Je, Mahakama imekwepa wajibu wake kikatiba katika hukumu ya kesi ya Tundu Lissu?

Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,940
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,940 2,000
Tulimsisikia Jaji Matupa wa mahakama kuu akitupilia mbali maombi ya kesi ya Tundu Lissu ya kutaka kurejeshewa ubunge wake, ambao alikuwa akidai kuwa amevuliwa kinyume cha sheria

Katika Shauri hilo Mbunge Tundu Lissu alimtaka Spika Ndugai aithibitishie mahakama hiyo kwa kauli aliyoitoa Bungeni kuwa yeye Spika hajui alipo Mbunge Tundu Lissu.

Hivi katika mazingira ya kumiminiwa risasi 38 katika gari lake na 16 ya risasi hizo kumwingia mwilini na hadi hivi sasa yupo hospitalini Ubelgiji ambako anapata matibabu huku Dunia nzima ikifahamu hivyo, iweje Leo Spika Ndugai adai kuwa hajui alipo Mbunge wake Tundu Lissu??

Katika hukumu hiyo Jaji Matupa alieleza kuwa kuendelea na kesi hiyo na hatimaye kuamua kumvua ubunge Mtaturu, itakuwa ni kuleta mgogoro wa kikatiba kwa kuwa tayari Mbunge Mtaturu ameshaapishwa kwa hivyo kutakuwa na wabunge wawili!

Hebu tumuulize huyo Jaji Matupa, si ndiyo yeye alipokuwa akiisikiliza kesi hiyo katika hatua ya awali alipokuwa akijibu maombi ya upande mashitaka walipotaka Mbunge Mtaturu asiapishwe kwanza kabla kesi ya msingi kuanza kusikilizwa, alijibu kuwa hiyo si hoja ya msingi kwa kuwa kuapishwa kwa Mbunge hakuizuii mahakama yake kuweza kumvua ubunge wake, ili mradi tu ithibitike kuwa kaupata ubunge huo pasipo halali??

Ndipo hapo ninapojiuliza iweje Jaji Matupa atoe kauli mbili zinazikinzana katika kesi hiyo moja??

Turudi kwenye mfumo wa uongozi bora, tunatambua wazi kuwa katika nchi yoyote iliyo na uongozi bora ni lazima iwe na "separation of power" katika mihimili mitatu ya uongozi ambayo ni Mahakama, Bunge na Serikali, katika kile kinachoitwa "check and balance" katika mihimili hiyo mitatu

Kila mhimili umepewa wajibu wake kikatiba, ambapo mhimili wa mahakama ndiyo umepewa wajibu wa kutafsiri sheria ili yule anayeona ameonewa basi atalipeleka Shauri lake huko ili lipate kuamriwa.

Hivi katika mazingira kama ya kesi ya Tundu Lissu Vs Spika wa Bunge, kwa serikali kuweka mawakili 15 dhidi ya 4 wa Tundu Lissu, kwa ajili tu ya kuweka tu mapingamizi ili kesi hiyo isianze kuisikilizwa, hatuoni kama serikali hii iliwekeza nguvu kubwa mno kwa kesi hiyo??

Inawezekanaje kwa serikali kuweka mawakili wengi kiasi hicho kwa kesi ambayo "haiwahusu" ambayo mshitakiwa ni Spika wa Bunge, ambao ni mhimili mwingine unaojitegemea, ambapo nao una mawakili wake??

Hivi katika mazingira haya wananchi tukimbilie wapi, iwapo chombo chetu cha mahakama, klichopewa wajibu kikatiba, kinakwepa wajibu wake??

Hivi sasa ndipo ninapoelewa kwa Rais Magufuli alipotamka huko nyuma, kuwa mhimili wake yeye ambao ni serikali kuwa ndiyo "supreme" kwa kuwa ndiyo umejichimbia zaidi chini!
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,940
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,940 2,000
Saa 10 dak 20 watu bado mnahasira na hukumu?
Ni wajibu wangu kama mwananchi kusema pale ninapoona mambo hayaendi sawa ndani ya nchi yangu

Hebu tu-refer hukumu ya kesi huko Uingereza kwa kutamka kuwa maamuzi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Boris Johnson ya kuamua kuwa nchi yake inaweza kujitoa kwenye umoja wa Ulaya "Brexit" hata pasipo makubaliano, kuwa siyo halali

Tukumbuke pia uamuzi huo wa mahakama umekuja baada ya Waziri huyo mkuu tayari kupata kibali cha Malkia wa nchi hiyo cha kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya hata pasipo makubaliano

Ina maana kwa kesi kama hiyo ingekuwa nchini kwetu, mahakama "ingekwepa" wajibu wake kwa "kusingizia" kuwa kuamua kesi hiyo ingeleta mgogoro wa kikatiba!

