Jaji amlazimisha Tundu Lissu kuingia kizimbani

Magamba bwana, wanawadharirisha tu majaji!!
Hebu tusubiri mazingaombwe mengine ya majaji kwenye kesi hii!
 
aitambue zanzibar kama sehemu ya muungano kwanza ndo tumuelewe , vingine8yo
Wewe mjinga nini kwani aliyekwamibia Lisu hatambui muungano ni nani? Lisu anachopigania muungano uwe na uwiano mzuri na uwanufaishe watu wa pande zote!

This is totally ****!
 
Naomba mnisaidie hapo kidogo yawezekana mie sijui hili; kwani nan anatakiwa kuanza kupanda kizimbani ni mtuhumiwa au shahidi?
(b)Ni nani anamamlaka ya kumpandisha shahidi kizimbani ili atoe ushahidi wake ni mtuhumiwa mwenyewe au muendesha mashtaka(Jaji)?

Nitashukuru nikipata majibu sahihi!!
 
hivi mtu akikuambia zanzibar siyo nchi ndani ya muungano, lakini ni nchi nje ya muungano ndiyo kajibu nini?
Zanzibar wana katiba, bendera na wimbo wao wa taifa.
Zanzibar ni nchi ndani ya muungano mazee!

Back to topic
asap
na tanganyika ni nchi nje ya muungano!?
 
Nadhani hakuna tatizo kwa Mdaiwa namba moja kuanza kujitetea. Ingawa imetokea kwamba yeye mwenyewe anajiwakilisha kwahiyo kuambiwa aanze kutoa utetezi inaonekana haijakaa vizuri kwa watu wengine lakini naona jaji amefanya jambo la msingi tu.
Tusubiri tu kusikia hao mashahidi wake watasema nini.
 
Tatizo ninaloliona, ni kwa mahakimu na majaji, na wao wamekuwa wana sihasa, kiasi kuwa wamesaidia kuidharirisha taaluma ya sheria.hawatoi hukumu ya kweli bali wanatoa hukumu ya kuwafurahisha watu fulani tena wachache kwa maslahi yao. Hii itavuruga utulivu uliopo sasa,Enyi wana sheria simamieni haki ya wanyonge ndipo mtakapofanikiwa katika kazi zenu,vinginevyo..................kwenu!!
 
na tanganyika ni nchi nje ya muungano!?

Tanganyika haina Bendera, haina Wimbo wa Taifa haina Katiba yaani ipo ipo tu.
Tanganyika siyo nchi ndani wala nje ya muungano.
Labda tuipiganie Tanganyika yetu ipate Uhuru wa kweli
 
Katika hali isiyo ya kawaida, jaji Moses Mzuna, anayesikiliza kesi ya kupinga matokeo ya Jimbo la Singida mashariki, leo asubuhi amemlazimisha mbunge wa Jimbo hilo, TUNDU LISSU- CHADEMA, apande Kizimbani. Awali baada ya kesi kuahirishwa jana, Tundu Lissu alisema atakuja na mashahidi wasiozidi watano. Hata hivyo asubuhi ya leo baada ya mahakama kuanza, Tundu Lissu alimwomba shahidi wake wa kwanza SHABAN HAMISI LYIMU kuingia kizimbani, lakini Jaji akakataa, na kumwamuru Tundu Lissu apande kizimbani.

maelezo ya awali ya Lissu ni haya,

Mimi naitwa Tundu Antiphace Mughwai Lissu,
Umri wangu kwa sasa ni miaka 44, nakaa Ikungi Singida, Dodoma na Dar es Salaam. Mimi ni Mbunge wa Jimbo la Singida mashariki, tangu siku matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa 31/10/2010. Vile vile mimi ni wakili wa mahakama kuu na mahakama zilizo chini yake kasoro mahakama ya Mwanzo. Vile vile Mimi ni Mwachama wa CHADEMA, tangu 2003, tangu wakati huo mimi ni mkurugenzi wa sheria, na katiba makao makuu DSM. Mimi pia ndio mnadhimu Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani, na waziri kivuli wa sheria na katiba. Niliwahi kuwa mwanachama wa CCM, katika miaka ile ambayo usipokuwa mwana CCM usingeruhusiwa kwenda Chuo Kikuu. Nililazimika kujiunga na CCM ili niweze kwenda Chuo kikuu. Niliacha kuwa mwananchama wa CCM siku niliposajiliwa kuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Septemba 1991, tangu baada ya hapo nimekuwa katika siasa za upinzani................ Tutaendelea kuwajuza yote yanayojiri........... Mashahidi wote watatu wapo, na Lissu anataka kukamilisha mashahidi wote leo
Jana pia mlituambia hivihivi kwamba mtaendelea kutujuza yatayokuwa yakijiri lakini wapi,.. Leo napo ni yaleyale.. ahadi bana daaah!!
 
Duuuh hii tamu sanaaa,kama awe anairudia rudia kila saa vile:)
Kesi za Uchaguzi: Hizi kesi lengo kubwa ni watu kupatiwa haki na kuondoa wasiwasi juu ya ushindi wa mbunge, diwani hata rais kama sheria zitaruhusu, hasa kwa kuangalia taratibu za uchaguzi kama zilizingatiwa ama la, maadili ya uongozi na yafananayo. Cha kushangaza katika kesi hizi ni kuwa majinmbo yanayochukuliwa na upinzani ndipo sheria na kanuni zinazingatiwa, ndipo mahakama ina pesa za kuharakisha kesi lakini majimbo yaliyoenda CCM kesi huchelewa na mara nyingine hupigwa danadana mpaka miaka 5 ikamilike angalia UBUNGO YA MNYIKA NA CHARLES KEENJA; Ukiangalia sasa kesi ya UBUNGO YA MNYIKA NA HAWA NG'HUMBI inaenda haraka, LEMA YA ARUSHA na LISSU YA SINGIDA. I can smell a rat somewhere.

ZANZIBAR NCHI SI NCHI: NCHI-country, maanake kipande cha ardhi yenye mipaka yake(TERRITORY) na kwa maana hiyo Zanzibar ni kipande cha ardhi(territory-country). Kuna DOLA-SOVEREIGN STATE ambayo Zanzibar haina vigezo vya kuwa dola huru lakini inaweza kuwa jimbo(state) ndani ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kama inavyoweza kuwa Tanzania Bara(REPUBLIC OF TANGANYIKA,1961-1964 April 26)

TATIZO LIKO WAPI KWENYE U-NCHI WA ZANZIBAR
KATIBA YA JM YA TANZANIA(1977): Inazungumzia JMT kama NCHI na si kama DOLA HURU uteuzi wa maneno ndilo tatizo hapa.Badala ya DOLA HURU inayojumuisha nchi mbili zilizokuwa huru.(KATIBA YA JMT-1977 IBARA YA 1)

MUUNDO WA MUUNGANO
SHIRIKISHO(federation) ya People's Republic of Zanzibar na Republic of Tanganyika ambapo baada ya Muuungano zingekuwa kama majimbo yenye tawala za ndani na tukawa na mambo machache ya msingi yanayoshughulikiwa kishirikisho ama muungano. Maanake tungekuwa na serikali tatu (Zanzibar, Tanganyika na Federation Republic of Tanzania; ama
MUUNGANO(Union) kati ya Zanzibar na Tanganyika na ambapo tungeondoa serikali za awali tukabaki na serikali moja tu ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

MFUMO POPO
Tuko kwenye mfumo upi kati hizi ZANZIBAR ina serikali ya ndani wakati Tanganyika ilikufa tukawa na Muungano,, kwa kukebehi mtu anaweza kusema kuwa ZANZIBAR ni kama KOLONI la TANGANYIKA iliyojivika vazi la MUUNGANO lakini wakawa wanapewa usemi mkubwa kuliko wa-BARA wenyewe.

NAWASILISHA.
 
nawashauri magamba kutambua nguvu ya uma ni mbaya.Raia mmoja mwenye hasira iliyojikusanya ni sawa na askari 1000.Wanapopambana na wapinzani wanatuongezea hasira.Watakuja juta
 
Back
Top Bottom