Kwenye maisha ya watu wengi kuna wakati unafika unasema,
I've reached the end of the road!
Yaani unaona kabisa umefika ukomo na njia zote zimeonekana kufungwa
Mara nyingi katika nyakati kama hizo, watu hufanya maamuzi magumu na ya kutisha; maamuzi ambayo wakati mwingine huwaletea mafanikio, na wakati mwingine huwaacha na majuto ya maisha
Je, ni uamuzi gani mgumu au wa hatari uliowahi kufanya baada ya kuona huna chaguo jingine, hata kama moyoni hukupenda kuufanya?
Naanza mimi👇
MAAMUZI MAGUMU BAADA YA KUFILISIKA KWENYE BIASHARA YA MBAO.NA KUPATA MTAJI TENA.
Wakuu nilishawahi kushare kwenye reply za thread ya
ShesRise_1 jinsi nilivyofilisika kwenye biashara ya mbao.
Hivyo hapa tutaendelea nilipoishia na maamuzi ya kuanza upya.
Baada ya kupoteza fedha za biashara niliamua kwenda wilaya nyingine asiyonifahamu mtu yeyote. Nilifanya hivyo ili kutuliza akili na kujipanga upya.
Nilikaa gesti kuja kushtuka kwenye akaunti nimebakiwa na elfu 60 tuu. Nikachukua maamuzi ya kutafuta geto na kulala chini tuu.
Mungu mwema nikipata geto la 15k kwa mwezi umeme upo na maji ya kisima. Katika hilo geto niliukuta mkeka hivyo nikapata Cha kutandika chini ila chakujifunika ilikua shuka la kimasai na msimu ulikua ni wa mvua😂😂😡. Wilaya ilikua na baridi sana lakini ndio hivyo sikuwa na njia mbadala.
Maisha ya geto yakaanza, msosi wa kununua ukanishinda maana uchumi ulikua umeshanikataa. Nikachukua maamuzi magumu ya kuanza kupika😔😔💔
Nikanunua kigai Cha mkaa na sufulia 2 😂😂😂. Haya maisha nilikua sijayazoea kabisa hivyo kama kuteseka ndio nilianzia hapa.
Nilikua nakula mara Moja Kwa siku ili kupunguza gharama ya chakula, pia nilikua naona uvivu sana kuwasha mikaa. Hivyo Kuna kipindi ilifikia napika pilau ya kula siku 3😔😔😔, nakula kiporo tena ambacho hakijapashwa. Kupika pilau haikua maisha bora kwangu Bali ilikua ni kupunguza gharama ya mboga pia ili nisichoke kula chakula kimoja siku3 mfululizo.
Hayo makosa ya kujipikia ndio yaliyosababisha nikakosa baadhi ya vitamins mwilini ambazo zilinipelekea kutaka kupalalaizi😔😔💔. Mungu ni mwema nilishuka mapema nikapata vidonge pia nikashauliwa kula nyama, samaki, mayai ndio Hali ikanirudia poa.
Nilikaa katika mazingira hayo kwa miezi mitatu. Katika muda huo niliishi kwa kukopa na kudai madeni yangu kwa watu.
Kuna siku nikafikia maamuzi magumu, nikajiambia moyoni kuanzia Leo sitakopa tena Hela ili nipate chakula, kama Mungu ameamua nidhalilike au nife bhasi ni bora nife kuliko kujiaibisha kwa namna ya kukopakopa Hela.
Kweli niliweka huo msimamo na msosi ulivyoisha niliamua kukaa tuu huku nikisubiri wadeni wangu wanilipe.
Aisee! Maisha yalikua magumu zaidi😔 maana nilikua nafunga bila maombi na kufungua nakunywa maji na kulala🥺. Ikafikia kipindi uvumilivu ukanishinda nikawa naenda kupita kwenye mashamba waliovuna mahindi naokota yale mabaki naenda geto kukaanga bisi ndio kinakua chakula changu.
Mungu ni mwema kuna siku mdeni wangu akanilipa kama laki6, Aisee! Ile Hela iliisha katika hali ambayo sikuielewa na ni ndani ya wiki mbili tuu.
Baada ya hiyo fedha kuisha nikaja na wazo jingine kwamba kwasasa, nikipata fedha inabidi nikajaribu maisha mengine kwenye migodi ya dhahabu. Hivyo katika maamuzi haya nilisali sana nikamkabidhi Mungu mipango yangu.
MAAMUZI MAGUMU YA KWENDA MGODINI.
Kuna siku nilimpigia mdeni akaniambia tarehe fulani nitakulipa 150k. Nikasema hii fedha itanitosha kufika huko na kuanza life na mengine yatajulikana mbele ya safari. Kweli tarehe ilipofika nikaingiziwa
Gharama ya nauli mpaka kufika ilikua 40k, nikanunua begi 20k, 30k nikaweka emergency na 50k ndio nikasema itanisukuma siku mbili tatu nikifika huko.
Mipango sio matumizi😂😂😂💔, hiyo 50k ilikatika kabla hata sijapanda gari, sababu kubwa ya kupoteza hiyo fedha ni uzi*nz*😡😡😡💔. Hapa nilipata funzo kubwa sana la majuto, kitu ambacho kilinisaidia sana nikiwa mgodini, wanawake niliwaona kawaida sana.
Kesho yake asubuhi nilipanda gari kuelekea mgodini.
MAKOSA YENYE FAIDA
Kutokana na nilipokua nakwenda sipafahamu, hivyo nilikata tiketi ya linapoishia gari.
Ndani ya gari nakutana na abiria mwenzangu tumwite Japhet.
Mimi: naitwa Zirlovimovic Zirkov, natokea mkoa X nakwenda kwenye machimbo japo sikufahamu na sijawahi kufika.
Japhet: Anhaa!sawa, lakini kama unakwenda kwenye machimbo ni bora ukashukia sehemu X, Y au Z maana huko unakokwenda hakuna machimbo kabisa lakini pia kutokana na hali yako ni ngumu sana kupata vibarua kwasasa maana shughuli za huko ni za msimu tuu.
Mimi: Sawa, kwasababu nimeshakata tiketi ya huko bhasi ngoja nifike alafu nitajua Cha kufanya huko huko.
Safari ukiendelea huku nikipiga story za maisha na Japhet, Japhet alitokea makao makuu ya nchi akiwa na mke wake pamoja na mtoto wake. Safari yake ilikua ya kikazi alinionesha picha alizompiga rais na viongozi wengine wengine.
Tunafika Kijiji Y, gari inasimama muda mrefu sana. Namuuliza Japhet hapa panaitwaje?
Japhet: Hapa panaitwa Y, hapa ndio Kijiji Cha mwisho wanachochimba madini huko mbele hutoona mgodi wowote.
Mimi: Anhaa nashukuru sana.
Safari inaendelea na tunafika mwisho wa gari, Mimi tunaagana na Japhet na nachukia namba yake kwamba tutawasiliana endapo mambo yatakaa poa ili nipate kutumia fursa za kijijini hapa.
Baada ya kuagana na Japhet ilikua ni mida ya saa12 jioni, njaa inauma lakini pia ninauchovu mkali sana.
Nikawaza nipate chumba Cha elfu5 nitue begi langu lakini pia nipumzike na uchovu maana usiku sikulala lakini pia safari imenichosha sana.
Natembea mwendo wa kama mita700 naona kibao Cha gesti lakini nikijipima naona haya maji siyawezi. Nikamfuata dogo
Mimi: Oyaa! Mambo aje mdogo wangu?
Dogo: Poa bro ni kwema?
Mimi: Uhakika dogo, hivi hapa napata wapi gesti ya 5k kushuka chini?
Dogo: Daah! Bro toka nipajue hapa sijawahi kuona gesti ya bei hiyo. Gesti ni kuanzia buku7
Mimi: Bhasi sawa, napata wapi hiyo gesti.
Dogo: Hapo uliposhukia na gari.
Narudi mpaka stendi ya mchongo sioni kibao chochote Cha gesti😳. Naamua kumfuata mtu, Bro mambo aje? Nataka chumba Cha bei chee hapa.
Jamaa: Anhaa usijali bro, twende nikuoneshe.
Tukaenda mpaka maeneo, nikaoneshwa ila sikuridhika nacho ikabidi nisepe. Jamaa akanipeleka sehemu nyingine.
Duuh! Hapo ndio palikua pa hovyo kuliko unavyodhania, Yaani ukuta ni ceiling board, alafu nayo imetoboka, milango ni imechoka inabidi uunyanyue upande ndio uufunge. Umeme vyumbani hakuna😳😳😳💔
Nikatoka kurudi chumba Cha kwanza, naambiwa chumba kimeshachukuliwa💔💔😔.
Nikarudi pale kwa ovyo zaidi, nikalipia elfu 7 yangu nikazama chumbani, weka begi langu na kutoka nje kula.
Baada ya kula nikanunua maji yangu makubwa.
Nafika geto najisachi mfukoni, najikuta nimebakiwa na Tsh 17,500/= tuu
Usiku niliwaza na kutafakari mengi, mawazo yangu makubwa ni kesho naanzia wapi au nifanye kitu gani hapa? Wazo la mwisho lilikuja kwamba nifuate kilichonileta ambacho ni kwenda MGODINI.
Asubuhi nilishtuka kama saa12, nikaenda kwa mhudumu weka simu chaji, nikarudi kulala huku nikiwaza niende sehemu ipi ya mgodi?
Ilipofika saa3 asubuhi, nikapaki begi langu vizuri tia na maji yangu kwenye begi. Tayari kwa safari ya kwenda MGODINI.
Kwasababu pale tuliposimama na gari muda mrefu niliona mazingira yake, bhasi nikasema nitaenda kwanza pale nikajaribu life.
Safari ya kwenda Kijiji Y inaanza.
Nilitembea umbali wa kama kilometer 1 ndio naikuta stendi na gari ilikua inatoka. Hivyo Nikadandia
NDANI YA GARI NAKUTANA na KONDA MBABE ALINISHUSHA KWENYE GARI😔😔
Salange ndio alikua anakusanya nauli
Salange: Nauli hapo bro
Mimi: Kijiji Y bei gani?
Salange: Elfu 7
Mimi: Nikakunja ngumi kumaanisha Nina elfu 5
Salange: Hapana bro, maliza yote.
Mimi: Nikamfuata salange, kumueleza hali yangu😂😂 maana nilikua nimesimama karibu n mlango.
Salange: Poa, ngoja nibonge na konda.
Salange: Konda amegoma mwanetu hivyo wewe maliza tuu.
Mimi: Sina zaidi ya hiyo😎😎😎
Konda: Big hiyo nauli haipo, labda tukushushe mbele.
Mimi: Kimoyomoyo kwa kuwa hanifahamu mtu Sawa tuu.
Nikashushwa kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea Kijiji Y kwa miguu. Kufupisha story
Nilitembea kuanzia saa4 asubuhi mpaka saa12 jioni pasipo kupumzika na jua lilikua Kali sana lakini Mungu alinitetea.
Njiani nilikutana na madogo wawili wanaenda kijijiY pia kumsalimia mama Yao. Hivyo nililngozana na hawa madogo mpaka mgodini na mama yao ndiye alinipokea nikakaa kwenye kambi yake siku 5.
Inshort mambo mengi yalitokea lakini Mungu alinishinishindia.
Mara ya kwanza tuliokota mawe na mwenyeji wangu, mume wa huyo mama. Aisee! Tukitumia siku3 kukusanya mawe mpaka kusaga alafu tukapata elfu kumi kama elfu kumi😂😂😂😔😔💔💔😡.
Ukapita mgao wa elfu 5 kwa 5.
Naamua kuanza kuchimba pekeeangu, kweli baada ya kazi ngumu na ya kuchosha na malipo yake kuwa elfu 5, niliumia moyoni ila nikapiga moyo konde.
Nilizunguka kwenye lile shamba ili kupata sehemu ya kuanza kuchimba, baadae nikajikuta nachimba sehemu moja hivi. Kulikua hakuna mtu anaechimba hapo.
Bhasi nilianza kuchimba na baadae nikaanza kuyakuta mawe. Mind you mimi kimuonekano naonekana kama mtu fulani soft sana, alafu mayai mayai, lakini ukweli wangu naujua mimi mwenyewe.
Kutokana na muonekano wangu, watu wengi walikua kama wananichukulia poa kama nitaiweza kazi ya kuchimba. Bhasi mimi sijali lolote nafanya kile kilichonileta.
Baada ya kutoa mawe mengi watu ndio wakaanza kunisifia, mawe yako mazuri, sijui Nini na Nini. Mimi sijali
Watu wanaanza kupiga sample mawe yangu, baada ya kuchimba nilikua nayakusanya sehemu Moja. Kuna mawe yalikua yanaonesha vidhahabu hivyo nilikua nayafukia chini ya yale mawe mengine.
Kutokana na watu kukagua mawe yangu ikabidi nisage tuu. Nilisaga mizunguko miwili nikakamatisha na kukamua nikapata dhahabu gram 1.6 ambayo ilikua sawa na Tsh 367,000/=
Baada ya kupata hicho kiasi ilikua ni kama nimetangaza vita. Nilipokua nakaa ikabidi nihame maana wao ndio walikua watu wa kwanza kuonyesha chuki zao.
Pale nilipokua nachimba pakazingirwa, Yaani hata njia ya kufika duarani kwangu nikawa Sina.
Nikawaonesha upande wangu wapili wa shilingi. Wale wote waliokuwa wanachimba jirani nikawachana kwamba waondoke na pia sitaki mtu achimbe kwenye shimo langu na ukijiona wewe ni kiburi sana bhasi ingia nikutie sululu ya kichwa. Toka hapo heshima ikawepo.
Story kuwa fupi nilichimba mpaka mita8 kwenda chini ndio nikapata mtu wa kunisaidia ambaye ni John. Huyu jamaa nilimpigia simu aje tufanye kazi tena na nitakuwa namlipa 600k kwa mwezi japo sikuwa na uhakika wa kupata hiyo fedha😂😂😂
John alikuja tulifanya kazi kwa pamoja na tukaufikia MWAMBA, urefu wa duara ulikua MITA 10 na zaidi kwenda chini, hivyo Mimi ndio nilikua naingia chini na John anabakia juu kwaajili ya kuvuta udongo na mawe.
Mwisho namshukuru Mungu aliniwezesha kupata milioni 20+ ndani ya miezi miwili nikiwa mgodini.
Hayo ndio yalikua maamuzi magumu kwangu na Mungu alinishinishindia. The rest is history