Duh! Habari mpya kutoka huko Hong Kong, China zinaeleza kuwa kama atapatikana na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya unga, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff Jack Patrick atatumikia kifungo cha miaka kumi jela.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kilikwenda kumtembelea Jack akiwa nyuma ya nondo baada ya kuruhusiwa kumuona tangu Machi mosi, mwaka huu, mwanamitindo huyo amekata tamaa na hana matumaini ya kutoka jela hivi karibuni.
Aisee Jack Cliff anatia huruma sana, hana matumaini ya kutoka hivi karibuni na ana maumivu ya kupitiliza, kilisema chanzo hicho.
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Jack anasema kuwa kesi yake ni ngumu na endapo atapatikana na hatia, basi atakumbana na kifungo, si chini ya miaka kumi, jambo ambalo limemfanya kudondosha machozi kila kukicha huku akituma salamu nyumbani kwao Bongo.
Jack alikamatwa na unga kilo 1.1 huko Macau, Hong Kong mwezi Desemba, mwaka jana ambapo sasa kesi yake itaanza kuunguruma Septemba, mwaka huu.
Afadhali kama alitoka maana alimpa kila kitu huyo bossushuz lakin alivyokamatwaa akawekwa jela huyu Jack ndio ikawa furaha kwake!! najua atafight atapata pesa tu,
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.