Jaji Ihema, Kumbe Tundu Lissu alikuwa sahihi...

Msendekwa

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
442
168
Huyu jaji alitajwa na Lissu kuwa hajui kuandika hukumu, na alishawahi kulalamikiwa na Mzee Alute wa Singida.
Leo nimeamini, kwani ripoti kapika, kupika kwenyewe hajui, haijaiva, halafu akawa anatetemeka tu.
Kwanini Makunga asitoke na ripoti yake ili kujitenga na upotovu wa akina Ihema?
 
Nimemwangalia akisoma ripoti yake. Anaonekana haamini anachokisoma. Hivi mtu anayetakiwa kujiuzulu aunde tume halafu hiyo tume iwe na huru kweli na itoe taarifa bila upendeleo!! Kalaghabaho.
 
Hujui kuwa Jaji Ihema ndiye alieongoza tume ya Nchimbi kuhusu mauaji ya Mwangosi?
Hujui kuwa amesoma ripoti yake leo, pamoja na mambo mengne akidai
"NGUVU YA POLISI ILIYOTUMIKA KUTAWANYA WATU, HAIKUHUSIKA KUMUUA Mwangosi!"
Na kwamba hawawezi kutaja chanzo cha kifo, wataingilia mahakama!
Sasa ambacho hukuelewa ni nini ewe kichwa ngumu?
 
Hakuna Jaji pale wakati akisoma roho ilikuwa inamsuta hadi anatetemeka........hakika huu ni ujinga
 
andika habari ieleweke usidhani kila mtu anaelewa kama unavyoielewa wewe.
dizain fluni habari yako haieleweki

lakini mkuu wew bila bakora utaelewa kweli kichwa jiwe, anyway hayo yametokea itv wakati huyo jaj mstaafu anasoma ripoti alikuwa anjiuma na hana amani wala confidence, inaonekana alichokuwa anakisema ni cha uongo
 
sijaamini alichosema huyo jaji, eti nguvu ile ya polisi haikutumika kumuua marehemu, dah kweli mahakama zetu hazipo huru
 
lakini mkuu wew bila bakora utaelewa kweli kichwa jiwe, anyway hayo yametokea itv wakati huyo jaj mstaafu anasoma ripoti alikuwa anjiuma na hana amani wala confidence, inaonekana alichokuwa anakisema ni cha uongo

Bora hata umenisaidia, nilikuwa najiuliza nimuelezeeje bwana Kichwa ngumu, maana mambo haya yako wazi leo nzima, halafu eti yeye hajasikia na wala haelewi!
 
Kama huyu ndio aina ya Majaji tulionao, basi tumekwisha! Yaani kaenda kutumia mapendekezo ya Mkama kama ndio Mapendekezo ya kamati! Kweli hapo hamna kitu!
 
Hujui kuwa Jaji Ihema ndiye alieongoza tume ya Nchimbi kuhusu mauaji ya Mwangosi?
Hujui kuwa amesoma ripoti yake leo, pamoja na mambo mengne akidai
"NGUVU YA POLISI ILIYOTUMIKA KUTAWANYA WATU, HAIKUHUSIKA KUMUUA Mwangosi!"
Na kwamba hawawezi kutaja chanzo cha kifo, wataingilia mahakama!
Sasa ambacho hukuelewa ni nini ewe kichwa ngumu?

Hadidu za rejea za Dr Nchimbi kwa Tume yake hizi hapa:

1.Je nini chanzo cha Kifo cha Daudi Mwangosi?
2. Je ni kweli kwamba kuna uhasama kati ya waandishi wa habari mkoani Iringa na Jeshi la Polisi?
3. Je ni kweli kwamba kuna waandishi 3 walipanga kuuawa na jeshi la Polisi mkoani Iringa?
4. Je Ukubwa wa nguvu iliyotumika ulikua sahihi?
5. Je zipo taratibu zozote za vyama vya siasa kukata rufaa visiporidhika na maamuzi ya Jeshi la Polisi?
6. Je ni kweli kuna tatizo la mahusiano baina ya jeshi la polisi na vyama vya siasa?

Kama huyo Jaji alijua mambo ya kuingilia mahakama kwanini atafune kodi ya walala hoi?
 
kwa kweli nimesikitishwa saaaaana na na huyu jaji ihema, kweli njaa mbaya sana. kwa hili la ihema, hakyanani naiona kabisa Tanzania inayoingia kwenye machafuko. siamini kama hawa ndo watu tunaowategemea kutoa haki kwenye vyombo vyetu vya kisheria, na kama hakuna haki ni wazi watu watajichukulia sheria mkononi na amani itapotea. ni bora hata wangekaa kimya tuu kama walivyofanya kwa ulimboka. hivi ni kweli serikali ya ccm bado inafikiria kuwa watanzania hatuna akili kiasi hicho?????????
 
Nimeamini kuwa Tundu Lissu hakika ni mkweli.Yule kama ni kweli alikuwa Jaji basi mahakama zetu ni aibu isiyo bebeka.Nimesoma ripoti ya MCT iko wazi kabisa kuwa mauaji yale yalipangwa na Polisi sasa tume ya Jaji huyu inaongea upuuzi ambao hata walioona sura ya yule Jaji waliona inasema nini
 
Ripoti ya kamati ya jaji Ihema imejaa usanii kuliko ukweli.Je,wanamdanganya nani?
 
Jaji hana tatizo, hiyo ndio kula yake, ninayewashangaa tangu mwanzo ni nini hasa makunga alichokifuata? lakini utategemea aseme nini wakati yeye na kibanda wamefungwa midomo kwa kesi zilizoko mahakamani ndio maana sisi wengine tulimshangaa alivyokubali kuwemo kwenye tume badala ya kutangaza kwamba hawezi kwa sababu ana kesi, tatizo lao nao hao wakina makunga wanasubiria uDC, hata alipouawa mwenzao hawawezi kusema chochote, wanawaachia waandishi wa chini ndio waseme maana they have nothing to loose, hao MCT ni agency ya serikali yaani wanaoturudisha nyumba ni hao hao wanaojiita waandishi
 
Hujui kuwa Jaji Ihema ndiye alieongoza tume ya Nchimbi kuhusu mauaji ya Mwangosi?
Hujui kuwa amesoma ripoti yake leo, pamoja na mambo mengne akidai
"NGUVU YA POLISI ILIYOTUMIKA KUTAWANYA WATU, HAIKUHUSIKA KUMUUA Mwangosi!"
Na kwamba hawawezi kutaja chanzo cha kifo, wataingilia mahakama!
Sasa ambacho hukuelewa ni nini ewe kichwa ngumu?

Ambacho sijaelewa amesema, mwangosi aliuawa akiwa kazungukwa na askari wasiopungua saba! Hapo sawa. Pili kasema polisi hawahusiki na mauaji, !!! ()Mh! Sawa anyway!!! Halafu mtu mwingine simfahamu akasema mambo mengine hayakusemwa kwa sababu ya kisheria wasiingilie uhuru wa mahakama...!!! ( Sasa walichokuwa wanakifanya pale ni nini.) Nani kawatuma??? Yaani vichwa vyote vile pale vimeshindwa kutuambia muuwaji nani?? Ila wakati anakufa alikuwa kazungukwa na watu zaidi ya saba!! Hizo picha hawakuziona? Wauwaji si ndio wale !!! Wapeleke hizo picha shule za msingi wanafunzi wa point muuwaji pale. Na bosi wao alikuwapo pale naye hakuona muuwaji??
 
Ripoti imejaa usanii mtupu.Hivi hawana aibu kuitoa ripoti? Watanzania wa leo siyo wa Kudanganywa.
 
Huyu jaji alitajwa na Lissu kuwa hajui kuandika hukumu, na alishawahi kulalamikiwa na Mzee Alute wa Singida.
Leo nimeamini, kwani ripoti kapika, kupika kwenyewe hajui, haijaiva, halafu akawa anatetemeka tu.
Kwanini Makunga asitoke na ripoti yake ili kujitenga na upotovu wa akina Ihema?

Imani ya kuwa Mwangosi aliuawawa na Polisi ndiyo inafanya watu wasikubaline na ripoti. mimi naona wako sahihi. Tukumbuke kuwa ripoti hiyo ilijumuisha wanahabari wenyewe.
 
Back
Top Bottom