Jaji Lubuva ataka Tume ya Uchaguzi ifumuliwe

Jaji Lubuva ataka Tume ya Uchaguzi ifumuliwe

Jaji Lubuva Mungu anakuona alivyomfanyia Dad wetu Lowasa hiyo tume haifai kufumuliwa bali inatakiwa kuondolewa yote hafai tena kuendelea kushikilia nafasi hizo.
Mwachen mzee wa watu akajipumzikia kwa amani. Mmemsema weee kwa miaka kadhaa kuwa ni fisadi. Tena kwa kujitapa kuwa na ushahidi. Baada ya kuja mkaamua muue ajenda za ufisadi na kumsafisha. Kwa maslahi binafsi tu ya baadhi ya viongozi. Taifa hili mnataka kulipeleka wapi.
 
Hayo mawazo yangu unatakiwa kuyaheshimu hata kama hayakupendezi Lowasa tunaamini 2020 ataingia IKULU.
Hahahahahaha. Ataingia ikulu kufanya nini. Labda tueleze. Ikulu kuna biashara gani kule??
 
"Kwa hapo baadae tunaona kuwa kuna umuhimu wa serikali kufanyia marekebisho katika muundo huu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuwa na watumishi wake katika kila halmashauri nchini badala ya kuendelea kuwatumia wakurugenzi ambao wapo katika halmashauri,” alisema Jaji Lubuva.

Kosa letu na chanzo cha umaskini wetu ni huu hapa.
Hivi kweli serikali ndo ifanye mabadiliko ya tume... Au kuwepo na chombo chenye mamlaka kikatiba kama bunge kwa ajili ya kufanya mabadiliko hayo..?!
Hivi refa wewe mwenyewe mchezaji wewe mwenyewe kocha wewe mwenyewe alafu ufanye mabadiliko yatakayosababisha mpinzani wako awe na uwezo wa kukushinda...??
 
Note =Tume ya Uchaguzi iliyokuwepo haifai hata kufumuliwa bali inatakiwa kubadilishwa kabisa tunataka Tume huru ya Uchaguzi .
Jaji Lubuva anatakiwa kusema wazi Tume yake ya uchaguzi haipo huru kwa sababu viongozi waandamizi wa Tume hiyo wote ni wateule wa Rais.
Libuva ataka NEC ifumuliwe

Akizungumza jana wakati wa kukabidhi taarifa ya tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, alisema ushauri huo umo katika mapendekezo yaliyotolewa ndani ya ripoti hiyo.

Lubuva alisema katika mapendekezo hayo, serikali imeshauriwa kubadili muundo wa tume hiyo ili kuwa na ofisi na wafanyakazi wake katika kila halmashauri zote nchini pamoja na Zanzibar.

Kwa muda mrefu NEC imekuwa na watumishi katika ofisi yake kuu jijini Dar es Salaam wakati wasimamizi wa majimbo na wasaidizi pamoja na waratibu katika ngazi za mikoa wamekuwa wakiteuliwa wakati wa uchaguzi.

“Kwa hapo baadae tunaona kuwa kuna umuhimu wa serikali kufanyia marekebisho katika muundo huu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuwa na watumishi wake katika kila halmashauri nchini badala ya kuendelea kuwatumia wakurugenzi ambao wapo katika halmashauri,” alisema Jaji Lubuva.

Katika tathmini hiyo matokeo, alisema mwitikio wa wapigakura katika baadhi ya maeneo ulikuwa mdogo kutokana na watu wachache kujitokeza kupiga kura ikilinganishwa na waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura.

“Baadhi ya sababu zilizotolewa ni pamoja na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa kupiga kura kutokana na elimu ya mpigakura kutowafikia walio wengi ikiwa ni pamoja na wapigakura wengi waliojiandikisha kutaka vitambulisho kwa ajili ya matumizi mengine na uwapo wa hofu ya vurugu siku ya kupiga kura,” alisema.

Alizitaja changamoto zingine kuwa ni pamoja na mpigakura kutoruhusiwa kupiga kura katika eneo tofauti na lile alilojiandikishia, wapigakura kushindwa kupiga kura siku ya uchaguzi kutoka na kugawa mipaka mipya ya kiutawala na majimbo.

Baada ya tathmini hiyo, alisema tume imeandaa na kuambatanisha mpango wa utekelezaji wa muda mrefu na mfupi juu ya hatua muhimu za ufumbuzi wa changamoto zilizoainishwa na wadau wa uchaguzi.

Naye Waziri wa nchi Ofisi ya Wziri Mkuu, Jenista Mhagama, alisema kuwa Tume inatakiwa kufanyia kazi changamoto na upungufu uliojitokeza ili kuboresha uchaguzi mkuu ujao.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima, alisema toka tume hiyo ianzishwe mwaka 1993, tathimi hiyo iliyokabidhiwa kwa serikai ni ya kwanza kufanyika.

Aidha, alisema kutokana na changamoto ambazo zilijitokeza katika uchaguzi mkuu uliopita, tume inatarajia kuongeza muda wa kutoa elimu kwa mpigakura ili kuboresha uchaguzi mkuu ujao.

