Jaji amlazimisha Tundu Lissu kuingia kizimbani

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Katika hali isiyo ya kawaida, jaji Moses Mzuna, anayesikiliza kesi ya kupinga matokeo ya Jimbo la Singida mashariki, leo asubuhi amemlazimisha mbunge wa Jimbo hilo, TUNDU LISSU- CHADEMA, apande Kizimbani. Awali baada ya kesi kuahirishwa jana, Tundu Lissu alisema atakuja na mashahidi wasiozidi watano. Hata hivyo asubuhi ya leo baada ya mahakama kuanza, Tundu Lissu alimwomba shahidi wake wa kwanza SHABAN HAMISI LYIMU kuingia kizimbani, lakini Jaji akakataa, na kumwamuru Tundu Lissu apande kizimbani.

maelezo ya awali ya Lissu ni haya,

Mimi naitwa Tundu Antiphace Mughwai Lissu,
Umri wangu kwa sasa ni miaka 44, nakaa Ikungi Singida, Dodoma na Dar es Salaam. Mimi ni Mbunge wa Jimbo la Singida mashariki, tangu siku matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa 31/10/2010. Vile vile mimi ni wakili wa mahakama kuu na mahakama zilizo chini yake kasoro mahakama ya Mwanzo. Vile vile Mimi ni Mwachama wa CHADEMA, tangu 2003, tangu wakati huo mimi ni mkurugenzi wa sheria, na katiba makao makuu DSM. Mimi pia ndio mnadhimu Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani, na waziri kivuli wa sheria na katiba. Niliwahi kuwa mwanachama wa CCM, katika miaka ile ambayo usipokuwa mwana CCM usingeruhusiwa kwenda Chuo Kikuu. Nililazimika kujiunga na CCM ili niweze kwenda Chuo kikuu. Niliacha kuwa mwananchama wa CCM siku niliposajiliwa kuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Septemba 1991, tangu baada ya hapo nimekuwa katika siasa za upinzani................ Tutaendelea kuwajuza yote yanayojiri........... Mashahidi wote watatu wapo, na Lissu anataka kukamilisha mashahidi wote leo
 
Inawezekana jaji alikuwa sahihi, kwani unapoanza kujitetea kabla ya kuleta mashahidi unaanza wewe, ndiyo maana jaji alimtaka tundu lissu kupanda kizimbani.
 
aitambue zanzibar kama sehemu ya muungano kwanza ndo tumuelewe , vingine8yo
 
Katika hali isiyo ya kawaida, jaji Moses Mzuna, anayesikiliza kesi ya kupinga matokeo ya Jimbo la Singida mashariki, leo asubuhi amemlazimisha mbunge wa Jimbo hilo, TUNDU LISSU- CHADEMA, apande Kizimbani. Awali baada ya kesi kuahirishwa jana, Tundu Lissu alisema atakuja na mashahidi wasiozidi watano. Hata hivyo asubuhi ya leo baada ya mahakama kuanza, Tundu Lissu alimwomba shahidi wake wa kwanza SHABAN HAMISI LYIMU kuingia kizimbani, lakini Jaji akakataa, na kumwamuru Tundu Lissu apande kizimbani.

maelezo ya awali ya Lissu ni haya,

Mimi naitwa Tundu Antiphace Mughwai Lissu,
Umri wangu kwa sasa ni miaka 44, nakaa Ikungi Singida, Dodoma na Dar es Salaam. Mimi ni Mbunge wa Jimbo la Singida mashariki, tangu siku matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa 31/10/2010. Vile vile mimi ni wakili wa mahakama kuu na mahakama zilizo chini yake kasoro mahakama ya Mwanzo. Vile vile Mimi ni Mwachama wa CHADEMA, tangu 2003, tangu wakati huo mimi ni mkurugenzi wa sheria, na katiba makao makuu DSM. Mimi pia ndio mnadhimu Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani, na waziri kivuli wa sheria na katiba. Niliwahi kuwa mwanachama wa CCM, katika miaka ile ambayo usipokuwa mwana CCM usingeruhusiwa kwenda Chuo Kikuu. Nililazimika kujiunga na CCM ili niweze kwenda Chuo kikuu. Niliacha kuwa mwananchama wa CCM siku niliposajiliwa kuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Septemba 1991, tangu baada ya hapo nimekuwa katika siasa za upinzani................ Tutaendelea kuwajuza yote yanayojiri........... Mashahidi wote watatu wapo, na Lissu anataka kukamilisha mashahidi wote leo

Hii nimeipenda.
Tanks Mkuu endelea kutupa updates
 
Yaani hii hali ya mabwanyenye wa CCM kukandamiza haki na demokrasia ina nikera sana mimi nimeanza kuwachukia kwa dhati wana CCM wote wakiwemo ndugu zangu na rafiki zangu, sina namna naona itakuwa hivyo hadi siku tutakapokomboa nchi yetu
 
Ccm wanataka wabunge wote wa chadema walio na kesi wafutiwe ubunge kwa sababu zao binafsi... Mbunge yeyote anasema kweli ccm wanamtafutia kesi... Kwa taarifa yenu kati ya watu ambao kikwete anawaogopa hapa nchini ni tundu lisu.... Akifuatiwa na john mnyika, g. Lema....
Hao jamaa wote wanatakiwa wavuliwe ubunge ili azma ya ccm itimie ili waweze kuiendesha nchi jinsi wakavyo waoooo...... Sasa ndipo nguvu ya umma inapoanza kufanya kazi na ccm watashindwa na hizo falsafa zao za kihuni zisizo na tija kwa taifa ...
Magamba chungeni saaaaaaaaaaana... Acheni kuchezea haki za watu... Hamjatuchagulia hao wabunge bali ni sisi wenyewe tumeamua kuwachagua ili tuweze kufanya kazi nao....
 
aitambue zanzibar kama sehemu ya muungano kwanza ndo tumuelewe , vingine8yo

Anaitambua, na wengineo tunaitambua. Si ni kama Manyarra na Kigoma tu? Tofauti huku kuna mkuu wa mkoa.sasa utambuzi gani unataka? au ule wa kuwa nchi huru ndani ya muungano?
:focus:
Jee, hili nalo linahusiana na hii kesi au yale yale ya Arusha (Mpango mzima??)
 
aitambue zanzibar kama sehemu ya muungano kwanza ndo tumuelewe , vingine8yo

Hivi Mtu akikuambia Zanzibar siyo nchi ndani ya Muungano, lakini ni Nchi nje ya Muungano ndiyo kajibu nini?
Zanzibar wana Katiba, Bendera na Wimbo wao wa taifa.
Zanzibar ni Nchi ndani ya Muungano mazee!

Back to topic
asap
 
Huyu Tundu Lissu atakuwa amebobea katika masomo ya JURISPRUDENCE na LEGAL METHODS. Vilevile akagusa kwenye CONTROVERSIAL AREAS IN HUMAN RIGHTS na PHILOSOPHICAL FOUNDATIONS OF HUMAN RIGHT. Nayasema hayo wakuu kutokana na huo utambulisho alioutoa.
 
Katika hali isiyo ya kawaida, jaji Moses Mzuna, anayesikiliza kesi ya kupinga matokeo ya Jimbo la Singida mashariki, leo asubuhi amemlazimisha mbunge wa Jimbo hilo, TUNDU LISSU- CHADEMA, apande Kizimbani. Awali baada ya kesi kuahirishwa jana, Tundu Lissu alisema atakuja na mashahidi wasiozidi watano. Hata hivyo asubuhi ya leo baada ya mahakama kuanza, Tundu Lissu alimwomba shahidi wake wa kwanza SHABAN HAMISI LYIMU kuingia kizimbani, lakini Jaji akakataa, na kumwamuru Tundu Lissu apande kizimbani.

maelezo ya awali ya Lissu ni haya,

Mimi naitwa Tundu Antiphace Mughwai Lissu,
Umri wangu kwa sasa ni miaka 44, nakaa Ikungi Singida, Dodoma na Dar es Salaam. Mimi ni Mbunge wa Jimbo la Singida mashariki, tangu siku matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa 31/10/2010. Vile vile mimi ni wakili wa mahakama kuu na mahakama zilizo chini yake kasoro mahakama ya Mwanzo. Vile vile Mimi ni Mwachama wa CHADEMA, tangu 2003, tangu wakati huo mimi ni mkurugenzi wa sheria, na katiba makao makuu DSM. Mimi pia ndio mnadhimu Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani, na waziri kivuli wa sheria na katiba. Niliwahi kuwa mwanachama wa CCM, katika miaka ile ambayo usipokuwa mwana CCM usingeruhusiwa kwenda Chuo Kikuu. Nililazimika kujiunga na CCM ili niweze kwenda Chuo kikuu. Niliacha kuwa mwananchama wa CCM siku niliposajiliwa kuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Septemba 1991, tangu baada ya hapo nimekuwa katika siasa za upinzani................ Tutaendelea kuwajuza yote yanayojiri........... Mashahidi wote watatu wapo, na Lissu anataka kukamilisha mashahidi wote leo

Duuuh hii tamu sanaaa,kama awe anairudia rudia kila saa vile:)
 
Back
Top Bottom