Mtangazaji wa kituo cha runinga cha startv Bi.Ivona Kamuntu ameeleza kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakipo katika Muungano kwa madai kuwa kimeshajitoa.
Mwandishi huyo ameyasema hayo katika kipindi cha medani za siasa na uchumi cha leo wakati akifanya mahojiano na naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia January Makamba. Amedai kuwa vyama vya CCM na CUF ndivyo bado viko katika muungano!
MY TAKE:
Kauli kama hii inadhihirisha namna waandishi wetu wa habari walivyo weupe vichwani na mara nyingine wanapojivika ukada wa vyama vya siasa badala ya kujikita katika weledi. Na Ivona leo amejipambanua wazi jinsi anavyotindikiwa weledi katika tasnia ya habari na siasa za nchi hii.
Mdau wa startv na JF
Yahya Mohamed naomba ukimpata Ivona Kamuntu umlete hapa aje kutueleza ni lini CHADEMA walijitoa katika Muungano.