mkuu njia unayoweza kupendekeza ya wananchi kuchukua hatua apart from ballot box labda ni maandamano,na hawa jamaa kwa sababu wanajua kuwa hawako fair watatumia polisi, na kwa sababu polisi wetu akina Chagonja wenyewe hawako safi watakupiga risasi kesho yake haraka chagonja atatangaza kuwa umepigwa na kitu kizito kilichorushwa na waandamanaji na marehemu alikuwa anakimbilia polisi kupata ulinzi,kwisha.umeongea vizuri mkuu lakini tatizo hapa sio ccm bali ni Watanzania (yaani sisi). Hivi fikiria kidogo: Ukija kupanda ndege alafu ukapata ushuhuda wa wazi kuwa rubani hana uwezo wa kutosha unafanyaje? ...au chukulia unaenda kituo cha basi alafu unaona dereva amelewa chakali si unachagua gari nyingine na hata kama umeshalipa si angalau unaonyesha ujasiri wa kudai kurudishiwa nauli yako!?
Sasa sisi tumeshawajua hawa watu na hatufanyi maamuzi yoyote.
Nakumbuka issue ya akliyekuwa mbunge wa Temeke (Kihiyo) ilianza kama masihara lakini ikaishia kujulikana kuwa hakuwahi kusoma DIT/Dar Tech
Kama unamtetea Jaji mkuu kudanganya umri ni haki yako lakini si kwa staili hii ndugu yangu.
Kama aliruka madarasa basi isemwe hapa kwamba aliruka kutoka darasa la kwanza hadi la tano, na ilikuwa lini, i mean mwaka gani, sio maneno matupu kama haya unayoandika hapa, muhimu ni kuweka ushahidi tu wa hilo.
Mwalimu Nyerere alipata bahati hiyo ya kuruka madarasa na wengine wapo waliopta bahati hiyo. Kinachotafutwa hapa ni ukweli wa umri wake na si kutafuta njia nyingine yeyote nyepesi nyepesi na za uongo uongo ya kujustfy utetezi wako juu ya tuhuma hizi za kughushi umri
Kuna kila dalili za ukweli kuhusu hili.
Kuna jamaa wa TISS kanitonya hiyo issue ipo na Usalama wa taifa walikuwa wanatafuta namna ya kuificha sana tangu Lissu alipoanza kufumua uozo wa baadhi ya majaji.
Ataficha miaka ,lakini uso hautauficha utazidi kumporomoka tu na atazidi kuonekana babu,si mashavu yameshaanza kulegea tayari muda si mrefu atakuwa kama babu mla tambuu
Na kwa lishe gani aliyoipata miaka hiyo hadi alipokuwa na miaka minne aonekane ana urefu au size ya kumruhusu kuanza Darasa la kwanza???? Mimi nadhani ilipaswa ajitokeze atufafanulie umri wake ili mgongano huu uishe na heshima yake, ya serikali na ya chombo anachokiongoza viweze kutendewa haki. Akikaa kimya na kujifungia haitamsaidia zaidi ya kumvunjia heshima yeye, familia yake, aliyemteua na ya serikali kwa ujumla. Nadhani ni wajibu wa kiongozi wa umma kutoa ufafanuzi wa jambo ambalo umma umeli-doubt on you or on your office.jamani nyosheni maelezo kuwa kipindi hicho kuanza la kwanza ukiwa na miaka 4 ilikuwa haiwezekani kwani hata miaka ya 80 ulikuwa ukitaka kuanza unaambiwa ushike mkono sikio kwa kupitisha mkono wako kichwani..kifupi kama huna mika nane na kuendelea ilikuwa haiwezekani..tumchunguze hata jk utakuta naeyumo maana tuliambiwa ni kijana mwenzetu..