Jairo la Kuvunda halina ubani

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,831
Luhanjo 'aliboronga' kumsafisha Jairo
KATIBU Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo ama hakujua au alifanya makusudi kumsafisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo katika kashfa ya kuzichangisha fedha taasisi za wizara hiyo, kwa sababu Serikali ilishatoa waraka kuzuia utaratibu huo.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Khijjah alitoa waraka maalumu kwa makatibu wakuu wa wizara zote unaowazuia kuchangisha au kupokea fedha kutoka taasisi zilizo chini yake kwa sababu yeyote ile.

Waraka huo namba 3 wa Machi 7, mwaka huu, wenye kumbukumbu namba TYC/A/400/620/18, unaonyesha kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kuonekana kwamba baadhi ya mashirika na taasisi za umma zinatoa ruzuku au mikopo kwa wizara, bila kuzingatia taratibu na sheria. Kwa mujibu wa waraka huo, makatibu wakuu wa wizara, wakuu wa mashirika na taasisi za umma watakaoshindwa kuzingatia agizo hilo, watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni na taratibu zilizowekwa.

“Kwa kuzingatia misingi hiyo, Wizara haipaswi kupewa fedha za ziada kupitia mashirika na taasisi zilizo chini yake,” unaeleza waraka huo ambao Mwananchi imeuona. Waraka huo unazidi kueleza: “Endapo kutatokea mahitaji yatakayolazimu Wizara kuzichangisha fedha taasisi zilizo chini yake, mashirika au taasisi za umma, lazima ipate kibali cha Waziri wa Fedha baada ya kushauriwa na Mlipaji Mkuu wa Serikali (PMG) na Msajili wa Hazina kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2008.” inaaminika kuwa Luhanjo na Jairo wanaujua waraka huo kwa sababu nakala zake zilitumwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhani Khijjah hakutaka kuzungumzia waraka huo kwa madai kwamba amekuwa nje ya ofisi kwa muda mrefu. Alishauri mwandishi awasiliane na Msemaji wa Wizara ya Fedha na Uchumi au Kamishna wa Bajeti.
“Sikiliza ndugu yangu, mimi kwa sasa ni mgonjwa, nimekuwa nje ya ofisi kwa muda mrefu, hebu mtafute PR (Ofisa Uhusiano) au Kamishna wa Bajeti ndiyo wanaohusika na mambo hayo ni muda mrefu sasa sina kumbukumbu nzuri,” alisema Khijjah.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovic Utouh alipotakiwa kueleza kama katika uchunguzi wake dhidi ya Jairo walifahamu uwepo wa waraka huo, alisema asingeweza kusema chochote sasa kwa kuwa suala hilo sasa lipo mikononi mwa Kamati Teule ya Bunge.

“Mimi nakushauri upige simu huko ilipotoka barua hiyo, huenda tulipata au hatukupata hiyo haisaidii kwa sasa kwani kumeshaundwa Kamati Teule ya Bunge kufuatilia jambo hilo,” alisema Utouh na kuongeza: “Sitaki kuonekana naingilia kazi ya Kamati.”

Luhanjo hakutaka kuzungumzia suala hilo akisema: "Sipo tayari kujibu swali lako katika mazingira haya, elewa kijana!" Jairo hakupatikana kuzungumzia suala hilo kutokana na simu yake ya mkononi kuita bila ya kupokewa.

Taarifa za kuwapo kwa waraka huo zimepatikana wakati Bunge limeunda Kamati Teule kuchunguza utaratibu uliotumiwa na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa kupitisha wa bajeti.
Julai 18 mwaka huu, Jairo alituhumiwa bungeni kwamba amezichangisha fedha taasisi zilizoko chini ya wizara yake kwa ajili ya kupitisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/2012.

Tuhuma hizo zilitolewa na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo alipokuwa akichangia Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa na Waziri William Ngeleja.

