Pinda amtisha Rais Kikwete; Aweza kujiuzulu wakati wowote “kulinda hadhi yake” | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda amtisha Rais Kikwete; Aweza kujiuzulu wakati wowote “kulinda hadhi yake”

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 1, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]

  [​IMG]
  Na Mwandishi wetu - Imechapwa 25 April 2012

  [​IMG][​IMG]
  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda aweza kujiuzulu wakati wowote kwa kile kilichoelezwa ni “kulinda hadhi yake,” MwanaHALISI limeelezwa.


  Taarifa kutoka mjini Dodoma zinasema iwapo Rais Jakaya Kikwete hatafukuza mawaziri watuhumiwa ufisadi na kushindwa kazi, basi Pinda aweza kujiuzulu.

  Kwa siku nne mfululizo, wabunge wamemkoromea Pinda, wakitaka achukue hatua dhidi ya mawaziri wanane; la sivyo ang’atuke yeye.


  Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe, aliongoza mchakato wa kukusanya saini za wabunge ili kutoa hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu kwa kushindwa kusimamia mawaziri.


  Mawaziri wanaotuhumiwa wametajwa katika ripoti za kamati tatu za kudumu za bunge zikinukuu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.


  Ripoti ya CAG inayoonekana chachu kuu kwa wabunge kushinikiza mawaziri kujiuzulu, inaanika upotevu, wizi, ukwepaji kodi na matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi katika serikali na taasisi zake.


  Lakini hadi juzi Jumatatu, wakati bunge likiahirishwa, Rais Kikwete alikuwa hajatoa neno juu ya shinikizo la wabunge kwa Pinda.


  Wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema hatua ya rais kunyamazia malalamiko dhidi ya mawaziri wake, yaweza kumpotezea mtendaji mkuu anayeonekana msafi.


  Vyanzo mbalimbali vya habari vimesema tuhuma dhidi ya mawaziri na watendaji wengine serikalini ni za muda mrefu, lakini rais aliyewateua, ameamua kuwabeba.


  Hata baada ya kuwa baadhi ya mawaziri wanatuhumiwa wizi, ubadhirifu wa fedha za umma na kushindwa kuwajibika kikazi, bado rais ameendelea kunyamazia.


  Akizungumzia ukimya wa rais, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amesema, “…kama rais angefuata ushauri wangu wa kuvunja baraza la mawaziri mapema mwaka huu, haya ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu yasingekuja.”


  Dk. Slaa aliyekuwa akihutubia mkutano wa hadhara jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, alisema, “Uozo wa serikali unatokana na baadhi ya mawaziri kufanya ubadhirifu kwa muda mrefu bila kuchukuliwa hatua.”


  Wiki hii zimepatikana taarifa kwamba mawaziri wawili wa Kikwete wamenunua nyumba za mabilioni ya shilingi jijini Dar es Salaam.


  Mawaziri hao, miongoni mwa wanaoshinikizwa kujiuzulu, hawakupatikana kwa simu hadi tunakwenda mitamboni, ili watoe kauli kuhusu tuhuma hizo.


  Hata hivyo, taarifa za upande unaotetea rais zinasema Pinda ndiye ameshindwa kutumia madaraka yake kudhibiti wabunge hadi wakafikia hatua ya kumkoromea.


  Wabunge wenyewe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanamtetea Pinda kwamba asingeweza kuzuia kauli za kupinga ubadhirifu, hata kama wenye nia tofauti walipata nafasi ya kujipenyeza.


  Mbunge ambaye hakutaka kutajwa jina amesema, kuna waliopaza sauti eti kwa kuwa “rais alikataa kuwaongezea posho” huku wengine wakidai baadhi ya mawaziri wakifukuzwa, wao wanaweza kufikiriwa kupanda ngazi.


  “Tatizo ni kwamba pamoja na shinikizo kwa waziri mkuu, bado rais haonekani kushtuka. Hii inaleta hisia kwamba naye anataka kumtosa,” amesema.


  Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki) amesema kuchoka malalamiko ndiko kumewasukuma kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.


  “Wabunge wamechoka kuona mawaziri wana mali nyingi zisizolingana na vipato vyao. Wanatumia madaraka vibaya kula rushwa, na hakuna hatua zinazochukuliwa. Ndio maana tunataka kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.”


  Amesema ingawa rais halazimishwi kutekeleza mambo anayoshauriwa, lakini kunyamazia hayo yote ni kama kumwangusha waziri mkuu wake.


  “Inawezekana hii ikawa ni kumwangusha waziri mkuu; maana huwezi kujua hasa inapokuwa siyo mteule wake wa kwanza. Unajua chaguo lake la kwanza alikuwa Lowassa (Edward) na huyu akaja kama chaguo la pili,” alisema.


  Pinda aliteuliwa mara ya kwanza Februari 2008, baada ya Lowassa kujiuzulu.


  Mbunge wa Bunda, Alphaxard Lugola amesema, “…naona tulikofikia katika hili, tuko sahihi. Hatuna nia mbaya na chama chetu. Tunalenga kuisaidia serikali. Nawashangaa wenye chama chetu wanaotushutumu.”


  Lugola amesema ameamua kuwaunga mkono wabunge waliotia saini azimio la kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu kwa kuwa si yeye peke yake, bali wabunge wote wanataka serikali iwe na nguvu na iwaondoe mawaziri walioshindwa kazi.


  “Nashangaa wanatulaumu eti tunataka kuangusha serikali ya CCM. Hoja hii haikuletwa na wapinzani; imeletwa na kamati ya bunge. Sioni sababu ya kutoiunga mkono,” amesema.


  Mbunge mwingine wa CCM, Deo Filikunjombe (Ludewa), amesema tangu aweke saini azimio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu, “…napigiwa simu kila kona kunipongeza, lakini ajabu wengine kwenye chama wananuna.”


  Amesema wabunge wamefikia hatua hiyo katika kutimiza wajibu wao wa kuisimamia serikali badala ya kuendelea kuishauri tu kama walivyokuwa wamezoea.


  “Wabunge tumechoka. Hao mawaziri wanane unaosikia wanalalamikiwa ni wachache tu; wako wengi wenye matatizo makubwa. Na hatua unazoona sio mwisho wake. Tunataka kukaa kama bunge imara kuisimamia serikali,” ameeleza.


  Katika mkutano wa saba wa bunge uliomalizika Jumatatu, wabunge wa CCM na wa upinzani walishikamana kutaka kumng’oa Pinda iwapo mawaziri watuhumiwa hawatajiuzulu au kufukuzwa.


  Februari mwaka huu, taarifa zilisema Rais Kikwete alikuwa anakusudia kubadilisha mawaziri kwa sababu ya “kuyumba kwa serikali,” lakini hakufanya hivyo.


  Taarifa zinasema inawezekana alisita kutokana na vyombo vya habari kufichua mkakati wake mapema.


  Bunge liliahirikishwa bila mawaziri watuhumiwa kuonyesha dalili za kujiuzulu; baadhi wakiapa hawatajiuzulu.


  Mawaziri hao ni Mustafa Mkulo wa wizara ya Fedha, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige.


  Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Hadji Mponda.


  Maeneo makuu ambayo CAG ameripoti ubadhirifu na wizi ni pamoja na Wizara ya Afya (Sh. 10 bilioni), Mabilioni ya JK (Sh. 21 bilioni), ukwepaji kodi (Sh. 15.4 bilioni), Maliasili na Utalii (Sh. 875 milioni) na magari ya serikali (Sh. 5 trilioni).


  Pia katika Shirika la Viwango (Sh. 29.3 bilioni), mishahara hewa (Sh. 1.8 bilioni), Tanesco (Sh. 600 bilioni), Bodi ya Pamba (Sh. 2 bilioni), ununuzi tata (Sh. 8 bilioni), Idara ya Mhasibu Mkuu (Sh. 49. bilioni) na udhamini wa serikali Sh. 3 bilioni.


