Jaji Werema kuchukua fomu wiki hii

Status
Not open for further replies.

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,835
18,248
Kada maarufu wa CCM na aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, anatazamiwa kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa na chama chake kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapema wiki hii. "Haiko wazi ni tarehe gani rasmi atafanya hivyo lakini, kwa vyovyote vile, itakuwa ndani ya wiki hii". "Alisema mpambe wake mmoja".

Kuchukua fomu kwa kada huyo nguli wa CCM kutafanya jumla ya watia nia kutoka mkoani Mara kufikia 5. Mpaka sasa makada 4 kutoka Mara wameishachukua fomu za kuwania uteuzi.

Jaji Werema alijiudhuru wadhifa wake wa AG kufuatia kashfa ya ESCROW ambayo bado inaendelea kuitikisa nchi. Pia Werema aliwahi kumuita Mbunge Kigoma kusini, Dr David Kafulila, jina la TUMBILI baada ya mbunge huyo kumuandama sana na tuhuma za Escrow bungeni.

MAONI YANGU

Naona ndoto za urais wa nchi hii kurejea mkoa wa Mara zinakaribia kutimia. Mpigania uhuru na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mtakatifu Julius Kambarage Nyerere, ni mwenyeji wa mkoa wa Mara.


:israel:
 
Sasa hivi imekuwa ni fasheni kwa yeyote aliye wahi kutuhumiwa jambo lolote na kujiuzulu kuona achukue fomu. Yaani Tanzania ukituhumiwa kuwa mwizi badala ya jambo hilo kukutia aibu ndio kwanza lina kupa umaarufu na unapata wapenzi wengi wa kukusupport.
Hii ni ishara kuwa CCM imetuharibia nchi na kuufanya wizi na ufisadi kuwa jambo la fahari sana. Ndio maana Lipumba kasema wale waliostahili kuwa jela leo hii wanatamba mikoani kutafuta wadhamini.
 
Mmh makubwa, yaani wengi wanaochukua fomu za kutaka kugombea ni makada wenye Kashfa kubwa sana za kifisadi. Mfano Lowassa, Muhongo, Ngeleja, Kitine, Sumaye, Pinda, na sasa Werema!!
 
Bangi sasa zinatumika siyo uongo hii ni zaidi ya uongo.

mkuu, usiwe na shaka, tusubiri tuone kama kweli atachukua ndani ya wiki hii kama alivyodhamiria. tatizo ni kwamba hata wezi wakubwa kabisa katika nchi hii wanatamani kuingia magogoni. rahisi kikwete ameufanya urais wa nchi hii uonekane ni suala rahisi na linaloweza kufanywa na mwendawazimu yeyote yule. hii ni hatari sana.
 
Mwanasheria mkuu ni mwanachama wa chama cha SIASA au amejiunga baada ya kustaafu?
 
Mwanasheria mkuu ni mwanachama wa chama cha SIASA au amejiunga baada ya kustaafu?

Werema ni mwanaCCM tangu akiwa chipukizi wa Tanu Youth League (TYL). wewe unadhani mtu asiyekuwa mCCM anaweza na rais na mwenyekiti wa CCM kuwa AG, CJ, RC au DC?
 
Last edited by a moderator:
Mbona tetesi zilikuwa hata Jaji Augustini Ramadhani nae angechukua fomu kesho JutanoJumatano au ni uzushi tuuu?
 
Hapo nasubiri siku mkuu anatoka tutasikia mengi sana.Hii tayari imejithihirisha.
Kama alivyosema leprofeseli lipumba kuwa,wanaotaka uraisi CCM ni wale wanaotakiwa kuwa jela.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom