Sekretarieti ya Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA imewasilisha waraka Maalumu kwa Kamati kuu ya Chama hicho ya kutokuwa na imani na Katibu Mkuu wa CHAUMMA na mgombea Urais wa Chama hicho katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 Salum Mwalimu.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata kwenye chumba chetu cha habari Royal Tv leo Jumatatu Juni 29, 2026, kutoka kwa chanzo chetu cha uhakika ndani ya Kikao hicho cha kamati kuu, miongoni mwa wajumbe na viongozi wa Sekretarieti ya CHAUMMA taifa waliosaini waraka huo ni pamoja na Benson Kigaila, Edward Kinabo, Ismail Kangeta na Elia Gregory Mahwa.
Wengine waliosaini waraka huo kupitia kwenye Kikao hicho kinachoendelea muda huu Makao Makuu ya CHAUMMA, Kinondoni Jijini Dar Es Salaam ni Aisha Madoga, David Chiduo, Dorcas Mpatili na Mohamed Pume.
Miongoni mwa yale yaliyotajwa katika waraka huo wa kutokuwa na imani na Salum Mwalimu ni pamoja na kutokuwa muwazi katika mapato na matumizi ya Chama kufanya ubadhirifu wa fedha za chama, kubadilisha msimamo wa Chama kwa utashi na matakwa yake binafsi na kushindwa kuheshimu uongozi na kuendesha chama mithili ya mali yake binafsi.