  Taarifa za kuaminika zinasema mawaziri husika walibanwa katika kikao cha wabunge wa CCM, Alhamisi iliyopita wakitakiwa kujiuzulu; la sivyo waziri mkuu ajiuzulu kwa kushindwa kuwawajibisha.


  Pinda aliyeongoza kikao hicho, aliahidi juzi hiyo kuwa angeeleza hatua ambazo zimefikiwa katika kumaliza suala hilo. Hadi anatoa hoja ya kuahirisha bunge hakusema lolote.


  Ukimya wake uliwaacha wabunge na dukuduku; na hata Spika Anne Makinda alipohoji wakati wa kupitisha hoja ya kuahirisha bunge, sauti za kukataa zilisikika kama zinawiana au kupita zile za kukubali.


  Hata hivyo, kwa mamlaka yake alihitimisha, “Nafikiri walioafiki wameshinda.”   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Kwanini kutishiana kama watoto; kwanini asijiuzulu ni muda mrefu sasa toka Bunge liahirishwe

  Au anasubiri utamu wa Uwaziri Mkuu tena?
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hili ni samba la Kibrazil!
   
 4. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa vitendo ambavyo JK amemfanyia pinda, afu pinda anaona shwari tu, hachukui hatua yoyote, ni lazima huyu Pinda atakuwa ameshachukuliwa msulule muda mrefu sana, yani hapa limebaki gogo, lkn watu wanaona mtu.
   
 5. mwangalizi

  mwangalizi JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 60
  Kaa kimya!
   
 6. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kwa jinsi alivyotendwa na JK kama angekuwa mtu msimamo angekuwa ashasepa ili pinda alisha-pinda toka zamani hawezi kujiuzulu aache utamu wa waziri mkuu
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Pinda ni msukule ndo maana hajitambui
   
 8. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Pinda gani?

  Yule aliyelia bungeni? amtishie JK mwanajeshi?

  You must be dreaming!
   
 9. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Pinda ni dhaifu sana hana uwezo wa kuwa PM. Aondoke tu.
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Maneno yako yanakuwa kama ya utani lakini inawezekana ni kweli kwani hapa tunashuhulika na watu wanaoamini mambo ya ushirikina kwa kwenda mbele; lakini kumbuka pia kuwa Pinda anatoka Sumbawanga ambako nako kwa utamaduni huo hawako nyuma!!
   
 11. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,696
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Pinda anafaa kuwa TAMISEMI siyo uwaziri mkuu
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  JK si mwanajeshi. Hakumaliza masomo. Alitoroka.
   
 13. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Acha majungu kamanda!
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kamtishia Kikwete au kalialia mbele ya Kikwete? Hahaha. Kama ana ubavu wa kumtishia Kikwete kwa nini asiwe na ubavu wa kutishia watumishi chini yake?
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hivi nani ana uafadhali kati ya Pinda na JK ? Wale wanajuana mie sisemi wacha nile ugali wangu na mlenda
   
 16. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  wewe sidhani kama zimo sawasawa umekuwa unakurupuka na mada ambazo hazina kichwa wala miguu hivi hujisikii aibu? kwani kuwa mwanajeshi ndio nini?? umeambiwa wanatishiana kupigana?? siasa ni mbinu na akili sio vita halafu kumbuka jk ndio kamteua pinda so lazima waheshiane! ila wewe unaleta swaga zako za kipuuzi!!
   
 17. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kama anaachia ngazi na aachie ngazi-mambo ya kutishana watu wazima yashapitwa na wakati
   
 18. T

  Tesha1 New Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania tutanyanyasika mpaka lini tutawachumia hawa mafisadi mpaka lini HII NI CHUNGU ISIYO NA KIPIMO eti tanzania nchi ya amani na upendo ni kweli hii kitu
   
Loading...