Tuhuma nyingine zilizokuwa zimetolewa na Shellukindo ni za kulipa masurufu ya safari za watumishi walio chini ya wizara hiyo na taasisi zake, ambao tayari walikwishalipwa na wizara na taasisi zenyewe.Tuhuma hizo zilimfanya Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo kumpa Jairo likizo ya malipo ili kupisha uchunguzi ambao ulifanywa na Ofisi ya CAG ambao katika taarifa yake, haukuthibitisha madai hayo hivyo Jairo kurejeshwa kazini Agosti 23, mwaka huu.

Kamati ya Bunge ya kuchunguza sakata ya Jairo, ni ya pili kuundwa wakati wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, zote zikiwa kwa wizara hiyohiyo ya Nishati na Madini.

Februari 7, 2008 aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na waliowahi kuwa mawaziri wa Nishati na Madini, Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi walilazimika kujiuzulu baada ya kutajwa katika ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza mkataba tata wa Kampuni ya Kufua Umeme wa Dharura ya Richmond. Kamati hiyo iliongozwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Dk Harrison Mwakyembe. Dk Mwakyembe sasa ni Naibu waziri wa Ujenzi.

Agosti 25, mwaka huu Spika wa Bunge, Anne Makinda alitangaza majina ya wabunge watano, wanaounda Kamati Teule kumchunguza Jairo. Walioteuliwa ni Injinia Ramo Makani Matala, Gosbert Blandes, Mchungaji Yohane Israel Natse, Khalifa Suleiman Khalifa na Martha Umbulla.

Mwananchi
 
Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
Hapo kwenye Red ni Msumari wa moto kwa Fisadi Jairo na hakuna adui mkubwa kwake kama Mzee Luhanjo ambaye alikua na huu waraka kwenye mi-faili zake pale ikulu lakini bado tu akaendelea kumfunga kamba mwenzake bila huruma.

Wananchi bado tunaendelea kufuatilia kwa karibu sana sakata hili hadi kujulikane hizo fedha ziliko na kwa faida ya nani.

Luhanjo 'aliboronga' kumsafisha Jairo
KATIBU Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo ama hakujua au alifanya makusudi kumsafisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo katika kashfa ya kuzichangisha fedha taasisi za wizara hiyo, kwa sababu Serikali ilishatoa waraka kuzuia utaratibu huo.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Khijjah alitoa waraka maalumu kwa makatibu wakuu wa wizara zote unaowazuia kuchangisha au kupokea fedha kutoka taasisi zilizo chini yake kwa sababu yeyote ile.

Waraka huo namba 3 wa Machi 7, mwaka huu, wenye kumbukumbu namba TYC/A/400/620/18, unaonyesha kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kuonekana kwamba baadhi ya mashirika na taasisi za umma zinatoa ruzuku au mikopo kwa wizara, bila kuzingatia taratibu na sheria. Kwa mujibu wa waraka huo, makatibu wakuu wa wizara, wakuu wa mashirika na taasisi za umma watakaoshindwa kuzingatia agizo hilo, watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni na taratibu zilizowekwa.

Mwananchi
 
kaly

Member
Aug 6, 2011
63
3
Kamati iliyoundwa ifanye kazi vizuri ili ije na matokeo yenye tija. Luhanjo alikurupika ngoja tusubiri kamati.
 
kilemi

JF-Expert Member
Mar 13, 2009
544
98
Duh, siasa ni balaa! Huyu CAG heshima zote alizojizolea wakati akiwa pale NBAA ameamua kuziuza kwa wanasiasa. Au anataka kugombea ubunge? Kama huo waraka anao na akashindwa kuufanyia kazi atakuwa ameidhalilisha taaluma yake kwa kiasi kikubwa.
 
taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,087
526
Duh, siasa ni balaa! Huyu CAG heshima zote alizojizolea wakati akiwa pale NBAA ameamua kuziuza kwa wanasiasa. Au anataka kugombea ubunge? Kama huo waraka anao na akashindwa kuufanyia kazi atakuwa ameidhalilisha taaluma yake kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotumika sasa (Kifungu cha 144 (6)), suala la CAG kugombea ubunge haliwezekani.
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,998
1,156
Duh, siasa ni balaa! Huyu CAG heshima zote alizojizolea wakati akiwa pale NBAA ameamua kuziuza kwa wanasiasa. Au anataka kugombea ubunge? Kama huo waraka anao na akashindwa kuufanyia kazi atakuwa ameidhalilisha taaluma yake kwa kiasi kikubwa.
Kwa mtazamo wangu mimi, huyu CAG ndo ana aibu na mzigo mkubwa wa fedheha wa kubeba katika sakata hili kuliko LUhanjo. yeye CAG ndiye aliyefanya uchunguzi ulioonyesha kuwa jairo hakuna na matatizo. Inawezekana kuwa alifanya hivyo kwa kufuata maelekezo ya Luihanjo, lakini huo ni mzigo mwingine kwake. kama mtaalamu, hapaswi kufanya kazi kwa kufuata maelekezo ya wakubwa.
 
Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
408
Kamati iliyoundwa ifanye kazi vizuri ili ije na matokeo yenye tija. Luhanjo alikurupika ngoja tusubiri kamati.
Huyu mzee Luhanjo kila siku huwa najiuliza hivi yeye utumishi wake hauna ukomo? Maana sitaki kuamini kuwa eti hajafikia umri wa kustaafu hata kidogo!!!! Hawa ndio watu wanaotaka kuendesha mambo kwa akili zao zilizochoka kama wao wenyewe!!
 
Daniel Anderson

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
872
140
Ngoma sasa imefika patamu. Luhanjo ni mdogo katika hili, simuweki CAG kabisa, huyu ndo mdogo kabisa.
Ukifuatilia hili suala utaona kuwa mkuu wa nchi amehusika zaidi na pengine hawa walikuwa wanatekeleza maagizo ya jk.
Hebu kumbuka PM alivyojibu mara ya kwanza tuhuma hizi bungeni, alikuwa tayari kumtoa jairo on the spot kutoka ofisini. Akasema anamngoja rais na rais akakataza kuchukuliwa maamuzi YOYOTE mpaka arudi.
CAG akapewa kazi ya kuchunguza hili, (kwa maelekezo maalumu) akatekeleza wajibu wake. Ninaimani kuwa hata rais alipewa majibu ya ripoti hiy6 kabla luhanjo hajaisoma kwa media.
Baada ya kuona moto wa wabunge akaamuru jairo apumzike.
Kwanza hata sabubu za serikali kumpumziisha hakuma! Walimpumzisha awali kupisha uchunguzi, ukakamilika, wakajiridhisha hakuna kanuni iliyovunjwa, wakamrudisha.
Ukweli ni kuwa jk anajua wanachokifanya katika mchezo huu, na yeye ndiye aliyepaswa kuchunguzwa.
 
kilemi

JF-Expert Member
Mar 13, 2009
544
98
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotumika sasa (Kifungu cha 144 (6)), suala la CAG kugombea ubunge haliwezekani.
Sasa kama hahitaji siasa, ilikuwepo haja ya kufuatana nao kwenye kazi zake? Lakini tusijadili sana magazeti, hebu tusubiri riport ya tume!!
 
Bobby

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
2,182
1,871
Duh, siasa ni balaa! Huyu CAG heshima zote alizojizolea wakati akiwa pale NBAA ameamua kuziuza kwa wanasiasa. Au anataka kugombea ubunge? Kama huo waraka anao na akashindwa kuufanyia kazi atakuwa ameidhalilisha taaluma yake kwa kiasi kikubwa.

