Jaji Lubuva ataka Tume ya Uchaguzi ifumuliwe

Jaji Lubuva ataka Tume ya Uchaguzi ifumuliwe

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
7,533
Reaction score
22,289
Note =Tume ya Uchaguzi iliyokuwepo haifai hata kufumuliwa bali inatakiwa kubadilishwa kabisa tunataka Tume huru ya Uchaguzi .
Jaji Lubuva anatakiwa kusema wazi Tume yake ya uchaguzi haipo huru kwa sababu viongozi waandamizi wa Tume hiyo wote ni wateule wa Rais.
Libuva ataka NEC ifumuliwe

Akizungumza jana wakati wa kukabidhi taarifa ya tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, alisema ushauri huo umo katika mapendekezo yaliyotolewa ndani ya ripoti hiyo.

Lubuva alisema katika mapendekezo hayo, serikali imeshauriwa kubadili muundo wa tume hiyo ili kuwa na ofisi na wafanyakazi wake katika kila halmashauri zote nchini pamoja na Zanzibar.

Kwa muda mrefu NEC imekuwa na watumishi katika ofisi yake kuu jijini Dar es Salaam wakati wasimamizi wa majimbo na wasaidizi pamoja na waratibu katika ngazi za mikoa wamekuwa wakiteuliwa wakati wa uchaguzi.

“Kwa hapo baadae tunaona kuwa kuna umuhimu wa serikali kufanyia marekebisho katika muundo huu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuwa na watumishi wake katika kila halmashauri nchini badala ya kuendelea kuwatumia wakurugenzi ambao wapo katika halmashauri,” alisema Jaji Lubuva.

Katika tathmini hiyo matokeo, alisema mwitikio wa wapigakura katika baadhi ya maeneo ulikuwa mdogo kutokana na watu wachache kujitokeza kupiga kura ikilinganishwa na waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura.

“Baadhi ya sababu zilizotolewa ni pamoja na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa kupiga kura kutokana na elimu ya mpigakura kutowafikia walio wengi ikiwa ni pamoja na wapigakura wengi waliojiandikisha kutaka vitambulisho kwa ajili ya matumizi mengine na uwapo wa hofu ya vurugu siku ya kupiga kura,” alisema.

Alizitaja changamoto zingine kuwa ni pamoja na mpigakura kutoruhusiwa kupiga kura katika eneo tofauti na lile alilojiandikishia, wapigakura kushindwa kupiga kura siku ya uchaguzi kutoka na kugawa mipaka mipya ya kiutawala na majimbo.

Baada ya tathmini hiyo, alisema tume imeandaa na kuambatanisha mpango wa utekelezaji wa muda mrefu na mfupi juu ya hatua muhimu za ufumbuzi wa changamoto zilizoainishwa na wadau wa uchaguzi.

Naye Waziri wa nchi Ofisi ya Wziri Mkuu, Jenista Mhagama, alisema kuwa Tume inatakiwa kufanyia kazi changamoto na upungufu uliojitokeza ili kuboresha uchaguzi mkuu ujao.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima, alisema toka tume hiyo ianzishwe mwaka 1993, tathimi hiyo iliyokabidhiwa kwa serikai ni ya kwanza kufanyika.

Aidha, alisema kutokana na changamoto ambazo zilijitokeza katika uchaguzi mkuu uliopita, tume inatarajia kuongeza muda wa kutoa elimu kwa mpigakura ili kuboresha uchaguzi mkuu ujao.

Kailima alisema katika maeneo mengi waliyofanya tathimini, imebainika kuwa idadi kubwa ya watu walikuwa hawana elimu ya mpigakura hali iliyosabisha wengi kushindwa kutumia haki yao ya msingi kuchagua kiongozi wanayemtaka.

Alisema tume inapendekeza elimu ya mpigakura iwe inatolewa katika kipindi cha mwaka mzima na sasa wamejipanga kuifanya elimu hiyo kuwa endelevu hadi uchaguzi mwingine utakapofanyika mwaka 2020.
029A4017.JPG.jpg
 
Once more unto the breach ,
dear friends , once more; Or close the wall up
with our English dead.
 
[HASHTAG]#NIPASHE[/HASHTAG] Mwenyekiti NEC, Jaji Damian Lubuva ameshauri NEC kufumuliwa na kuwa na muundo mpya tofauti na ilivyo sasa https://t.co/bfXHBKJaFB
Note =Tume ya Uchaguzi iliyokuwepo haifai hata kuvumuliwa bali inatakiwa kubadilishwa kabisa tunataka Tume huru ya Uchaguzi .
Jaji Lubuva anatakiwa kusema wazi Tume yake ya uchaguzi haipo huru kwa sababu viongozi waandamizi wa Tume hiyo wote ni wateule wa Rais.
Anajutia alichokifanya mwaka jana,nabado wataumbuka...Mungu waonyeshe hawa wadhalimu.
 
Jaji Lubuva Mungu anakuona alivyomfanyia Dad wetu Lowasa hiyo tume haifai kufumuliwa bali inatakiwa kuondolewa yote hafai tena kuendelea kushikilia nafasi hizo.
 
[HASHTAG]#NIPASHE[/HASHTAG] Mwenyekiti NEC, Jaji Damian Lubuva ameshauri NEC kufumuliwa na kuwa na muundo mpya tofauti na ilivyo sasa https://t.co/bfXHBKJaFB
Note =Tume ya Uchaguzi iliyokuwepo haifai hata kuvumuliwa bali inatakiwa kubadilishwa kabisa tunataka Tume huru ya Uchaguzi .
Jaji Lubuva anatakiwa kusema wazi Tume yake ya uchaguzi haipo huru kwa sababu viongozi waandamizi wa Tume hiyo wote ni wateule wa Rais.
Akiwemo yeye
 
Back
Top Bottom