Jairo ajiuzulu wadhifa wake

Status
Not open for further replies.
hii nchi inavichaa wengi sana inabidi tuwe tunawapima akili wabunge, madiwani kabla ya kugombea maana hili limeshakuwa nitatizo kila mara hawajui hata wanataaarifa kamili wao hawajui. viongozi wetu hawajui kwanini watanzania ni masikini na wanawaongoza kwa hilo wala sishangaai maana ndio tanzania.
 
Hilo ni dili lao wote lazima alindwe kwa gharama yoyote ile. Na si kwa wizara hiyo tu, wizara zote ndiyo mfumo wanaotumia kupitisha bajeti zao, ndiyo maana kila bajeti ya wizara fulani ikipitishwa lazima jioni yake wabunge wa CCM lazima wakeshe pale Kilimani Club wakila na kunywa kwa gharama za wizara husika ndiyo maana mibunge ya CCM piga uwa lazima ipitishe bajeti kwa kishindo ndiyoooooooooooooooo, kama mataahira vile.
 
na baraza nzima la mawaziri na manaibu waziri pamoja na makatibu wazira wote wajiuzulu mara moja......maana wana copy na ku paste...ndio maana uchumi wetu unapolomoka kwa kasi....kikwete...ngoma zito waingize zito na mbowe na silaa ndani ya serikali yako....maana wote ni watanzania tena wazalendo na wanaweza kutumikia nchi....
kikwete mwenyewe anatakiwa ajiuzulu haraka sana kwani angekua anafanya kazi kwa umakini na ukaribu na mawaziri wake yote haya yasingetokea ila anakula starehe nje ya nch kila kukicha na kuacha kila waziri ajiamulie atakalo na hawachukulii hatua yyt na hy ni dalili ya kutudharau watanzania.
 
Inaelekea humjui vizuri Kikwete wewe? Kwani angewaachia wenzake madaraka nchi ingeyumba namna hii? Ni kwamba Kikwete ni Rais yeye, waziri yeye, mkurugenzi yeye, balozi yeye. Kila jambo ni lazi yeye aagize na aamue. mwingine yeyote akiamua ni lawama tupu, na yupo likely kupoteza nafasi. Kwani kilichomponza Lowassa ni nini? Si hivyohivyo kujifanya na yeye ana maamuzi kama mtendaji mkuu wa serikali? Sasa yupo wapi? Hawa akina Ngeleja usione vile wanahangaika hawapati jawabu la tatizo la umeme, ni kwamba Kikwete ndiye anayesema kifanyike nini kwenye kila wizara.

Aah, ndiyo maana anasafiri kila nchi kwa ziara ambazo wangeweza kwenda mawaziri au wawakilishi wengine!
Kweli hii ni nchi inatawaliwa na Vasco Dagama
 
Asante nimeipenda, Inaonekana umemchunguza kitambo! Kishahada cha Uchumi alichosoma ndo kinampa kibrii hataki kusikiliza ushauri wa wataalam walibobea ktk nyanja mbalimbali!
 
Pinda kakanusha anasema labda jairo kaipeleka hiyo barua kwenye vyombo vya
habari lakini sio kwake hivo anamsubiria JK Atue bongo kutoka kwa madiba ndio ataamua ila yeye na ofisi yake
hana taarifa yeyote TBC News imerushwa muda sio mrefu

Hana taarifa kwa kuwa hajakabidhiwa yeye barua, lakini kutokuwa na taarifa haimaanishi kuwa Jairo hajajiuzulu,
tusubiri tuone uongo wao...
 
Pinda kakanusha anasema labda jairo kaipeleka hiyo barua kwenye vyombo vya habari lakini sio kwake hivo anamsubiria JK Atue bongo kutoka kwa madiba ndio ataamua ila yeye na ofisi yake hana taarifa yeyote TBC News imerushwa muda sio mrefu

ndo mchezo wao sasa hivi.........rostam mewapa barua ya kuachia nyadhifa zake lakini hawataki kusema ukweli ...

jairo kawasilisha barua leo ila pinda anakwepa labda kwa kuwa raisi hajaipitisha ila barua imefika kunakohusika
 
Nchi hii inaviongozi wenye kibuli na majivuno sana,watu wanakosea na bado wanaendelea kuwepo serikalini?katiba mpya inabidi iweke wazi adhabu ya mafisadi na wahujumu uchumi.
 
Aah, ndiyo maana anasafiri kila nchi kwa ziara ambazo wangeweza kwenda mawaziri au wawakilishi wengine!
Kweli hii ni nchi inatawaliwa na Vasco Dagama
Jamaa ameshindwa hata kukopi and paste from Mkapa. Wakati yeye Kikwete akiwa ni waziri wa mambo ya nje, safari nyingi za nje alikuwa anakwenda yeye, Mkapa alimwamini kama mwakilishi mzuri wa taifa (japo wakati mwingine inasemekana alikuwa anaacha mikutana na kwenda kujirusha na vimada). Lakini cha kushangaza yeye leo kamteua Membe kuwa waziri wa mambo ya nje, halafu mambo yote yanayohusiana na mambo ya nje anafanya yeye!! Membe ni kama sanamu tu. Kikwete ni kama hamuamini yeyote. Na hilo ndilo linalowapa wakati mgumu mawaziri wake katika suala zima la kufanya maamuzi na kufanya kazi kwa ubunifu. Kikwete ni zero kabisa.
 
Huyu jamaa asiachwe ajiuzulu hivihivi ni wakati mwafaka sasa police na takukuru wamweke chini ya ulinzi asije kukimbilia nje kama kina daudi balali, rostam aziz mwishowe tunaambiwa kafia huko ili ukweli kuhusu watuhumiwa wengine ufichwe ndani ya kapeti...jamani tanzania tuamke huyu jamaa awe chini ya ulinzi, kweli kama Polisi hawana upendeleo kuwakamata kina mbowe tu, basi mkamateni huyu jamaa kwani ushahidi upo..
 
kwa kweli hapa ni magumashi mtindo mmoja. Ni matumaini yangu kwamba ukweli utajulikana siku moja na huenda hata ngeleja mwenyewe anajua hili
 
Huu ndo ujinga aliokuwa naukataa Laila Odinga kuwa na cheo kisichokuwa na maamuzi,anashindwa kumwajibisha hata balozi wa nyumba kumi atamweza katibu wa wizara?cheo hakina thamani bali anaingiza posho tu.
 
Inasemekana TZS 1bn/- zimekusanywa, tukichukua idadi ya wabunge 320 kila mmoja angelamba 3.125m/-, Loo! Aibu sana. Mapato haramu kabisa!
 
kikwete mwenyewe anatakiwa ajiuzulu haraka sana kwani angekua anafanya kazi kwa umakini na ukaribu na mawaziri wake yote haya yasingetokea ila anakula starehe nje ya nch kila kukicha na kuacha kila waziri ajiamulie atakalo na hawachukulii hatua yyt na hy ni dalili ya kutudharau watanzania.
kila waziri angejiamulia atakalo si pinda angeshamuwajibisha jairo?
 
Kujiuzulu siyo issue, mii nataka nione jamaa anawekwa selo, kifungo miaka 30.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom