Mazindu Msambule
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 7,509
- 6,862
Chezea Tundu Lissu wewe, huyu jamaa kila anacho kisena huwa ameisha kifanyia research ya kutosha, alitoa kama tahadhari na sasa leo tumeona!
Hiyo kauli sio ya Mwananchi ni kauli ya tume, Mwananchi wamenukuu tu.
...jamani huyu IHEMA mkumbeni kuwa ndo huyu alotajwa na Tundu Lisu kuwa hakuwa na hata tu uwezo wa kuandika hukumu alipokuwa Mahakama Kuu. Je vp angekuwa na uwezo wa kuandika ripoti nzuri leo? Wenye akili ndo mtaanza sasa kumkubali Tundu-Lisu. Mind you: dhaifu ni dhaifu tu!!
wana macho lakini hawaoni, wana masikio na hawasikii! ...huyu jaji naye sina uhakika kama alikuwa kwenye list ya Mh. Lissu
Gazeti la mwananchi limeanza kupoteza dira! Watanzania tunaujua ukweli! Kuanzia leo sitanunua gazeti la mwananchi.hawa wahariri waganga njaa wanatumika kama toilet paper.
usiwahukumu gazeti la Mwanachi wao wamechukua jukumu la kukusaidia kujua yaliyosemwa na tume ya waziri.
hahhaha,,,,,sasa mdau unadhan watu wanaelewa dots zote za events,,,,,???wengine hawajui,mueleweshe tu taratibuHujui kuwa Jaji Ihema ndiye alieongoza tume ya Nchimbi kuhusu mauaji ya Mwangosi?
Hujui kuwa amesoma ripoti yake leo, pamoja na mambo mengne akidai
"NGUVU YA POLISI ILIYOTUMIKA KUTAWANYA WATU, HAIKUHUSIKA KUMUUA Mwangosi!"
Na kwamba hawawezi kutaja chanzo cha kifo, wataingilia mahakama!
Sasa ambacho hukuelewa ni nini ewe kichwa ngumu?
Hakuna Jaji pale wakati akisoma roho ilikuwa inamsuta hadi anatetemeka........hakika huu ni ujinga
Bora hata umenisaidia, nilikuwa najiuliza nimuelezeeje bwana Kichwa ngumu, maana mambo haya yako wazi leo nzima, halafu eti yeye hajasikia na wala haelewi!
Uchunguzi wa tukio la uhalifu daima hufanywa na polisi na baadaye kupelekwa mahakamani kama ushahidi.
Kwa nyakati fofauti, wengi wetu tumejifunza katika historia ya nchi yetu kwamba moja ya sababu za msingi ambazo Mwalimu Nyerere alizitaja miaka 50 iliyopita kwamba ni kikwazo kwa Maendeleo ya taifa letu ni uhaba wa wataalam wa kusaidia kujenga taifa. Hivyo, katika miaka ya mwanzo ya uhuru, ilimlazimu Mwalimu na serikali yake kuagiza wataalam kutoka nje na hawa walikuwa wanalipwa na fedha za walipa kodi wa nchi yetu. Miaka 50 baadae, hali sio tofauti sana kwa maana ya kwamba bado kama taifa, hatuoni bado mchango wa kutosha kutoka kwa wataalam wetu katika kuendeleza nchi yetu. Tunabaki kujiuliza, tatizo ni nini hasa:
JokaKuu,
Ukitazama siasa za CCM, hiki sio chama kinacho appreciate wasomi tena tofauti na miaka ya mwalimu. Nimetolea mfano jinsi gani wasomi wa chuo kikuu walivyokuwa wanashirikishwa katika mijadala inayohusu hali ya nchi kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nina kitabu kimoja kinachoelezea pia ni jinsi gani Mwalimu Nyerere alipata ujasiri wa kuingiza nchi yetu kwenye ujamaa kutokana na wasomi wengi wa Mlimani kukubaliana na mtazamo wake, tatizo likaja tu baadae kwenye utekelezaji. Miaka ya sasa, tuna wasomi wengi sana na wenye hekima sana kutokana na elimu yao na uzoefu wao lakini hawatumiki ipasavyo na wakitumika ni kwa malengo ya kisiasa peke yake na wakishatumika na kufanikishia watawala malengo yao, shughuli yao imekwisha. Pia Tazama tume ya katiba, wengi ya walioteuliwa mle ni kwa malengo ya kisiasa tu; inastaajabisha kuona mawakili wa katiba (constitution lawyers) kama Professor Shivji wanaachwa katika tume hii; hakuna msomi anayejulikana ndani na nje ya nchi kuhusu utafiti wake katika masuala ya katiba kama Issa Shivji; Wasomi wengi walioteuliwa mle ni wale wenye political orientation ya CCM - hili halina mjadala, kama wapo wenye mtazamo ambao ni no-partisan basi ni wachache sana. Na wanasiasa wengi walioteuliwa mle ni kwa ajili ya to heal political wounds, na sio vinginevyo.
The bottom line ni kwamba wasomi wanapotumika kama unavyosema, basi mara nyingi huwa on a partisan way (kwa malengo ya kisiasa - CCM), na sio non-partisan (kwa maslahi ya taifa over and above party politics).
mimi nakushangaa wewe uliyekuwa unategemea haki itendwe na serikali hii, wewe unafikiria kwanini serikali ilikataa kuunda Tume huru yenye nguvu ya kisheria kwa sababu wana nia ya kuwalinda watu wao conclusion yako uliyofikia leo wenzako akiwemo Tundu Lissu walishafikia mwezi uliopita. siku nyingine uwe unasikiliza ushauri wa bure wa chadema hautoumia kichwa tena mkuu.