Jaji Ihema, Kumbe Tundu Lissu alikuwa sahihi...

Hujui kuwa Jaji Ihema ndiye alieongoza tume ya Nchimbi kuhusu mauaji ya Mwangosi?
Hujui kuwa amesoma ripoti yake leo, pamoja na mambo mengne akidai
"NGUVU YA POLISI ILIYOTUMIKA KUTAWANYA WATU, HAIKUHUSIKA KUMUUA Mwangosi!"
Na kwamba hawawezi kutaja chanzo cha kifo, wataingilia mahakama!
Sasa ambacho hukuelewa ni nini ewe kichwa ngumu?

Hata ile kamati nyingine iliyoundwa na wanahabari wenyewe wamekiri katika ripoti yao kuwa tangu mwaka 2011 kulikuwa hakuna maelewano baina ya POLISI na wanahabari. sasa wanalalamika kwa nini wakati kumbe walikuwa wanafanya makusudi ili mradi tu POLISI ndiyo waonekane wabaya.
 
Ripoti imejaa usanii mtupu.Hivi hawana aibu kuitoa ripoti? Watanzania wa leo siyo wa Kudanganywa.

Mkuu pointi moja tu ya kuchukua ambayo hata ile tume ya wanahabari wenyewe imeseama ni kwamba kumbe muda mrefu kumekuwa na bifu baina ya POLISI na wanahabari mkoani Iringa. Hilo ndilo kubw ana la kufanyia kazi, Wandishi wa habari walijue hilo na Polisi nao walijue ili makosa yasijekujirudia tena. Kila upande ukiendekeza ubabe hakika hali itazidi kuwa mbaya.
 
lakini mkuu wew bila bakora utaelewa kweli kichwa jiwe, anyway hayo yametokea itv wakati huyo jaj mstaafu anasoma ripoti alikuwa anjiuma na hana amani wala confidence, inaonekana alichokuwa anakisema ni cha uongo

Huwezi kubadili hulka ya mtu. Jaji hakuwa akitetemeka wala nini bali ni jinsi anavyoongea kwa wale tunaomjua Jaji siku nyingi ndivyo anavyoongea, ni mtu wa kuongea taratibu na hana haraka wala papara, sasa kwa vile watanzania tumezoea kusikia wanasiasa wanapeta midomo kwa mbwembwe tusitegemee na hawa majaji kuongea kwa mbwembwe.
 
Nilishasema usitegemee kupata ukweli na haki kutoka serikali ya CCM hiyo sahau kabisa kwa yeyote anayetegemea kusikia ukweli kutoka kwenye serikali dahifu atasubiri sana na hatokaa asikie haki wala ukweli. Uongo na upotoshaji wa ukweli ndiyo sifa kuu ya serikali DHALIMU
 
Kwa kifupi,ripoti ya Tume/Kamati yake aliyoiongoza ni batili. Ni batili kwa sababu moja iliyo wazi. Hawakuzingatia hadidu za rejea. Jaji Ihema amezidi kujivua nguo. Iweje aseme sasa kuchunguza chanzo cha kifo cha Mwangosi ni kuingilia Mahakama? Kwanini asiseme siku alipokabidhiwa hadidu hizo? Jaji gani hajui hata kiini cha Tume/Kamati yake kuwa ni kujua nini hasa kilichosababisha kifo cha Mwangosi? Nani atamwamini na Ripoti yake ya kinafiki kama hii? Na arudishe posho zetu...aende akaisome kwa wana-CCM. Ujinga mtupu!
 
Anaeteua akiwa Njegele, unategemea anaeteuliwa aweje!? mbwa kala mbwa
 
Hujui kuwa Jaji Ihema ndiye alieongoza tume ya Nchimbi kuhusu mauaji ya Mwangosi?
Hujui kuwa amesoma ripoti yake leo, pamoja na mambo mengne akidai
"NGUVU YA POLISI ILIYOTUMIKA KUTAWANYA WATU, HAIKUHUSIKA KUMUUA Mwangosi!"
Na kwamba hawawezi kutaja chanzo cha kifo, wataingilia mahakama!
Sasa ambacho hukuelewa ni nini ewe kichwa ngumu?

Mkuu unapotoa habari, ueleweke siyo kila mmoja kaona hiyo taarifa. JF inasomwa hadi nje ya nchi hivyo brevity is very important
 
Kama angekuwa Mtu makini na Jaji mwadilifu, angejitoa mara baada ya Mh Lissu kuipinga hiyo Kamati na kumtuhumu huyo jaji professional
 
Uchunguzi wa tukio la uhalifu daima hufanywa na polisi na baadaye kupelekwa mahakamani kama ushahidi.
 
Mkuu unapotoa habari, ueleweke siyo kila mmoja kaona hiyo taarifa. JF inasomwa hadi nje ya nchi hivyo brevity is very important

Na unapokuwa hujaelewa, kuna namna ya kuuliza, sio kwa jinsi huyu "Kichwa ngumu" alivyofanya.
Pia, habari za Ripoti ya Ihema zimetapakaa humu tangu mchana, hivyo assumption ilikuwa ni kwamba wana JF wengi wanaelewa kinachoendelea.
 
Huyu jaji ni janga la kidunia, hivi hata huo ujaji wa kisanii alipewaje?? Hii nchi inatia aibu aisee...

Wanampa maujiko ya bure kamanda Lissu maana kwa jinsi nilivyomuona jaji Ihema leo chochote atakachosema Lissu kuhusu jambo lolote watu tutakuwa tunaamini tu
 
Kwa nini majaji wa Tanzania wamezoea kutumiwa na CCM kama ile mipira ya zinaa?
 
Huwezi kubadili hulka ya mtu. Jaji hakuwa akitetemeka wala nini bali ni jinsi anavyoongea kwa wale tunaomjua Jaji siku nyingi ndivyo anavyoongea, ni mtu wa kuongea taratibu na hana haraka wala papara, sasa kwa vile watanzania tumezoea kusikia wanasiasa wanapeta midomo kwa mbwembwe tusitegemee na hawa majaji kuongea kwa mbwembwe.
Nenda chooni naona umezidiwa vibaya na .......!
 
andika habari ieleweke usidhani kila mtu anaelewa kama unavyoielewa wewe.
dizain fluni habari yako haieleweki

Habari hautaweza kuielewa kama haujapitia ripoti ya kamati ya Nchimbi juu ya mauaji ya Mwangosi mtoa mada hajakosea report ni mbovu.
 
Yani ingekuwa nchi za wenzetu wapenda haki yani kesho nchimbi ange achia ngazi na kamati yake kuhukumiwa na wananchi,huu ni uhuni na watanzania tumezidi kudanganywa na pia kudanganyika na amani tuliyo nayo haya yote yanaletwa na aman iliyo kithili embu cku 2jalibu jambo likitokea la ajabu 2 anzishe chafuko moja la kuitishia amani nchi hii,utaona viongozi wetu watakavyo toa majibu magum kwa maswali magum.
 
Imani ya kuwa Mwangosi aliuawawa na Polisi ndiyo inafanya watu wasikubaline na ripoti. mimi naona wako sahihi. Tukumbuke kuwa ripoti hiyo ilijumuisha wanahabari wenyewe.
Kwa kuwa walikuwepo wanahabari ndani ya kamati, basi report ni sahihi? Thanx n may God bless you
 
Back
Top Bottom