Je, ni sahihi kusema Tundu Lissu alitelekeza jimbo lake la Singida Mashariki?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,798
12,240
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amempongeza mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu akisema jimbo hilo lilikuwa limetelekezwa na Tundu Lissu.

Mtaturu amechaguliwa hivi karibuni kuwa mbunge wa Singida Mashariki kuchukua nafasi ya Lissu ambaye Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alitangaza kuwa amepoteza sifa za kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza leo Jumatatu Septemba 16, 2019 katika hafla ya uzinduzi wa rada za kuongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Rais Magufuli amewapongeza wajumbe wa kamati ya Bunge ya Miundombinu pamoja na mbunge huyo wa Singida Mashariki, aliyemtaka akawatetee wananchi bila kujali vyama.

“Nimefurahi kumuona hapa kwenye Kamati ya Miundombinu mbunge wa CUF (hakumtaja jina), lakini pia na mheshimiwa nani yule wa lililokuwa jimbo lililokuwa limetelekezwa. Ni jimbo gani hili.”
Huku akikuna kichwa Magufuli amesema, “Lilikuwa la Tundu Lissu ameshika huyu (huku akimnyooshea kidole Mtaturu).”
Ameongeza, “Safi kabisa hongereni mpigie makofi na ameingia na kazi nakuahidi Serikali yangu tutashughulikia maji katika jimbo hilo.”

Septemba 9, 2019 Mahakama Kuu ilikataa maombi ya Lissu kufungua shauri la maombi ya kutengua uamuzi wa Ndugai uliosababisha ubunge wake kukoma.

Ilisema mwanasheria mkuu huyo wa Chadema hakupaswa kuwasilisha maombi hayo, alitakiwa kufungua kesi ya kupinga uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo.
Akisoma uamuzi huo Jaji Sirillius Matupa amesema kama maombi yake yakikubaliwa yatasababisha uvunjaji wa katiba kwa kuwa italazimika kuwa na wabunge wawili kwenye jimbo moja.

Lissu alifungua maombi chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai ambaye amempa mamlaka ya kisheria kumwakilisha, ikiwa ni hatua ya awali kabisa ya kupigania kurudishiwa ubunge wake.
Katika maombi hayo namba 18 ya mwaka 2019, dhidi ya Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Lissu aliomba kibali cha kufungua shauri kupinga taarifa ya Spika ya kukoma kwa ubunge wake na mahakama iteunge taarifa hiyo.
Lissu yuko nchini Ubelgiji, kwa ajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu ambao hadi sasa hawajajulikana, tangu Septemba 7, 2017, aliposhambuliwa, katika makazi yake, jijini Dodoma akitokea bungeni.

Juni 28, 2019, wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge, Ndugai alitangaza kukoma kwa ubunge wa Lissu, huku alijitetea kuwa si yeye aliyemvua ubunge bali ni matakwa ya Katiba ya Nchi.

Alitaja sababu za uamuzi huo kuwa ni kutokuhudhuria vikao vya bunge kwa muda mrefu bila kumjulisha Spika kwa maandishi mahali aliko na kutokuja taarifa za mali na madeni kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Baada ya uamuzi huo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ilitangaza jimbo hilo kuwa wazi na Mtaturu kupita bila kupingwa baada ya washindani wake 12 kushindwa kurejesha fomu.

Source: Mwananchi
 
Nafikiri wale wote waliokuwa nyuma ya "conspiracy" ya Lissu wote wameweza kujitokeza wenyewe hadharani. Ila kanuni ni ile ile ya anguko lao;
1. Being used (by evil powers)
2. Being misused.
3. The being abused (what now follows)
4. Eventually being confused.

They wanted some, then they will get some.
 
Ee Mungu Baba, dhamira za mioyo yetu waijua hata kabla hatujasema.

Kwa ufupi, wewe ndiwe ulimponya mtumishi wako Tundu Lissu pamoja na shambulio lile kubwa sana lakutoa uhai hata wa tembo.

Hatujui makusudio yako yalikuwa ni nini, lakini Leo mwenye mamlaka ya kidunia ambayo wewe ndio uliruhusu ametamka hadharani kuwa Lissu amelitelekeza jimbo na sasa limepata mtu makini na yeye atapeleka maji ambayo hakuyapeleka siku zote.

Jee Baba Muumba ni kweli Lissu amelitelekeza Jimbo kama mtoro au ni mgonjwa? Wewe baba ndio unajua kila kitu, na sisi hatuna uwezo wa kumpigania Lissu kwani tukijitokeza hadharani TUMEKWISHA!

Wapo walikatazwa hata kumuona hospitali na wakafyata, wasivae T-shirt za get well soon walipobisha wakakumbana na vipigo na hata waliokusanyika kukuomba umponye Lissu acha kabisa! Ndio walijuwa kuwa kukuomba jambo wewe ni lazima huyo MTUKUFU lazima akubali kwani kwake yeye kwa nini tukuombe wewe na sio yeye ambaye ni ALFA NA OMEGA kwa sasa?
Sasa Baba shuka, baba shuka uvipigane vita hivi mwenyewe! Kwa nini unaruhusu tukupiganie mapenzi yako wakati unaweza kujipigania mwenyewe?

Huyu ni kiongozi wa wanyonge lakini wewe ni mfalme wa wafalme kwa nini utuachie vita vyako. Shuka Baba shuka uonyeshe wana Ikungi uko nao, Wanachadema uko nao na Wa Tanzania wanaoona nguvu zako zinaporwa nao pia watambue Baba umeshuka.

Twakuomba Utusikie. Amen
 
On a yote haya!
mdudechadema___B2dzfOhgag0___.jpeg
 
Sikuwepo kwenye huo mkutano lakini naweza kuwa na uhakika kuwa alishangiliwa sana. Hii inathibitisha upumbavu wa wengi wa wasaidizi wake na wananchi walio wengi.

Inasikitisha sana Rais kutoa matamko yanayostahiki mtu aliyerukwa na akili halafu watu wenye akili wanashangilia!
 
Ni kweli alilitelekeza muda sana. LISU kila siku alikuwa mahakamani kupambana na serikali na zaidi ya yote alishawaambia wananchi wasichangie chochote cha maendeleo. Makazi yake yalikuwa dar muda wote.
 
Mwl Nyerere alipenda sana kumwita Idd Amin Mwendawazimu!

Naona sasa tunajionea bayana uwendawazimu wa dikteta!! In kukosa aibu na kujitangaza waziwazi kwamba yeye ni muuuaji!

Tuna kazi kubwa!! Hili joka limefika hadi uvunguni linatutafuna bila haya huku baadhi ya wapumbavu wakilishangilia!!
 
Back
Top Bottom