Hivyo ndivyo mhimili wa mahakama unavyotakiwa kufanya kazi
 
T

Themagufulianz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2017
Messages
1,813
Points
2,000
T

Themagufulianz

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2017
1,813 2,000
Spika anajua yuko Belgium yes...
Hajuwi city?
Hajuwi hospitali gani anatibiwa?
Hajuwi taarifa za maendeleo ya tiba.
All u can do ni kuuza remorse kuwa alipigwa risasi.... nampa pole na nilichangia matibabu na ntachangia kama itafanyika tena harambee.
Haikuwa ngumu kwa Lissu anayeandikia mitandaoni kila Leo, familia yake, wanasheria wenzake, chama chake, wabunge wenzake na wengine wengi kutoa official report kwa mwajiri wake bunge/speaker.

Mahakama inatakiwa itetee huu uzembe ama Kiburi cha makusudi?

Akionewa ukweli ntakuwa mbele kuandamana na kama kuna michango muhimu inayomuhusu Lissu ntachangia.
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,940
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,940 2,000
Spika anajua yuko Belgium yes...
Hajuwi city?
Hajuwi hospitali gani anatibiwa?
Hajuwi taarifa za maendeleo ya tiba.
All u can do ni kuuza remorse kuwa alipigwa risasi.... nampa pole na nilichangia matibabu na ntachangia kama itafanyika tena harambee.
Haikuwa ngumu kwa Lissu anayeandikia mitandaoni kila Leo, familia yake, wanasheria wenzake, chama chake, wabunge wenzake na wengine wengi kutoa official report kwa mwajiri wake bunge/speaker.

Mahakama inatakiwa itetee huu uzembe ama Kuburi cha makusudi?

Akionewa ukweli ntakuwa mbele kuandamana na kama kuna michango muhimu inayomuhusu Lissu ntachangia.
Tunaelezwa kuwa kulikuwa na mawasilano kati ya Spika Ndugai na ndugu yake Tundu Lissu, Alute Mugwai, ya barua zisizopungua 16, je wewe unaweza kueleza mawasilano hayo yalikuwa hayataji hospitali aliyopo yeye Tundu Lissu??
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,940
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,940 2,000
Spika anajua yuko Belgium yes...
Hajuwi city?
Hajuwi hospitali gani anatibiwa?
Hajuwi taarifa za maendeleo ya tiba.
All u can do ni kuuza remorse kuwa alipigwa risasi.... nampa pole na nilichangia matibabu na ntachangia kama itafanyika tena harambee.
Haikuwa ngumu kwa Lissu anayeandikia mitandaoni kila Leo, familia yake, wanasheria wenzake, chama chake, wabunge wenzake na wengine wengi kutoa official report kwa mwajiri wake bunge/speaker.

Mahakama inatakiwa itetee huu uzembe ama Kuburi cha makusudi?

Akionewa ukweli ntakuwa mbele kuandamana na kama kuna michango muhimu inayomuhusu Lissu ntachangia.
Kwa maamuzi ya mahakama, imetoa "green light" kwa Spika Ndugai kuwafukuza Bungeni wapinzani atakavyo na yeye Spika anajua hata wabunge wa upinzani wakikimbilia mahakamani wataambulia patupu!
 
T

Themagufulianz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2017
Messages
1,813
Points
2,000
T

Themagufulianz

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2017
1,813 2,000
Tundu Lissu alikiri kuwa hakutoa taarifa kwa spika.... ulimsikia?
So spika alitakiwa atafute info kupitia hayo mawasiliano na sio yeye Lissu kutoa official taarifa?
Tunaelezwa kuwa kulikuwa na mawasilano kati ya Spika Ndugai na ndugu yake Tundu Lissu ya barua zisizopungua 16, je wewe unaweza kueleza mawasilano hayo yalikuwa hayataji hospitali aliyopo yeye Tundu Lissu??
 
T

Themagufulianz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2017
Messages
1,813
Points
2,000
T

Themagufulianz

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2017
1,813 2,000
kuna list ya wabunge watoro wakiwamo mawaziri na wengi wa wabunge wakiwa ccm spika alishatoa umewahi kuisikia boss?

Kwa maamuzi ya mahakama, imetoa "green light" kwa Spika Ndugai kuwafukuza Bungeni wapinzani atakavyo na yeye Spika anajua hata wabunge wa upinzani wakikimbilia mahakamani wataambulia patupu!
 
G

Gitarijosenga

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2019
Messages
204
Points
250
G

Gitarijosenga

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2019
204 250
Wewe umesoma sheria? Tuanzie hapo
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
118,572
Points
2,000
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
118,572 2,000
Tusihangaike sana na ishu ya TL.. Hatakaa ashinde popote iwe mvua liwe jua... Huyu alipaswa kuwa marehemu two years .. Amenusurika kifo kwa kudra za mwenyezi Mungu tu... Kumpa ushindi wowote ni kushindwa kubaya kwa wale waliotaka kummaliza na mwanzo wa mapambano mapya.... Hawako tayari kwa hili....
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,940
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,940 2,000
kuna list ya wabunge watoro wakiwamo mawaziri na wengi wa wabunge wakiwa ccm spika alishatoa umewahi kuisikia boss?
Nikuulize wewe wa timu ya Lumumba, hivi umewahi kumsikia Mbunge Nimrod Mkono au Mbunge Muhongo katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita??

Iweje yeye Spika Ndugai alivalie "njuga"_suala la Tundu Lissu, wakati akiwaachia wabunge wenzie wa CCM wawe watoro watakavyo??
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,940
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,940 2,000
Tusihangaike sana na ishu ya TL.. Hatakaa ashinde popote iwe mvua liwe jua... Huyu alipaswa kuwa marehemu two years .. Amenusurika kifo kwa kudra za mwenyezi Mungu tu... Kumpa ushindi wowote ni kushindwa kubaya kwa wale waliotaka kummaliza na mwanzo wa mapambano mapya.... Hawako tayari kwa hili....
Umenena kweli tupu Mkuu Mshana Jr
 
N

Ninaweza

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2010
Messages
9,230
Points
2,000
N

Ninaweza

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2010
9,230 2,000
Spika anajua yuko Belgium yes...
Hajuwi city?
Hajuwi hospitali gani anatibiwa?
Hajuwi taarifa za maendeleo ya tiba.
All u can do ni kuuza remorse kuwa alipigwa risasi.... nampa pole na nilichangia matibabu na ntachangia kama itafanyika tena harambee.
Haikuwa ngumu kwa Lissu anayeandikia mitandaoni kila Leo, familia yake, wanasheria wenzake, chama chake, wabunge wenzake na wengine wengi kutoa official report kwa mwajiri wake bunge/speaker.

Mahakama inatakiwa itetee huu uzembe ama Kuburi cha makusudi?

Akionewa ukweli ntakuwa mbele kuandamana na kama kuna michango muhimu inayomuhusu Lissu ntachangia.
Uzembe na kibri vinasababisha vipi mgogoro wa kikatiba?, .......then Matupa angetamka moja kwa moja kuwa NDUGAI you sahihi kumtimuwa Lissu bungeni
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,940
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,940 2,000
Uzembe na kibri vinasababisha vipi mgogoro wa kikatiba?, .......then Matupa angetamka moja kwa moja kuwa NDUGAI you sahihi kumtimuwa Lissu bungeni
Ni hali ya kushangaza kuona Jaji anakwepa wajibu wake wa kisheria!
 
T

Themagufulianz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2017
Messages
1,813
Points
2,000
T

Themagufulianz

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2017
1,813 2,000
Nikuulize wewe wa timu ya Lumumba, hivi umewahi kumsikia Mbunge Nimrod Mkono au Mbunge Muhongo katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita??

Iweje yeye Spika Ndugai alivalie "njuga"_suala la Tundu Lissu, wakati akiwaachia wabunge wenzie wa CCM wawe watoro watakavyo??
Kumsikia na kuwepo bungeni ni vitu vimbili tofauti....
Wako wanaokwenda wanalala tu ama kusoma magazeti
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,940
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,940 2,000
Kumsikia na kuwepo bungeni ni vitu vimbili tofauti....
Wako wanaokwenda wanalala tu ama kusoma magazeti
Tunachosema ni kuwa Spika Ndugai alikuwa akijua alipo Tundu Lissu.......

Kama alikuwa hajui alipo, aliwezaje kumlipa mshahara kwa kipindi chote kinachokaribia miaka miwili kama alikuwa hajui alipo??
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,940
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,940 2,000
Hajakwepa, kaelekezwa.
Kama ni hivyo ni hatari kubwa, kwa kuwa mhimili wa mahakama unatakiwa uwe "impartial"

Lakini mhimili hui kuwa chin ya Jiwe, basis nchi yetu imeangamia
 
M

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Messages
5,517
Points
2,000
M

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2013
5,517 2,000
Mleta hoja unayasahau yale maneno ya mwenye nchi kuwa, " siwezi kukulipa mshahara mnono, gari, nyumba na posho lukuki kisha utoe ushindi kwa wapinzani!"
Maneno haya yataishi hadi amalize ngwe yake! Na yataendelea kusimama kwa wateule wake wote hivyo usimshangae sana jaji kwani naye ni mteule!
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,940
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,940 2,000
We have interesting services for you:
We are professional research and business writers; we offer a diverse number of services ranging from research works and business document writing
 • Project plans & proposals
 • Business plans & proposals
 • Strategic plans
 • Research proposals
 • Final dissertations/Thesis
 • Public data collection
 • Data analysis
 • Hypothesis testing
 • Mathematical modeling
 • Structural modeling
 • Market analysis
 • Financial analysis and valuations
 • Order of the services
 • Annual reports
 • Memorandum and articles
 • Tender documentation
 • Literature editing
 • Executive speech writing
OUR TEAM IS DEDICATED TO WORK HARD TO SORT YOU OUT AT FRIENDLY RATES (+255) 0768-620781/ WHATSAPP 0653-620781
Wrong posting...........

Peleka kwenye jukwaa la matangazo
 
Forum statistics

Threads 1,336,673
Members 512,696
Posts 32,547,374
Top