Jaji Shangwa atoa mpya katika kesi ya kakobe.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Shangwa atoa mpya katika kesi ya kakobe....

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Oct 31, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,858
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Jaji atoa ushauri kumng'oa Kakobe [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Sunday, 30 October 2011 20:43 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  James Magai
  JAJI wa Mahakama Kuu, Augustine Shangwa amewashauri walalamikaji katika kesi inayomkabili Askofu Zachary Kakobe kuwashawishi waumini wa kanisa hilo, wamng'oe madarakani kama wana hoja za msingi.

  “Kama mnaona kuwa Askofu Kakobe anakwenda kinyume, basi muwekeni kiti moto na kama mnaona sasa amekuwa dikteta, hawafai basi tumieni nguvu ya waumini kumpindua katika nafasi hiyo,” alisema Jaji Shangwa.

  Jaji Shangwa alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa kwa ajili ya kupanga tarehe ya kutoa uamuzi wa kama Askofu Kakobe anastahili kushtakiwa au la.

  Hatua hiyo imekuja baada ya Askofu Kakobe kuwawekea pingamizi walalamikaji kwa kile alichoieleza Mahakama kuwa hawana haki kuzungumzia masuala ya kanisa kwa kuwa si viongozi tena.

  Uamuzi wa ama walalamikaji hao wana haki ya kumshtaki Askofu Kakobe au la, utatolewa Novemba 30, mwaka huu.

  Askofu Mkuu huyo wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), anakabiliwa na kesi ya madai Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akituhumiwa kwa ubadhirifu wa mali na fedha zaidi ya Sh14 bilioni pamoja na ukiukwaji wa katiba ya kanisa hilo.

  Kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2011, ilifunguliwa na Dezedelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma ambao wanadai kuwa ni wachungaji wa kanisa hilo.

  Hata hivyo, Kaduma amejitoa baada ya kupata ajali mbaya na kufanyiwa upasiaji kichwani, lakini msimamizi wa kanisa hilo wilayani Liwale, Mkoa wa Lindi, Mchungaji Ignas Innocent ameiomba Mahakama hiyo imwunganishe na walalamikaji hao katika kesi hiyo.

  Akisikiliza kesi hiyo juma lililopita, Jaji Shangwa mbali na kuwashauri waumini hao kuimaliza kesi hiyo wenyewe, alipendekeza walalamikaji hao wafungue kesi ya jinai katika maeneo yanayoonekana kuwa ni makosa ya jinai.

  Akisoma madai ya walalamikaji hao kipengele kimoja kimoja, Jaji Shangwa alihoji ni vipi Mahakama inaweza kuamua madai yanayohusiana na mapato na matumizi ya kanisa na taratibu nzima za uendeshaji wake.

  Jaji Shangwa alipendekeza kuwa kwa madai yanayoonekana kuwa ya jinai, walalamikaji hao wafungue kesi ya jinai badala ya madai.

  Alisema madai kama ya wizi na kusababisha kifo cha muumini, hayastahili kuchanganywa na madai kwa kuwa yenyewe ni ya jinai.

  “Madai kama haya ni ya jinai hivyo inabidi mfungue mashtaka ya jinai. Kama DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) akikataa mnaweza kufuata utaratibu wa private prosecution (mashtaka binafsi),” alisema Jaji Shangwa.

  Hii ni mara ya pili kwa Jaji Shangwa kuwashauri walalamikaji hao kutumia njia mbadala wa Mahakama kumaliza mgogoro wao dhidi ya Askofu Kakobe. Agosti Mosi, mwaka huu aliwashauri walalamikaji hao kutafakari upya juu ya madai yao ili kuona kama yana msingi.

  Pia aliwatahadharisha kuwa iwapo wataamua kuendelea nayo na katika uamuzi wa mahakama, wakashindwa, watajuta kwa sababu watatakiwa kumlipa Askofu Kakobe fidia kubwa na gharama za uendeshaji kesi, ambazo hana hakika kama watazimudu.

  Kabla ya kuwashauri walalamikaji hao, Jaji Shangwa alianza kwa kuonyesha wasiwasi wake juu ya msingi wa madai ya walalamikaji kuhoji matumizi ya fedha za kanisa hilo. Alisema kwa mfumo wa FGBF, Askofu Kakobe ndiye kanisa na kwamba mapato ya kanisa hilo ni mali yake kwa sababu, alilianzisha mwenyewe na kuhoji iweje wamhoji mtu anayetumia mali yake.

  “Kwani ni nani alimpa Kakobe uaskofu? Kakobe alijifanya mwenyewe, ni tofauti na maaskofu wa Katoliki ambao mpaka waende wakasomee.”
  Msiniambie nina-prejudge (nihukumu kabla), maana huwa mnatulaumu kesi kurundikana mahakamani. Mimi hapa natafuta suluhu na suluhu ni pamoja na kuondoa kesi mahakamani,” alisema Jaji Shangwa.

  Alihoji kosa la Askofu Kakobe kukusanya michango kutoka kwa wana jumuia na kwenye mikutano ya mahubiri anayofanya nchi mbalimbali kujengea nyumba yake kama walalamikaji wanavyodai.

  “Lakini si anatumia fedha zake? Mimi najiuliza maana ndiye alianzisha kanisa, kama kulikuwa na wafadhili ndipo akawafundisha na nyie mkawa wachungaji. Hizi fedha hapewi na Serikali ni za wale anaowatibu na wanaokuja kuombewa mapepo. Kwa hiyo anazikusanya kwa huduma, sasa mtamwulizaje na chake? Labda mngesema kuwa hawapi au anawapunja mshahara wakati mnashinda kanisani mnaombea mapepo, maana hii ni kazi kubwa.”

  Katika madai yao, walalamikaji hao walieleza kuwa, Askofu Kakobe alikusanya michango kutoka kwa waumini inayofikia Sh14 milioni kwa ajili ya kununulia kiwanja cha kanisa, lakini ikabainika kuwa kiwanja hicho kilinunuliwa kwa Sh4 milioni tu.

  Madai mengine katika kesi hiyo ni Sh2 bilioni wanazoeleza kuwa alipewa Askofu Kakobe kwa ajili ya kujengea makazi ya Kiaskofu, lakini mpango huo umekufa na badala yake anataka kuhamia Marekani kabla ya kurejesha fedha hiyo.

  Wachungaji hao pia wanataka Askofu Kokobe arudishe Sh800 milioni alizopewa kwa ajili ya kununulia vifaa vya kuanzisha kituo cha matangazo ya televisheni kwa maelezo kuwa vifaa hivyo havikununuliwa kwa kuwa eneo la mradi huo, limeathiriwa na mradi wa umeme wa msongo mkubwa.

  Kuhusu kifo cha mmoja wa waumini, walalamikaji hao wanadai kuwa, Askofu Kakobe aliwashawishi waumini kufunga siku saba bila kula, jambo lililosababisha mmoja wao kufariki dunia.

  Hati ya madai inaeleza kuwa walalamikaji hao wanamtuhumu Askofu Kakobe kuwa amekuwa akikusanya fedha nyingi kutoka kwa waumini wake kwa madai ya kufanyia shughuli na miradi mbalimbali ya kanisa na kuzitumia kinyume cha malengo.

  Mbali na kuzitumia isivyo, kama vile kugharamia kampeni za kisiasa kinyume cha katiba ya kanisa hilo, pia wanadai kwamba amekuwa hatoi taarifa ya mapato anayokusanya wala matumizi yake.
  Kuhusu ukiukwaji wa Katiba ya kanisa hilo, walalamikaji hao wanadai kuwa katiba inataka kuitishwa kwa mkutano mkuu kila baada ya miaka mitano, lakini Askofu Kakobe hajawahi kuitisha mkutano huo tangu mwaka 1989.

  Pia wanadai kuwa katiba ya kanisa hilo, inataka kanisa liwe na katibu mkuu na mweka hazina, lakini Askofu Kakobe amekuwa akifanya kazi zote hizo peke yake.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,858
  Trophy Points: 280
  mob justice should not be hailing from the court....................
   
 3. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,069
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  yeye si ndo kaanzisha kanisa?mlikuwa wote?sasa kwanini mumbanebane?wewe unajua madhumuni ya kuanzisha kanisa?kama vipi anzisha lako.aliyekufa kwa njaa ni ujinga wake kwani kalazimishwa.alitakiwa awe na akili za mbayuwayu.
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hii kesi ina tatizo....namna inavyoripotiwa (kwa makusudi fulani) au/na namna inavyisikilizwa (jaji mbona kama tayari anajua hukumu kabla hajasikiliza?). Bado naikumbuka ile sound clip ya mama rwakatare!
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Huyu jaji amekuwa akitoa ushauri huu tangu hii kesi ilipofunguliwa
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  I thank God that I have personal relationship with Him NOT any church or religion
   
 7. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Hao wachungaji watatu hata kama hawakuanzisha pamoja na Askofu Kakobe hilo FGBF Church,wakati mwingine idea inaweza kuwa ya Kakobe,ama wito alipewa Kakobe akajikusanya na familia yake nyumbani kwake K,nyama.Kila Jpili ibada. Bdae wakapatikana majirani,na wakafanya mahubiri labda stendi ya basi n.k.wakapatikana pengine waumini wapya mf.Kaduma,Angelo.Nao wakasali wakaalika ndugu zao mfano Angelo kumualika kakake Deuz. Wakijihesabu wako 6 ama 8 tu. Kakobe anawaambia acheni shughuli zenu zote muifanye kazi ya Bwana. Unakuja kukuta akina Angelo na ndugu zake wanatembea kwa mguu muda mrefu,wakati wa jua kali na chakula inakuwa shida. Tena unakuta walilazimika kuacha kazi,mmoja kati yao ama wote ilikuwa waanze kazi ama walikuwa BOT. Wanatoka nyumbani,wanahamia madarasa ya shule ya msingi Jamhuri mpaka kanisa linakua kiasi hicho. Wanafundishwa masomo ya Uchungaji na kupelekwa mikoani.Mf Kaduma kwenda Dodoma. Hapo unaongelea mambo ya takribani miaka 20 na ushee iliyopita. Hoja yangu ni kuwa Askofu anamiliki kanisa kwa kuwa ni idea,wito wake? Na waliosacrifice fani zao na kazi zao je?
   
 8. k

  kitimtim JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Hakuna kesi hapo, huo ni ubunifu na idea binafsi za kakobe, wao wanaona wivu, anzisheni na nyie project zenu.
   
 9. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  haya makanisa ya kilokole mcharuko kweli
   
 10. J

  Jamuhuri Huru Member

  #10
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu hiyo ndio inaitwa "Judicial Hunch", hapo inaonekana Mh Jaji anamfahamu Kakobe na hilo kanisa mbali na nafasi aliyonayo kama mwamuzi. Hapo mimi mwenzio namkumbuka Kabwetele...........
   
 11. h

  humphrey shonga Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yote haya ni matatizo ya kujitenga na kanisa mama na kinachofuata baada ya hapo ni taasisi binafsi kwa maslahi binafsi
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  we HUMPULE unataka wenzako wakale wapi? Makanisa ni bonge la dili
   
 13. K

  KASIGAZI Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kanisa maana yake original ni watu walioitwa/waliotengwa/waliochaguliwa. Watu hawa hawajulikani mahali popote isipokuwa kwa Mungu anayefahamu mioyo yao. Taasisi zote zinazojiita kanisa huku duniani si kanisa as such. Kwa hiyo hata huo utetezi wa kanisa mama siafikiani nao. Hakuna kanisa mama wala mtoto. Ukisema taasisi ya kidini mama nitakuelewa. Kanisa si la kakobe wala askofu yeyote, kaldinali wala papa, ni la YESU ,na liko katika kila taasisi ya kidini, na hata nje ya taasisi hizo. Kwa hiyo acha wana taasisi ya kakobe wakabane naye kama kuna mambo yao(si ya Mungu) amekiuka.
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wasiwasi wangu ni kwamba, aidha mheshimiwa jaji ni muumini/mashabiki wa kakobe ama amepotoka.

  Anachokifanya sasa kwa kudai ni ushauri ndio hukumu yenyewe anayowaandalia. Haiingii akilini jaji awashauri kufuta kesi na kwamba wakishindwa wataamuliwa kulipa gharama kubwa ambazo hawatozimudu, halafu utegemee kwamba ataweza kutoa hukumu tofauti na ushauri anaoutoa sasahivi.

  Hata kama kanisa ni la kakobe, fedha anazochangisha si za kwake, si stahili yake. Aanapokuwa anachangisha hizo fedha hasemi kwamba wamchangie, anwahimiza waumini kuchangia kwa ajili ya kazi fulani, mathalani kununua kiwanja, kujenga kanisa, kujenga nyumba ya askofu na mambo mengineyo. Sasa nashindwa kumuelewa huyu jaji anatumia sheria gani ama busara gani kutoona "wizi" unaofanywa na kakobe.
   
 15. D

  Delko Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao wachungaji watatu nadhani wanashindwa kutofautisha kati ya NGO na kanisa.

   
 16. E

  Evergreen Senior Member

  #16
  Nov 27, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Kwani wali-sacrifice kwa ajili ya Kakobe au kwa ajili ya Mungu? Si imani ndiyo iliwaongoza? Kwani wasimlilie Mungu waanze kupiga mayowe mitaani kama hayawani ambaye hajapata chakula kwa siku 2?
  Kama Kakobe ni Mwovu basi Hasira ya Mungu itakuwa juu yake,kama ni vinginevyo atazidi kubarikiwa kama jinsi ilivyo!!
  Simoni Petro alikuwa Mvuvi,aliacha Uvuvi akamfuata Yesu,he never complained,wafuasi wote wa Yesu walikuwa na kazi zao,waliziacha,wakamfuata Yesu,hakukuwa na kelele za Tumbo!!
   
Loading...