na Mnyalukolo - 27.05.08 @ 10:59 | #13543

kweli huu si uungwana hata kidogo yaani majirani tunashindwa kwenda kumpa pole mwenzetu, eti tupate kibali BOT. CCM, BOT, hapa mmekosea kuliko kuliko. Nchi gani sasa hii, ndiyo mmeshindwa kutawala kabisa, mjihuzuru sasa ili tupate viongozi ninyi wahuni, hampaswi kuongoza nchi.

na Jirani wa mama Balali, Boko, - 27.05.08 @ 11:02 | #13545

Watanzania tunapigwa changa la macho na Sirikali.lakini Dr slaa sisi watanzania tunaoichi marekani tunafanya kila jitihada kujuwa alilazwa Hospitali gani? au alikuwepo wapi yani state gani na nyumba gani? na tunawasiliana kila mtanzania kila state kutupa break news na tukijuwa hata hospitali basi jukumu litakuwa kwa vyama vya uchunguzi hapa marekani na kuchirikiana na utafiti wetu.kwahio tutajuwa mbichi na mbovu.kwani hili sio suala la Balali peke yake linahusu kila mtanzania na kwasuala lakifo kwanza leo Balali kecho mimi.kwahio tusilifumbie macho watanzania tujenge tanzania yenye kuheshimiana na ili tuondoe atui ufisadi nilazima walio fanya tuleni nao sahani moja?.bila hivyo tanzania tutakufakatika ufukara na kulea mabilionea wanayo ifukaricha nchi.

na jalome, massachusa boston u.s.a, - 27.05.08 @ 11:38 | #13556

Mnyalukolo #13545
Kwa namna moja nakuunga mkono,lakini usisahau kuwa Wahehe wana watani wa jadi,na wana nafasi yao katika shughuli kama hii,na huyu bibi anafahamu mambo yanavyokwenda!Sasa watani wa Mama Ballali tutapata wapi hiki kibali?
Mkapa kaongea mbona waandishi mpo kimya!
Nashuru pia kwa e-mails nilizozipata kuhusu suala la umoja wa wanaume Tanzania!

na gonga, safarini kwenda maswa, - 27.05.08 @ 11:53 | #13558

HIVI WEWE KIKWETE HAYA YOTE UNAYOYAFANYA NA RAFIKI ZAKO KONA LOWASA HAMJUI NANYI KUNA SIKU MUNGU ATAWAITA KWENYE KITI CHA HUKUMU MTASEMA NINI KWETU SISI WANYONGE MTATUONEA KWA FEDHA ZENU LAKINI MJUI MTAKUFA VIBAYA TENA KWA MATESO MAKALI MLIZENZI DITO LEO HII YUKO WAPI KAMA SIO BABA WA HAKI NDIYE ALIYESEMA BASI KUWENI NA HURUMA NA NCHI MLIOYOIKUTA WAHENGA WAMEICHA IKIWA IMEJAA UTAJIRI LEO HII MNAGEUZA WENU LOWASA BIBLIA INASEMA USIPO TUBU KIZAZI CHAKO KITALAANIWA SUBIRI HISTORIA SIKU ZOTE ITALIPA NA MALIPO NI HAPA HAPA

na mtanzania, dsm, - 27.05.08 @ 12:05 | #13560

Chadema/Nccr/Cuf/Udp na wapofu wengine kama hamjasoma vile, mnakurupuka kama mipaka na Mijibwa Mijizi, hamna mpya mambo yeshawashinda haya, Ngoma hamuiwezi.

na lyatonga, Tz Tandika
 
HIVI nani kawaambia balali hayupo dunia hii??? Jamaa habari zakuam jamaa kakutana naye ktk ------------
aliposema salalehh !!!!!!!!!!! wewe si umetutoka UNAJUA nini alijibu
Mimi yani yeye ni mzimu wa Balali
 
Teh teh teh teh!!!!!!!!!!!!!!!!! Hii awamu ya JK tutasikia mengi. Mpaka ifike 2015 sijui itakuwaje!!!
 
si mchezo so interesting!basi ni maajabu ya dunia!yaani watu wanakataliwa kwenda kuhani?au mama balali hajui kama mwanae kafa?so watu wakienda atashangaa kwa nini wanaenda kumhani?
 
Wanaogopa ataongea nini na hivyo kuamua kuweka ulinzi ili kumziba mdomo!!!! Mafisadi wanahaha kila kona kulinda wasiabike!!
 
wanamziba mdomo mama wa watu, kwa nini hawakumruhusu hata kwenda marekani kwenye msiba wa mwanae? wanaogopa atasema walizika gogo kule na kuwa mwanangu yupo visiwa vya malta na jana alinipigia simu--oyaaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom