Jaji Aliyemhukumu Nguza, Hakana Tuhuma

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,620
1,777
Jaji Aliyemhukumu Nguza "Babu Seya" Akana Tuhuma Kuwa Alishinikizwa Na Kiongozi Mmoja Wa Serikali

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Thomas Mihayo, jana aliukana uvumi ulioenea kuwa, kiongozi mmoja mkubwa wa serikali aliwashinikiza majaji ili watoe hukumu ya kifungo cha maisha kwa mwanamuziki mashuhuri nchini, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na watoto wake.

1316170054.jpg

Nguza Viking "Babu Seya" na mwanae Papii Kocha Nguza (jezi ya bluu)
Jaji Mihayo alisema alitenga muda wa kuongea na watoto wasichana waliodaiwa kubakwa na Babu Seya na wanawe na akagundua kwamba watoto hao walikuwa wamelawitiwa na kwamba tendo hilo lilikuwa limefanywa kwa kipindi cha miezi kadhaa.

Alisema aliwasikiliza watoto hao na akapata picha kamili ya kilichoendelea katika matukio hayo na pia aligundua kwamba wazazi wa watoto hao hawakuwa wanajua mwenendo wa watoto wao.

Alifafanua kwamba baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vikitoa ripoti isiyo sahihi ya kesi hiyo na akasema kwamba kama waandishi wangefanya uandishi wa kiuchunguzi, wangeweza kupata ukweli wa tukio hilo, "Kibaya ni kwamba waandishi hawakulichunguza tukio hilo kiundani, vinginevyo wangeweza kupata ukweli wenyewe," alisema Jaji Mihayo.

Alisema uandishi wa kiuchunguzi unakosekana Tanzania na akawaomba wanachama wa vyombo vya habari nchini kusoma hiyo ripoti mpya ya ufuatiliaji wa vyombo vya habari vya magazeti iliyozinduliwa na MCT kwa nia ya kubaini mapungufu yao katika eneo la kuripoti habari za uchunguzi na kuyasahihisha.

Hivi sasa Babu Seya na mwanaye mmoja, wanatumikia kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kuwalawiti watoto wanafunzi wa kike. Washtakiwa wawili waliachiwa huru na Mahakama ya Rufani."Hakika si kweli… Niliupitia mwenendo wa kesi hiyo na kubaini kwamba kilichokuwa kinasemwa mitaani kilikuwa ni uvumi usiokuwa na chembe ya ukweli...," "Na cha kushangaza, vyombo vya habari vilikuwa vikiutangaza uvumi huu," alisema Jaji Mihayo alipokuwa akizindua rasmi Ripoti ya Ufuatiliaji wa Vyombo vya Habari vya magazeti (Julai 2010-Juni 2011) ya Baraza la Habari la Tanzania (MCT) jana jijini Dar es Salaam.

Jaji Mihayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya MCT, alisema aliusoma kwa kina mwenendo wa kesi ya kulawiti dhidi ya Babu Seya na wanawe kama ulivyoandaliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kabla ya kutoa hukumu ya mwisho.

Alisema kwa kuwa Mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kuamua kuhusiana na shauri hilo, ilipokea ukweli wa mwanzo wa shauri hilo na ikauwasilisha Mahakama Kuu, "Kwa kweli ni mimi ndiye nilikuwa mwenyekiti wa kesi hiyo kama Jaji wa Mahakama Kuu na ndiye niliyetoa hukumu ya mwisho (ya kumhukumu Babu Seya na wanaye kifungo cha maisha)," alisema.
3.jpg

Thomas Mihayo (photo: ismail.co.tz)

Alisema wakati akizisoma nyaraka na mwenendo wa kesi toka katika mahakama hiyo ya chini (Mahakama ya Kisutu), aligundua kwamba kilichokuwa kikisemwa na watu mitaani ulikuwa ni uvumi tu, "Si kweli kwamba kulikuwa na ofisa mmoja mkubwa katika duru za serikali ambaye alitoa shinikizo kwa Majaji lililowafanya wafikie kwenye tamati hiyo ya kumhukumu Babu Seya na wanaye kifungo cha maisha," alisema.

Mundu

JF-Expert Member
Sep 26, 2008
2,707
636
Tutajua ukweli tu siku moja..kama sio sisi basi watoto wetu watajua..na kama sio hao, basi ni watoto wa watoto wetu...

kama ndio hivyo, basi ile methali ya kiswahili isemayo "lisemwalo lipo......" ifutwe kabisa na haifai kutumika tena kwakuwa haina maana na inapotosha ukweli

Kibaya zaidi..mbona mwanzoni walifungwa watu wanne...na baada ya rufaa wamebaki wawili.... Hivi ni kwa sababu hakuna rufaa nyingine tena, ndio mana jaji huyu anaamua kusema anayo yasema?

Vin Diesel

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
9,083
6,334
Amenena sahihi kabisa...vyombo vya habari kushabikia vitu bila kuchunguza ni hatari kwa nchi...sekta ya habari imevamiwa na makanjanja sana.

king kong

Senior Member
Aug 25, 2011
106
12
ukweli upo siku ukija basi kiongozi huyo yeye ataenda kimoja gerezani. Huu si utu ku fremiana kifungo cha maisha bora miaka ijulikane mtu awe na matumaini

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
45,228
100,027
Amenena sahihi kabisa...vyombo vya habari kushabikia vitu bila kuchunguza ni hatari kwa nchi...sekta ya habari imevamiwa na makanjanja sana.
pamoja na ukweli huo na hayo mengine nayo yana ka ukweli!. Jee unayajua na ya Liyumba?. Jee unamjua aliyemchongea kuwa anaongea na simu akiwa gerezani unamjua ni nani?. Wee subiri hiyo hukumu ya kukutwa na simu gerezani ndipo utaielewa vizuri hiyo framing!.

Wabogojo

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
354
87
Acheni kuingilia uhuru wa mahakama bana

Uhuru usipotumiwa vema matokeo yake ndiyo haya. Uhuru wa kweli ni ule wenye kutenda haki kwa wote na siyo kwa matabaka ya wachache tu, ndiyo maana jamii inakuwa na mashaka na hivi vyombo vyetu vya utawala.

Nsiande

JF-Expert Member
Jul 27, 2009
1,649
860
Mimi nina watoto wadogo kama kweli walilawiti kisheria walitakiwa kwenda jela miaka 30 na adhabu ngumu au hiyo ya kufungwa maisha,

lakini ningeshauri kuwe na investigative journalism, kuna story nilisoma ya John Grisham inayoitwa 'The Innocent Man' huyu mtu alikuwa kwenye deathrow na bahati nzuri kesi yake ikaweza kuwa reviewed na akajulikana hakufanya mauaji, hii ni based on true story, kungekuwa na NGO ambayo ni independent au a govt institution ambayo inaangalia mwenendo wa controversial cases kwa kwenda ndani na kuhoji parents, school teachers,friends of those kids,neighbours, kuchanganua mwenendo mzima wa case etc, kuangalia doctor's reports ( if they get access ) etc etc

Justice may be blind but it can see in the dark

utantambua

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,367
319
Huko marekani taasisi ya innocence project (kama nimeipatia spelling) imewezesha watu kibao kuachiwa huru ambao walihukumiwa kimakosa baada ya DNA ama baada ya kupitia inconsistencies kibao ktk ushahidi, pia tizama kipande kinaitwa struggle for justice ktk dstv ni channel ya crime and investigation utaona jinsi gani watu innocent walivoishia magerezani ama hata ktk death row

Pax

JF-Expert Member
May 3, 2009
268
87
Huko marekani taasisi ya innocence project (kama nimeipatia spelling) imewezesha watu kibao kuachiwa huru ambao walihukumiwa kimakosa baada ya DNA ama baada ya kupitia inconsistencies kibao ktk ushahidi, pia tizama kipande kinaitwa struggle for justice ktk dstv ni channel ya crime and investigation utaona jinsi gani watu innocent walivoishia magerezani ama hata ktk death row

Nakuunga mkono, Jaji kusema alienda kuzungumza na watoto na kupitia mafaili sio evidence, atuambie wazi wazi ni evidence gani zilitumika na kwenye maswala kama haya DNA test is the last resort, less than that tunadanganyana tu. Na nchi masikini kama ya kwetu framing is the likely posibility.

utantambua

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,367
319
Nakuunga mkono, Jaji kusema alienda kuzungumza na watoto na kupitia mafaili sio evidence, atuambie wazi wazi ni evidence gani zilitumika na kwenye maswala kama haya DNA test is the last resort, less than that tunadanganyana tu. Na nchi masikini kama ya kwetu framing is the likely posibility.

Mkuu umepiga kwenye point haswaaa. Kusikiliza maelezo ya mtu kumbuka kuna suala la emotions ambazo zinawezakukuteka na kujikuta unaegemea upande flani. Nadhani kuwa jaji hakuondoi fact kua naye ana emotions.

Nsiande

JF-Expert Member
Jul 27, 2009
1,649
860
Huko marekani taasisi ya innocence project (kama nimeipatia spelling) imewezesha watu kibao kuachiwa huru ambao walihukumiwa kimakosa baada ya DNA ama baada ya kupitia inconsistencies kibao ktk ushahidi, pia tizama kipande kinaitwa struggle for justice ktk dstv ni channel ya crime and investigation utaona jinsi gani watu innocent walivoishia magerezani ama hata ktk death row

Yes kilichowasaidia kupata aqcuital(sp) ni hiyo innocence project

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,938
1,427
Mi mtazamao wangu nana k una mambo ambayo watu wanamtetea babu seya hawaelewi au wanaelewa nusu tu.

Inawezekana kweli babu seya alimess na mtu fulani mkubwa ---- Hilo na mimi nasema inawezekana

Lakini inawezekana i uwa babu seya alikuwa anawalawiti watoto- Hilo nasema pia inawezekana

Kasoro na tatizo kwenye jamii yetu
Kasoro kubwa inaweza kuwa kwa nini ouvu wa babu seya umejulikana na umefkishwa mbele ya ya vyombo husika baada ya mtu fulani mkubwa kuigiliwa anga zake....Na kwa nini ilichukua mudaSasa watu watakuwa wanafanya makosa kama wanaangalia tu upande mmoja wa kwamba kilichofanya babu seya afikishwe mbele ya mkono wa sheria ni kumess na mkubwa . Ina maana asingemess na mkubw leo hii vitoto kibao zaiid vingekuwa vimeshaharibiwa na wala tusingejua.

Na hii sio kwa babu seya tu ndio system zetu zinavyofanya kazi sehemu nyingi. Watakuacha ufanye makosa wanakutazama na wanapata detail lakini siku ukionekana unakuwa tishio zaidi ndio unaibuliwa yale makosa amabyo ni kweli uliyatenda.kama hawajui basi zitatafutwa kashfa zako zote za kweli ili zianze kushgulikiwa.
Nchi nyingine wazazi na hata hao watto walitakiwa waishataki serikali na kulipwa fidia kwa kushindwa kuwalinda watoto wa na vitendo hivyo kuendelea kufanyika kwa muda bila vyombo husika kubaini.

La sivyo ndio maana watu wataendela kusema wametumia kivuli cha makosa ya kweli aliyofaya babu sema kumuhukumu kwa kitendo amabcho sio kosa lakini hakikumfurahisha mkubwa fulani.

Sasa tujiulize kuna kina babu seya wangapi ambao hawatashikwa sababu tu hawatamess na class A citzen

Mtanzania haswa

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
663
98
natumaini hao watoto washakua wakubwa sasa, nikikutana na mmoja wao natongoza akikubali tukiwa katikati ya majambozi nitamuuliza kama alifanywa na nguza na babake, hapo nitajua ukweli na nitawamwagia data

0 Reactions
Reply
Top Bottom