Kailima alisema katika maeneo mengi waliyofanya tathimini, imebainika kuwa idadi kubwa ya watu walikuwa hawana elimu ya mpigakura hali iliyosabisha wengi kushindwa kutumia haki yao ya msingi kuchagua kiongozi wanayemtaka.

Alisema tume inapendekeza elimu ya mpigakura iwe inatolewa katika kipindi cha mwaka mzima na sasa wamejipanga kuifanya elimu hiyo kuwa endelevu hadi uchaguzi mwingine utakapofanyika mwaka 2020.
View attachment 425957

Matatizo makubwa katika chaguzi zetu yana changiwa na tume hiyo kuonekana kama kwamba haiko huru.
- Huwezi kusema unatume huru ambayo ina base kusaidia upande mmoja hasa ule uliowaweka madarakani.
- Hakuna kitu kibaya kama kuwafanya watu hawana akili, mtu hapotezi muda wake kuja kupiga kura ambazo anajua hatima yake ni figisu.
- Kwa bahati nzuri malipo huwa hapahapa duniani, baadhi ya wakurugenzi walio hakikisha kuwa kwa gharama yoyote lazima wafurahishe kundi fulani badala ya wananchi wamelipwa hapahapa walikuwa daraja la watu fulani na mara tu watu hao walipo vuka wakabomoa daraja (wako vijiweni sasa). Huo ndo ujira wa dhuruma ya aina yoyote.
- Tuache figisu figisu tukiamua kuwa nchi ya kidemokrasia basi tuheshimu misingi uake.
 
Sasa kama anajua hayo kwa nini kiherehere cha kusimamia uchanguzi,hizo tume zote ya Tanzania na Zanzibar haziko huru,Africa tume kidogo zenye uhuru ni Zambia,Kenya na Botswana.
Usisahau GHANA
 
Siasa bila unafiki haziendi huyu si alipewa ma million na ulinzi Juuu yani huyu ndo wa kutusomea eti matoke jimbo fulan asilimia 0% .1
 
Namwomba Mungu aifumue hii tume kabla ya uchaguzi wa 2020!!
 
hakuna cha jaji, DR wa Pro hapa tanzania, wote wadhalilisha taaluma zao sababu tu ya kuendekeza njaa n kushindwa kujitegemea kutokana na elimu zao
 
Tatizo ni pale mwewe anapomtengenezea kifaranga kiota kizuuri na kumbembeleza aingie..
 
Tume hii sio huru miaka yote, tume inatakiwa ijiendeshe na kuwa na wafanyakazi wake sio kutegemea wakurugenzi ambao wote ni wa chama tawala, nashangaa kwa nini vyama vya upinzani hawalioni hili, hakuna mkurugenzi ambae yuko tayari katika halmashauri zao kushindwa uchaguzi ndo maana matokeo huchukua muda mrefu sana mshindi kutangazwa, tena kama upinzani umeshinda basi lazima vurugu au ubishani utokee kwanza ndo anatangazwa mshindwi, wakati umefika kwa vyama vya upinzani kuungana na kutetea tume huru ya uchaguzi, waanze na kuwakataa wakurugenzi wote kusimamia cuhaguzi, kwa sasa tume ianze mchakato wa kuajiri wenyewe na kuwasambazi katika halmashauri zote.
 
Amini msiamini Mwl JPM hawezi kuifanyia tume marekebisho. Anawajuwa wananchi ni wa aina gani !!!
Kumbukeni hotuba yake kule Singida kwenye sherehe za Ccm kutimiza miaka 39 "MTAWALA YEYOTE HAPENDI KUTAWALIWA HASA NA VYAMA HIVI VYA HOVYO HOVYO "
CCM itafanya chochote cha kuwahakikishia kubaki madarakani ikiwa ni pamoja na kung'ang'ania vyombo vya dola na vya maamuzi(NEC).
 
Amini msiamini Mwl JPM hawezi kuifanyia tume marekebisho. Anawajuwa wananchi ni wa aina gani !!!
Kumbukeni hotuba yake kule Singida kwenye sherehe za Ccm kutimiza miaka 39 "MTAWALA YEYOTE HAPENDI KUTAWALIWA HASA NA VYAMA HIVI VYA HOVYO HOVYO "
CCM itafanya chochote cha kuwahakikishia kubaki madarakani ikiwa ni pamoja na kung'ang'ania vyombo vya dola na vya maamuzi(NEC).


Unaota kivuli chako aisee
 
Aisee ngojeni mkulu ateue maka dar wa See See Emu ili alufu mbili na 20 apite kama ananawa.
 
Unaota kivuli chako aisee
Mr Kinje mimi si pro Gov. Lakini kwa aina ya watu tulionao sioni wa kutusaidia kupata tume huru. Hata wasomi wetu wanavunja moyo sana, bunge letu limejaa ushabiki mwisho wa siku ni NDIIOOOOOOOO

Wananchi wao wameshatiwa uoga na upofu
 
Back
Top Bottom