Kilemi mimi sishituki nikiona madudu anayofanya mzee wa watu CAG kwani niliyatarajia kulingana na aina ya serikali tulinayo. Infact mimi nilishtushwa tu siku alipokubali uteuzi wa CAG kwani nilijuwa fika kwamba Utoah tuliyekuwa tunayemfahamu wa NBAA hawezi kuwa the same Utoah kama CAG. Haiwezekani narudia tena HAIWEZEKANI MILELE NA MILELE ukatunza jina (to keep your name) kwenye fani na still ukawa mtumishi wa serikali ya Kikwete-this is completely impossible. So siku niliposikia amekubali uteuzi nikajua kwenye fani ya uhasibu/ukaguzi tumempoteza gwiji kwa kuwa kilichokuwa kikifuata sasa ni sanaa kwa kwenda mbele, mojawapo ni hii ya juzi ya jairo ambayo inathibitisha tu yale niliyotarajia.
 
Kamura

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
491
47
Huku ni kuingilia uhuru wa Tume huru iliyoundwa kuchunguza suala hili. Hatujapata matokeo ya Tume, magazeti tayari yamehukumu.
 
ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,721
6,466
hapo kwenye red ni msumari wa moto kwa fisadi jairo na hakuna adui mkubwa kwake kama mzee luhanjo ambaye alikua na huu waraka kwenye mi-faili zake pale ikulu lakini bado tu akaendelea kumfunga kamba mwenzake bila huruma.

Wananchi bado tunaendelea kufuatilia kwa karibu sana sakata hili hadi kujulikane hizo fedha ziliko na kwa faida ya nani.

hata jairo anao ofisini kwake, ni makusudi tu. Walijua hawatagundulika. Na kilichomponza jairo, ni kuwatukana wabunge wa ccm eti ni sawa na comedy kwa kutokuwa na msimamo.
 
ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,721
6,466
huku ni kuingilia uhuru wa tume huru iliyoundwa kuchunguza suala hili. Hatujapata matokeo ya tume, magazeti tayari yamehukumu.

yamehukumu nini na wewe *****? Kutuhabarisha juu ya waraka huo unaokataza wizara kuchangachisha fedha idara zilizochini yake ni vibaya.
 
HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
Kama kweli kuna huu waraka basi Luhanjo, Utouh na Jairo wote wanatakiwa kuwajibika.

Jairo anatakiwa kuwajibika kwa sababu alikiuka waraka halali wa serikali ulikuwa umetolewa na mamlaka halali inayosimamia fedha za serikali.
Utouh anatakiwa kuwajibika kwa sababu hakuwa makini katika utendaji wake wa kazi. Yeye kama mkaguzi mkuu wa serikali alitakiwa kujua kanuni na mashariti ya kutumia fedha zote za serikali. Na kama hajui hizo kanuni na masharti basi hajuia kazi yake na hivyo basi hana uwezo wa kusimamia hiyo ofisi yake.

Luhanjo anatakiwa kuwajibika kwa sababu yeye kama katibu mkuu kiongozi anatakiwa kujua uwepo wa huo waraka. Na anatakiwa kusimamia kanuni na taributi za ofisi kama zinaelekezwa na mamlaka husika.

Pia katibu wa fedha atakuwa hajatenda haki kwa watanzania katika suala hili kwa sababu ya kukaa kimya muda wote hali akijua kuwa kuna waraka wa wizara yake unakataza hicho alichofanya Jairo. Kulikuwa hakuna haja ya kutumia fedha nyingi kuchunguza hili jambo na kulijadili kama Katibu wa wizara ya fedha anangejitokeza mapema na kusema alichokuwa amefanya Jairo ni ukiukaji wa waraka halali wa wizara ya fedha na hivyo basi alitakuwa kuwajibishwa.
 
Kamura

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
491
47
yamehukumu nini na wewe *****? Kutuhabarisha juu ya waraka huo unaokataza wizara kuchangachisha fedha idara zilizochini yake ni vibaya.

Kwani waraka huo haukuwapo (tangu Machi 18, 2011) mpaka ikaundwa Tume ya kumchunguza Jairo ndio uibuliwe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom