EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
KATIBU Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo anadaiwa kuwakashfu wabunge kwa kuwafananisha na wasanii wa maigizo wa kikundi cha The Original Comedy. Jairo anadaiwa kutoa maneno hayo juzi nje ya ukumbi wa Bunge muda mfupi baada ya Bunge kuahirishwa na wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenda katika kikao chao kabla ya mjadala wa bajeti kuahirishwa juzi jioni.
Chanzo chetu cha habari kilichokuwa ndani ya kikao hicho cha wabunge wa CCM kiliiambia MTANZANIA juzi kuwa madai ya kashfa hiyo yaliwekwa wazi na Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaha alipokuwa akichangia mada katika kikao hicho. Kwa mujibu wa chanzo hicho, Jairo alitoa lugha hiyo iliyoonekana kuwaudhi wabunge wa CCM baada ya kukutana na Shaha nje ya ukumbi wa Bunge.
"Tulipokuwa katika kikao chetu hali ilikuwa mbaya kwa sababu wabunge walikuwa wakitoa madukuduku yao kuhusu hali ilivyokuwa juu ya hiyo bajeti iliyokwamishwa. Wakati tunajadili, Shaha alisimama na kueleza jinsi Serikali inavyotakiwa kufanya kukabiliana na huu mgawo wa umeme ambako alipendekeza inunuliwe mitambo haraka iwezekanavyo na Jairo achukuliwe hatua za haraka kwa kuondolewa katika nafasi yake. Pamoja na maelezo mengi aliyosema, alituambia kuwa wakati wabunge tumetoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya Bunge kuahirishwa, alikutana na Jairo, wakazungumza kisha akamwambia sisi wabunge ni kama ‘comedy' hatumfanyi kitu hata tukifanyaje.
Aliposema hivyo, wabunge wakalipuka kwa hasira wakasema lazima huyu ang'oke kwa sababu anaonekana kuwa na kiburi kwa kuwa anateuliwa na Rais. Kauli hiyo ya Shaha ikaungwa mkono na Mbunge wa Shinyanya Mjini, Stephen Masele ambaye alipigilia msumari na kusema alichosema Shaha ni kweli kwa kuwa hata yeye alimsikia. Inaonekana kauli hiyo ya Shaha ilimshangaza Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa kikao kwani aliuliza, ni kweli amesema hivyo?, ‘Shaha akasema ni kweli, ‘I swear' (naapa) aliniambia," kilisema chanzo chetu.
http://www.newhabari.com/2011/07/20/jairo-kashfa-nyingine/