Jairo ajiuzulu wadhifa wake

Jairo ajiuzulu wadhifa wake

Status
Not open for further replies.
Habari kutoka Dodoma zinaarifu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini amejiuzuru Rasmi wadhifa huo

More to follow

hiyo haitoshi inabidi na Boss wake na naibu wake wafuate mkondo coz hakuwa anaact bila kuwataarifu maboss wake waliomuweka hapo. kumstaafisha huyu 2 akutoshi huu uozo utaendelea katika wizara na Taasisi nyingine za hii Serikali legelege tuliyonayo.
 
Mimi nilifikiri atafukuzwa kazi, sasa kujiuzulu maanake nini? Jana Lema kaomba Ngeleja na Malima wawajibike, Makinda kawatetea, sasa kama Jairo kajiuzulu wao wanasubiri nini? Na Waziri Mkuu anasubiri nini? Na pia JK anasubiri nini kujiuzulu na kuitisha uchaguzi mkuu? Hii kupitisha bajeti kwa rushwa haiwezi fanyika bila baraka za JK bwana!!!
 
HAkuna aliyejiuzulu, anasubiriwa Mk.were aje atoe maamuzi! Hili linchi linakera sana
 
one side:Mheshimiwa huyu jamaa kaharibu mambo,kuna m-mbeya mmoja kakamata barua yake na ameisoma bungeni imebidi nilazimike kuondoa bajeti ya ile wizara bungeni,...other side😀ah sasa itakuaje bana?kwanini hamkumpa cash ya kutosha lakini hadi akatoka kusema?one side:naona umfukuze tu kazi bana au unasemaje maana waheshimiwa ndivo walivo komaa eti, tena mbaya zaidi hadi wa upande wetu sijui wamekunywa juice nyekundu+nyeupe+nyeusi??!!!!other side:aiseee,ntaweza kweli?au mwambie tu aandike baru ya kujiuzuru ili apate malupu lupu yake aondoke, kafanya kosa mwenyewe hakua makini kama wengine!!one side:eti eh?ila kweli ukimfukuza atatoa siri zetu nyingi maana naona kuna mashushushu wengi kweli tusio wajua,kama vipi ngoja niongee nae fasta!!!
tehe tehe tehe....!nimeyapenda mazungumzo yao!! Kikwete(VASCO DAGAMA) hajui kujengea heshima,ataendelea kuonekana dhaifu wa maamuzi siku zote za maisha yake! Chance kama hii ili kuwa turning point ya kuonyesha kwamba WAKIFANYA uzembe kamaa huo hawaachi! KWELI KUNGURU HAFUGIKI!!
 
Hivi "Source" maana yake ni nini???

Kama Ghost Ryder ni msaidizi wa Jairo na akamtuma kupeleka hiyo barua "source" atakuwa nani???
 
Hivi "Source" maana yake ni nini???Kama Ghost Ryder ni msaidizi wa Jairo na akamtuma kupeleka hiyo barua "source" atakuwa nani???
True usemayo mkuu,then huyu Ghost akipost habari zake niza ukweli
 
Pinda kakanusha anasema labda jairo kaipeleka hiyo barua kwenye vyombo vya habari lakini sio kwake hivo anamsubiria JK Atue bongo kutoka kwa madiba ndio ataamua ila yeye na ofisi yake hana taarifa yeyote TBC News imerushwa muda sio mrefu
 
268211_221137191263505_100001016768117_633587_5487199_n.jpg

hatatoka tu, PINDA natafuna maneno ili iweje na mabarua iko wazi kabisa hapa
yeye alipashwa kutoa msimamo wa serikali wahache ulegelege bana
 
Ukisikia kuoza kwa nchi ndiko huko. Hivi wanafikiri sisi Watanzania tunawaangalia kwa namna gani? Je, Pinda atasema nini leo kwa watoto wake? Maana inaonekana kabisa hana madaraka amewekwa pale kama utingo wa daladala na kazi yake ni kufuata upepo hata kwenye mambo muhimu kwa taifa. Cha kujiuliza anaitetea vipi katiba aliyoapa kwamba ataitetea?
 
pinda amekana tbc kuwa hana taarifa....hahahahaaaaaaaa......anashangaa kuwa issue imelick fasta....eti anasubiri jk atue dar na atoe maamuzi.........hahaha

barua ipo na amepewa ....
 
Ukisikia kuoza kwa nchi ndiko huko. Hivi wanafikiri sisi Watanzania tunawaangalia kwa namna gani? Je, Pinda atasema nini leo kwa watoto wake? Maana inaonekana kabisa hana madaraka amewekwa pale kama utingo wa daladala na kazi yake ni kufuata upepo hata kwenye mambo muhimu kwa taifa. Cha kujiuliza anaitetea vipi katiba aliyoapa kwamba ataitetea?
Inaelekea humjui vizuri Kikwete wewe? Kwani angewaachia wenzake madaraka nchi ingeyumba namna hii? Ni kwamba Kikwete ni Rais yeye, waziri yeye, mkurugenzi yeye, balozi yeye. Kila jambo ni lazi yeye aagize na aamue. mwingine yeyote akiamua ni lawama tupu, na yupo likely kupoteza nafasi. Kwani kilichomponza Lowassa ni nini? Si hivyohivyo kujifanya na yeye ana maamuzi kama mtendaji mkuu wa serikali? Sasa yupo wapi? Hawa akina Ngeleja usione vile wanahangaika hawapati jawabu la tatizo la umeme, ni kwamba Kikwete ndiye anayesema kifanyike nini kwenye kila wizara.
 
Katibu mkuu kama anaandika barua ya kujiuzuru atamwandikia aliyemteua ambaye ni Rais, na bila shaka kupitia kwa Katibu mkuu Kiongozi. Na hawezi kuachia madaraka hadi hapo atakapopewa jibu na aliyemteua kukubali ombi lake la kujiuzuru. Kwa hiyo, Pinda yuko sahihi kutokuwa na habari kwa mujibu wa ngazi za mawasiliano zilivyo (Kama kweli hilo limetokea). Pia makamu wa Rais (ambaye ndiye Kaimu Rais) hawezi kutoa jibu kwa swala hilo hadi Rais mwenyewe awe ofisini.

Note: Haya ni maoni yangu kwa jinsi ninavyoliona suala lenyewe.
 
Jamani atajuaje?
Kwani Jairo kikazi anareport kwa nani?
 
Hakuna mabadiliko ya kweli kama CCM iko madarakani, Mpaka ife
haya yote ni maigizo muhalifu anashtakiwa au kujiuzulu?
 
Na maelektroniki yote haya bado tunamsubiri mpaka harudi! Dah kweli hii ni bongo lala! Na hizi wk 3 tatu zinasubiri mpaka atue mhe? Maana mtendaji mkuu ndo huyo uhalali wake watia shaka! Kwa mwendo huu tutafika kweli?
 
pinda hamna anachukijua< hata hiyo barua ya jairo aliijua ila akasema hajui, huyu muulizeni kuhusu ma trekta na mbolea za ruzuku tu
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom